Ombi maalumu kwa makamu wa Rais - Shein | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi maalumu kwa makamu wa Rais - Shein

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwafrika wa Kike, Feb 1, 2008.

 1. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa sana Dk Shein,

  Naomba nichukue nafasi hii kwanza kwa kukupongeza kwa kazi nzuri sana unayofanya ya kufungua majengo, vituo, maduka ya nyama na biashara mpya katika nchi. Samahani kidogo kwa kuiita hii kazi yako kwa jina la kazi ya mikasi. Pamoja na haya, natoa wito maalumu kwako na kwa ofisi yako kulinusuru taifa letu tukufu la Tanzania.

  Ninakumbusha jambo unalolielewa vyema kabisa kuwa kikatiba wewe una ruhusa ya kufanya kazi ya uraisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pale mambo fulani fulani yanapojitokeza. Moja ya mambo hayo ni pale rais wa nchi anapokosa uwezo wa kutenda kazi zake kikamilifu (incapacitated). Najua wataalamu wa sheria na lugha watatumia tafsiri mbalimbali kuelezea hili neno incapacitated lakini kwa mtizamo wangu na watanzania wengi, Rais Kikwete kwa sasa anafit kabisa definition hii ya kukosa uwezo wa kutenda kazi zake kwa ukamilifu.

  Ninakuandikia hili huku nikikumbuka maneno ya mtanzania mmoja aliyewashauri watanzania kwenda kunywa chai na Kikwete kama walipenda sura yake au tabasamu lake. Kazi ya uraisi ni kubwa kuliko Kikwete alivyofikiria na inawezekana ameshindwa tu kusema hili wazi. Kwa vile mkuu wako wa kazi sasa ameshindwa kazi yake na anapeleka taifa la Tanzania kubaya, ni jukumu lako kutimiza kiapo ulichoapa kuwa utachukua kazi ya urais na kufanya kazi yako kwa maadili pindi itakapothibitika kuwa raisi hana uwezo tena wa kufanya hivyo.

  Chonde chonde Mheshiwa Shein, nchi yote inakuangalia wewe kufanya the right thing kipindi hiki cha mpito ambacho wanaccm wakifikiria nani wampitishe katika uchaguzi mkuu 2010. Tafadhali sana ikomboe nchi hii kwa kuchukua madaraka ya nchi toka kwa Kikwete na kuzuia zahama inayolikabili taifa la watanzania. Kumbuka kuwa watanzania wengi wamechoshwa na wizi huu unaondelea usiku na mchana wakati nchi ikiuzwa kwa wageni kama njugu.

  Ahsante sana na ubarikiwe kwa uamuzi huu unaotakiwa kuufanya haraka sana.

  Asante
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Bi.. mdogo, unaweza kuwa na point hapa.... ila huyo si alikuwa na BM? lakini sijasikia akihusishwa na ufisadi ila kama ulivyoashiria amebakia kufungua "migahawa na mabucha"...
   
 3. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Badala ya kuwa na power vacuum, Shein anaweza kuongoza serikali kwa mpito hadi uchaguzi mwingine ufanyike. Shein pia anaweza kuwa chaguo zuri zaidi kuliko Mwamunyange au afande mwita marwa wa kikosi ....... kule ........
   
 4. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MWK, hilo neno incapacitated hapo nadhani litaleta mgogoro hapa...kuwa na maana inayokubalika, na ambayo kwayo JK anaweza kufit ili kuhalalisha makamu wa rais 'kuchukua nchi'.

  Nadhani wataalam wa sheria wangetupa hasa ni mazingira gani tunaweza kusema kuwa rais amekuwa incapacitated?
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  Feb 1, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mnatufanya wengine tuumie kwa kucheka, mzee wa mikasi, hiyo ni ya kufungulia mwaka. Huyu mtu hata sijui umpe definition gani, maana huwezi hata jua kama ana-play safe au namna gani. Hivi amewahi kuchukua uamuzi gani wa kuonyesha kwamba naye yumo, au ule wa kupiga marufuku mifuko ya sandarusi!
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  NT,

  jaribu tu hata wewe mwenyewe kufikiria tafsiri na matumizi ya neno incapacitated na kisha ulinganishe anachofanya Kikwete sasa hivi kwenye issues za Buzwagi, Bandari, Richmonduli, Kiwira, rada, Benki kuu, kampuni ya reli, ....... kisha uunganishe fact kuwa Kikwete anazidi kutoa muda tu kwa kamati za kuchunguza kamati za kuchunguza tume za kuchunguza kamati iliyochunguza tume ili kamati ichunguzwe na..... huku Karamagi akiongezewa mkataba wa kufanya uvundo bandarini..... nimechanganyikiwa na nitakuwa dissapointed kama hili halifit tafsiri ya hilo neno!
   
