Kuhusu Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee: Mambo yako wazi ila wahusika wako kimya

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Mwanzo mwanzoni niweke wazi, kama ilivyo kawaida yangu, kuwa mimi si mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini au nje ya nchi hii. Nikiongozwa na uzalendo na utanzania wangu, huwa naunga mkono hoja zozote za kuujenga utaifa wetu na kuleta maendeleo ya Tanzania yetu. Natazama hasa mantiki na uzito wa hoja bila ya kujali ameisema nani na ni wa chama gani.

Pili, naomba kumpa pole Ndugu Jesca Kishoa kwa 'kulazimika' kufuta kauli yake kuwa 'alishaondolewa CHADEMA' ili kulinda Ubunge wake pale alipobanwa na kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika Daktari Tulia Ackson Mwansasu. Kishoa ni kama aliteleza katika kusema hivyo na akaifuta kauli yake 'kinyonge na kwa huruma' sana. Kuna wakati siasa huutweza hata utu angalau tu mambo yaende.

Hoja yangu hapa ni kuanika baadhi ya 'facts' ambazo zitaonyesha kuwa sakata la Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee liko wazi ila wahusika wanajifanya kutoona na hivyo kulinyamazia. Fuatana nami hapa ujionee yaliyo ya wazi;

Mosi, akina Halima Mdee walishtakiwa na KUFUKUZWA UANACHAMA na kilichokuwa chama chao cha CHADEMA. Mchakato wa hilo na UAMUZI huo ulitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika na hata Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikaeli Mbowe. Sitaki hapa nizungumzie utaratibu uliofuatwa kufikia UAMUZI huo kwakuwa sisi wafuatiliaji hatuna ushahidi juu ya hilo la utaratibu.

Pili, akina Halima Mdee walitangaza kukata rufaa ndani ya CHADEMA kupinga UAMUZI huo. Hadi hapa iko wazi kuwa kuna UAMUZI uliotolewa na CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee na huo UAMUZI ndiyo uliokatiwa rufaa na wahusika hao. Ifahamike pia kuwa UAMUZI huo unawafanya akina Mdee KUTOKUWA WANACHAMA wa CHADEMA hadi pale utakapobadilishwa na mamlaka ya rufaa ndani ya CHADEMA.

Tatu, katika uga wa kisheria, KUKATA RUFAA hakufuti UAMUZI uliofikiwa hadi pale rufaa itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi mwingine. Ndiyo kusema, kuanzia siku ya KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee, UAMUZI ule umebaki hata sasa. Ni kwamba, wote WALIOFUKUZWA UANACHAMA, si wanachama wa CHADEMA. Wanachopambania kwenye rufaa zao ni KUREJESHEWA UANACHAMA WAO ndani ya CHADEMA. Kama wao kwasasa ni wanachama wa CHADEMA, wamekata rufaa ili kupata uamuzi upi tena?

Nne, nakubaliana na Naibu Spika Daktari Tulia (alipokuwa akimueleza Jesca Kishoa Bungeni) kuwa kwa mujibu wa Katiba kila Mbunge lazima atokane na chama cha siasa. Tena, kupoteza UANACHAMA wa chama cha siasa ni kupoteza nafasi yoyote ya kisiasa ya kuchaguliwa kama Ubunge na Urais. Natofautiana na kaka na mtani wangu Pascal Mayalla aliyeandika humu JF kuwa Mbunge ANAPOTEULIWA hawezi kuondolewa na chama chake. Chama cha siasa kinaweza kumfukuza mwanachama wake na uongozi unakomea hapo.

Tano, akina Halima Mdee, kuanzia siku ya UAMUZI wa CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA, hawakupaswa kuendelea kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu iko wazi: SI WANACHAMA wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania kuwawezesha kuwa Wabunge wa Viti Maalum. Sikugusia mchakato wa kupatikana kwao kwakuwa sina ushahidi nao. Nazungumzia kilichotokea baada ya wao kutangazwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Wahusika wanaujua ukweli huu lakini wamekuwa kimya. Fedha za umma zinaendelea kuwalipa wasio Wabunge. Kulingana na Naibu Spika, Ofisi ya Spika haina TAARIFA YA KUFUKUZWA UANACHAMA WA CHADEMA kwa akina Halima Mdee. Hili lina ukweli gani? Linabadilije UAMUZI wa CHADEMA? Tuwe wakweli katika hili na kutenda yatupasayo kutenda kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi yetu.
 
Historia inaonyesha hawa siyo wabunge wa kwanza kufutiwa uanachama na hata hao wa mwanzo walivyofutwa uanachama na vyama vyao walikingiwa kifua na Spika na au mahakama.

Hili linatakiwa liwe funzo kwa sisi watazamaji na ambao ni wanachama wa vyama vya siasa.
 
Iliwahi kutokea kwa CUF pia lakini hii ya Chadema ni tofauti.

Akina Halima James Mdee na wenzake hawana uhalali wa kuwa bungeni tokea day one.

Mtu katoka jela usiku asubuhi anakuwa mbunge hicho ni kituko cha karne na aibu kubwa kwa mbunge mwenyewe ( kama ni mtu) na waliomuingiza!
 
Wahusika wakuu wa sakata hili ni mwendazake, Ndungai, Mitungi na Kitengo.
Ongezea na NEC.

Ndio maana suala limekuwa gumu. Kibwengo alipora kila kitu kwa tamaaa.

Pesa za mabeberu alitaka na viti vyote vya majimbo alitaka.

Hapo kina Halima wanalindwa lindwa ili angalau hao Mabeberu watoe hizo trilioni 2 lakini hakuna asiyejua kuwa kina Halima siyo wabunge halali.
 
Wakati wa uchaguzi mawazo ya mwendazake yalikua kwenye mitano ya nyongeza. The consequence came after and he over rode.
 
