Ombi Maalum kwa wale ambao tunawacheka na kuwadhihaki hapa JamiiForums Wabunge Viti Maalum CHADEMA

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Naona Watu wengi (Members) hapa tunawasema, tunawacheka, tunawadhihaki hadi kuwatukana huku tukiwaambia sijui wamenunuliwa na wana Njaa sana. Sitaki Kuwakatalia au Kupinga haya Maneno yenu Kwao hawa Wabunge Viti Maalum CHADEMA kutokea BAWACHA, ila GENTAMYCINE nina Ombi moja Maalum tu Kwenu na nitafurahi mkilitekeleza haraka tu hapa Jamvini.

Nawaombeni wale Wote ambao mnawacheka, mnawadhihaki na kuwaambia akina Mdee, Bulaya na Wenzake kuwa wana Njaa na wamenunuliwa au kuahidiwa Vyeo nanyi mtuwekee hapa Majina yenu halisia (siyo haya Fake na hizi ID's zetu) ili na Sisi wanaotujua vyema waweze kusema kama tuna njaa au hatuna ili tuweze pia Kuwatendea Haki hawa Wabunge Viti Maalum CHADEMA.

Kitu pekee tu ninachoweza kusema na tena nina uhakika nacho kwa 99.999% ni kwamba kwa hali ya Msoto ( Maisha Magumu ) hasa ya Kipato tuliyonayo Watanzania wengi wengi Wetu Zali hili au Mchongo huu wa kwenda Bungeni na Kupata Pesa pamoja n kile Kiinua Mgongo wala tusingekiacha na tungesalitiana tu. Cheza na Vitu vyote ila siyo Njaa. Tuacheni Unafiki katika hili.

Wabunge wote wa Viti Maalum CHADEMA kutokea CHADEMA hata Mimi GENTAMYCINE ningewashangaa mno kama mngeziachia Pesa za Bwerere kisha muanze Kusota na Kupigiana tu Miayo hapo Biafra Kinondoni na Mwenyekiti wenu Taifa Mbowe huku Tundu Lissu akipumzika zake tu huko Ulaya na Wazungu wakimlisha, wakimlipa na wakimtunza vile vile.

Watanzania (Waswahili) tumekuwa wepesi sana Kulaumu na Kuhukumu mno wakati tumesahau kuwa kwenye Njaa Unafiki na Usaliti hushirikiana.
 
Issue hapa siyo kwamba wamekubali hivyo viti bali wamevipatapataje. Kama njia ya kuvipata siyo halali basi ina maana hawastahili kuwa hapo walipo. Kama unataka kuhalalisha wizi kwa ajili ya njaa basi kuna mambo mengi tu hatuna haja ya kuyajadili hapa including Uchafuzi Mkuu uliopita na CCM kushinda kwa kishindo!!

Kumbuka kuwa kuna watu kibao mtaani wana njaa ila hawatumii njia halamu kujipatia maisha yao ya kila siku!!
 
Wakati mwingine ficha upumbavu wako.
Kama na wewe umenunuliwa kwa kuvuliwa vyupi ungana na hao wasaliti wenzako na jitaje jina halisi humu.
Unataka kutetea ujinga wakati unajua cdm wana katiba inayoeleza taratibu zote zilivyo.
Hata hivyo kama syo Lisu na kina mbowe hao mbwa wako wasaliti hivyo viti 19 wasingepata hata kimoja.
Shenzi wewe na wao
 
Kwani jamani tatizo liko wapi? Wenzetu wanawake wanasema kama hivyo viti maalumu vingewahusu hata wanaume, basi ungeshangaa na wanaume wangekupo kwenye list. Sisi tuache wande kufanya kazi bungeni kama tukiwafukuza Chadema najua wataenda mahakamani na watapiga miaka yao 5- mitano mwisho wa siku kundi lote hili tutawapoteza - watajiunga na vyama vingine period. Hawana cha kupoteza.
Shida yangu najiuliza ruzuku ya hawa wabunge itakwenda chama gani wakati tumeshaamua kuwafukuza nayo tutaikosa.
 
Back
Top Bottom