 7. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nadhani akichukua uraisi wa nchi kwa kipindi hiki cha mpito labda atazuia bleeding na kuiandaa nchi kwa rais mwingine kwani Tanzania haiwezi kuafford miaka yote ya Kikwete ikulu- ila kazi ya uwaziri wa michezo na utamaduni inaweza kumfaa sana Kikwete.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahaha guys spare my ribs!!!....Mzee wa watu jamani anaimarisha Muungano si ni mpemba yule?
   
 9. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MwK:
  Wengine tulishasema kuwa sasa tunamwonea huruma JK, hata huko kumsuta imebidi tunyamaze.
  Hapana, JK angeweza kujijengea heshima kubwa sana kama angeanza tu na kuwasambaratisha mashetani wanaokishikiria chama cha CCM, hata bila kufanya lolote katika haya uliyoyataja hapo juu. Yeye angemruhusu tu Shein asimamie shughuli za kila siku za serikali (hata ikiwa tu kwa maelewano kati yao binafsi bila ya kuwaelezea wananchi), halafu yeye Kikwete kama Mwenyekiti wa 'Chama Kilichooza' ajikite katika kukisafisha uchafu wote kabisa. Angehitaji tu miezi sita kuifanya kazi hiyo kwa ustadi kabisa na kuikamilisha. Lakini, aaaah, tunasikitika na kushangaa huyu ndugu yetu ni matatizo yapi yanayomsibu? Au ndio 'Alzheimer' hiyo inamuanza? Hana tofauti na mtindo aliokuwa akiutumia Kenyatta wakati wa mwisho mwisho wa utawala wake! Yeye yupo yupo tu!
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwafrika wa Kike,

  Thank you my dear for this. Hii ni wazi kuwa Taifa letu lipo hatarini na tunaomba kila mtu achangie kuliokoa taifa.

  Jemedari na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete hana uwezo kutangaza vita, hana uwezo kutumia dhamna ya madaraka yake kwa mujibu wa katiba.

  Shein, yakhe twakuomba tuokoe ati, maana twasikia Mamvi naye anavizia kiti cha enzi!
   
 11. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Incapacitated ni pale ambapo mtu yeyote anapokuwa mgonjwa kiasi cha kutoweza kufanya shughuli yoyote. Mfano ni wazir mkuu wa zamani wa Israel Arien Shalon amabaye aliugua na akawa "Totally incapacitated" hadi leo hii ninapoandika hapa. This if from medical point of view. From law or political point of view, wanaofahamu watueleze inakuwaje.
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sawa haya nnndio ya kuleta jamvini?

  basi wana africa wamemwengeza cheo cha kusimamia umoja wa wana africa
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  incapacitate
  Main Entry: in·ca·pac·i·tate [​IMG] Pronunciation: \ˌin-kə-ˈpa-sə-ˌtāt\ Function: transitive verb Inflected Form(s): in·ca·pac·i·tat·ed; in·ca·pac·i·tat·ing Date: 1657 1 : to make legally incapable or ineligible 2 : to deprive of capacity or natural power : disable
  - in·ca·pac·i·ta·tion [​IMG] \-ˌpa-sə-ˈtā-shən\ noun
   
 14. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #14
  Feb 1, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tulishakwambia hata Idd Amin pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa OAU. Sifa pekee kubwa ya kuwa mwenyekiti wa Au ni kuwa Head of State wa nchi yoyote aliye mwanachama, so...
   
 15. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  nadhani kuna tafsiri zaidi ya hii mkuu! the magic word hapa ni -able kama alivyoiweka Rev hapo juu!
   
 16. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nakuambia hii issue ya AU itakuwa justification ya kufanya ufisadi mwaka huu hadi watu wale nyasi!
   
 17. m

  mtambo Senior Member

  #17
  Feb 2, 2008
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kali sina la kusema.
   
 18. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MIMI SI MWANA-CCM LAKINI NILIWAAMBIA KUWA CCM NI CHAMA BORA NA IMARA KULIKO VYAMA VYOTE VYA SIASA HAPA NCHINI. (This is the fact). YATOKANAYO HAPA NI KAMA KIHORO AU KIWEWE CHA KUIONA CCM HAITETEREKI.
  I WISH NINGEKUWA KATIKA CHAMA CHENU HALAFU NIKALETA MABADILIKO.
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Feb 2, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Mwafrika Wa Kike ..brilliant..shein Is Much Far Better...alafu Jamaa Kina Jk Wana Mu Undermine Sana Nim Kama Hana Kazi Ya ,maana......
   
 20. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bado narudia hili ombi maalumu kwa mheshimiwa Shein.
  Tafadhali inusuru nchi yetu na haya yanayoendelea angalau kwa miaka mitatu iliyosalia!
   
Loading...