Yule kibwengo hakuwa na akili kabisa.
1619507464468.jpeg
 
Mwanzo mwanzoni niweke wazi, kama ilivyo kawaida yangu, kuwa mimi si mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini au nje ya nchi hii. Nikiongozwa na uzalendo na utanzania wangu, huwa naunga mkono hoja zozote za kuujenga utaifa wetu na kuleta maendeleo ya Tanzania yetu. Natazama hasa mantiki na uzito wa hoja bila ya kujali ameisema nani na ni wa chama gani.

Pili, naomba kumpa pole Ndugu Jesca Kishoa kwa 'kulazimika' kufuta kauli yake kuwa 'alishaondolewa CHADEMA' ili kulinda Ubunge wake pale alipobanwa na kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika Daktari Tulia Ackson Mwansasu. Kishoa ni kama aliteleza katika kusema hivyo na akaifuta kauli yake 'kinyonge na kwa huruma' sana. Kuna wakati siasa huutweza hata utu angalau tu mambo yaende.

Hoja yangu hapa ni kuanika baadhi ya 'facts' ambazo zitaonyesha kuwa sakata la Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee liko wazi ila wahusika wanajifanya kutoona na hivyo kulinyamazia. Fuatana nami hapa ujionee yaliyo ya wazi;

Mosi, akina Halima Mdee walishtakiwa na KUFUKUZWA UANACHAMA na kilichokuwa chama chao cha CHADEMA. Mchakato wa hilo na UAMUZI huo ulitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika na hata Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikaeli Mbowe. Sitaki hapa nizungumzie utaratibu uliofuatwa kufikia UAMUZI huoa kwakuwa sisi wafuatiliaji hatuna ushahidi juu ya hilo la utaratibu.

Pili, akina Halima Mdee walitangaza kukata rufaa ndani ya CHADEMA kupinga UAMUZI huo. Hadi hapa iko wazi kuwa kuna UAMUZI uliotolewa na CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee na huo UAMUZI ndiyo uliokatiwa rufaa na wahusika hao. Ifahamike pia kuwa UAMUZI huo unawafanya akina Mdee KUTOKUWA WANACHAMA wa CHADEMA hadi pale utakapobadilishwa na mamlaka ya rufaa ndani ya CHADEMA.

Tatu, katika uga wa kisheria, KUKATA RUFAA hakufuti UAMUZI uliofikiwa hadi pale rufaa itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi mwingine. Ndiyo kusema, kuanzia siku ya KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee, UAMUZI ule umebaki hata sasa. Ni kwamba, wote WALIOFUKUZWA UANACHAMA, si wanachama wa CHADEMA. Wanachopambania kwenye rufaa zao ni KUREJESHEWA UANACHAMA WAO ndani ya CHADEMA. Kama wao kwasasa ni wanachama wa CHADEMA, wamekata rufaa ili kupata uamuzi upi tena?

Nne, nakubaliana na Naibu Spika Daktari Tulia (alipokuwa akimueleza Jesca Kishoa Bungeni) kuwa kwa mujibu wa Katiba kila Mbunge lazima atokane na chama cha siasa. Tena, kupoteza UANACHAMA wa chama cha siasa ni kupoteza nafasi yoyote ya kisiasa ya kuchaguliwa kama Ubunge na Urais. Natofautiana na kaka na mtani wangu Pascal Mayalla aliyeandika humu JF kuwa Mbunge ANAPOTEULIWA hawezi kuondolewa na chama chake. Chama cha siasa kinaweza kumfukuza mwanachama wake na uongozi unakomea hapo.

Tano, akina Halima Mdee, kuanzia siku ya UAMUZI wa CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA, hawakupaswa kuendelea kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu iko wazi: SI WANACHAMA wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania kuwawezesha kuwa Wabunge wa Viti Maalum. Sikugusia mchakato wa kupatikana kwao kwakuwa sina ushahidi nao. Nazungumzia kilichotokea baada ya wao kutangazwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Wahusika wanaujua ukweli huu lakini wamekuwa kimya. Fedha za umma zinaendelea kuwalipa wasio Wabunge. Kulingana na Naibu Spika, Ofisi ya Spika haina TAARIFA YA KUFUKUZWA UANACHAMA WA CHADEMA kwa akina Halima Mdee. Hili lina ukweli gani? Linabadilije UAMUZI wa CHADEMA? Tuwe wakweli katika hili na kutenda yatupasayo kutenda kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi yetu.
HIVI WAO WANASEMA WAMEKATA RUFAA. WAMEKATA RUFAA YA KUTAKA KUREJESHEWA UANACHAMA WA CHAMA GANI NA WAPO BUNGENI KWA TIKETI YA CHAMA GANI?

WAHUSIKA WANAJUA WALISHAFUKUZWA UANACHAMA WA CHADEMA LAKINI MAMLAKA ZA BUNGE WANAWALAZIMISHA WAFUTE KABISA KAULI YA KUFUKUZWA UANACHAMA.
 
SPIKA HAKUTAKIWA KUMLAZIMISHA JESCA KISHOA AFUTE KAULI, BALI ALITAKIWA KUMFUKUZA BUNGENI KWA KUKOSA SIFA YA KUWA MBUNGE. HALAFU HUYO MBUNGE NDIYE AWE NA KAZI YA KUPIGANIA UBUNGE WAKE AKIWA NJE YA BUNGE. AKISHINDA HIYO VITA YA KUPIGANIA UBUNGE WAKE NDIPO ARUDI BUNGENI. HUWEZI KUPIGANIA UBUNGE WAKO WAKATI UPO BUNGENI. SASA UTAKUWA UNAPIGANIA NINI WAKATI UBUNGE UNAO?
 
Back
Top Bottom