Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Bi.. mdogo, unaweza kuwa na point hapa.... ila huyo si alikuwa na BM? lakini sijasikia akihusishwa na ufisadi ila kama ulivyoashiria amebakia kufungua "migahawa na mabucha"...
MWK, hilo neno incapacitated hapo nadhani litaleta mgogoro hapa...kuwa na maana inayokubalika, na ambayo kwayo JK anaweza kufit ili kuhalalisha makamu wa rais 'kuchukua nchi'.
Nadhani wataalam wa sheria wangetupa hasa ni mazingira gani tunaweza kusema kuwa rais amekuwa incapacitated?
Mnatufanya wengine tuumie kwa kucheka, mzee wa mikasi, hiyo ni ya kufungulia mwaka. Huyu mtu hata sijui umpe definition gani, maana huwezi hata jua kama ana-play safe au namna gani. Hivi amewahi kuchukua uamuzi gani wa kuonyesha kwamba naye yumo, au ule wa kupiga marufuku mifuko ya sandarusi!
Mnatufanya wengine tuumie kwa kucheka, mzee wa mikasi, hiyo ni ya kufungulia mwaka. Huyu mtu hata sijui umpe definition gani, maana huwezi hata jua kama ana-play safe au namna gani. Hivi amewahi kuchukua uamuzi gani wa kuonyesha kwamba naye yumo, au ule wa kupiga marufuku mifuko ya sandarusi!
NT,
jaribu tu hata wewe mwenyewe kufikiria tafsiri na matumizi ya neno incapacitated na kisha ulinganishe anachofanya Kikwete sasa hivi kwenye issues za Buzwagi, Bandari, Richmonduli, Kiwira, rada, Benki kuu, kampuni ya reli, ....... kisha uunganishe fact kuwa Kikwete anazidi kutoa muda tu kwa kamati za kuchunguza kamati za kuchunguza tume za kuchunguza kamati iliyochunguza tume ili kamati ichunguzwe na..... huku Karamagi akiongezewa mkataba wa kufanya uvundo bandarini..... nimechanganyikiwa na nitakuwa dissapointed kama hili halifit tafsiri ya hilo neno!
incapacitated
sawa haya nnndio ya kuleta jamvini?
basi wana africa wamemwengeza cheo cha kusimamia umoja wa wana africa
Incapacitated ni pale ambapo mtu yeyote anapokuwa mgonjwa kiasi cha kutoweza kufanya shughuli yoyote. Mfano ni wazir mkuu wa zamani wa Israel Arien Shalon amabaye aliugua na akawa "Totally incapacitated" hadi leo hii ninapoandika hapa. This if from medical point of view. From law or political point of view, wanaofahamu watueleze inakuwaje.
Tulishakwambia hata Idd Amin pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa OAU. Sifa pekee kubwa ya kuwa mwenyekiti wa Au ni kuwa Head of State wa nchi yoyote aliye mwanachama, so...
Mheshimiwa sana Dk Shein,
Naomba nichukue nafasi hii kwanza kwa kukupongeza kwa kazi nzuri sana unayofanya ya kufungua majengo, vituo, maduka ya nyama na biashara mpya katika nchi. Samahani kidogo kwa kuiita hii kazi yako kwa jina la kazi ya mikasi. Pamoja na haya, natoa wito maalumu kwako na kwa ofisi yako kulinusuru taifa letu tukufu la Tanzania.
Ninakumbusha jambo unalolielewa vyema kabisa kuwa kikatiba wewe una ruhusa ya kufanya kazi ya uraisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pale mambo fulani fulani yanapojitokeza. Moja ya mambo hayo ni pale rais wa nchi anapokosa uwezo wa kutenda kazi zake kikamilifu (incapacitated). Najua wataalamu wa sheria na lugha watatumia tafsiri mbalimbali kuelezea hili neno incapacitated lakini kwa mtizamo wangu na watanzania wengi, Rais Kikwete kwa sasa anafit kabisa definition hii ya kukosa uwezo wa kutenda kazi zake kwa ukamilifu.
Ninakuandikia hili huku nikikumbuka maneno ya mtanzania mmoja aliyewashauri watanzania kwenda kunywa chai na Kikwete kama walipenda sura yake au tabasamu lake. Kazi ya uraisi ni kubwa kuliko Kikwete alivyofikiria na inawezekana ameshindwa tu kusema hili wazi. Kwa vile mkuu wako wa kazi sasa ameshindwa kazi yake na anapeleka taifa la Tanzania kubaya, ni jukumu lako kutimiza kiapo ulichoapa kuwa utachukua kazi ya urais na kufanya kazi yako kwa maadili pindi itakapothibitika kuwa raisi hana uwezo tena wa kufanya hivyo.
Chonde chonde Mheshiwa Shein, nchi yote inakuangalia wewe kufanya the right thing kipindi hiki cha mpito ambacho wanaccm wakifikiria nani wampitishe katika uchaguzi mkuu 2010. Tafadhali sana ikomboe nchi hii kwa kuchukua madaraka ya nchi toka kwa Kikwete na kuzuia zahama inayolikabili taifa la watanzania. Kumbuka kuwa watanzania wengi wamechoshwa na wizi huu unaondelea usiku na mchana wakati nchi ikiuzwa kwa wageni kama njugu.
Ahsante sana na ubarikiwe kwa uamuzi huu unaotakiwa kuufanya haraka sana.
Asante
Mwafrika Wa Kike ..brilliant..shein Is Much Far Better...alafu Jamaa Kina Jk Wana Mu Undermine Sana Nim Kama Hana Kazi Ya ,maana......