Ombi la msaada wa namna ya kupata mkopo wa mil 50. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi la msaada wa namna ya kupata mkopo wa mil 50.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mrekebishaji, Feb 26, 2011.

 1. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu naombeni ushauri, kuna kitu kinanipa changamoto sana, nina wazo la bishara ambalo nimelifanyia utafiti wa kutosha tatizo sina mtaji kwa maana ya cash/pesa taslimu

  Naomba msaada wetu wa namna ya kupata mkopo benki wa kama Mil 50. Kwa sasa nina kanyumba ka kiaina hapa tabata kisukulu ambako hakana hata title deed. Samahani nimekuwa muwazi zaidi ili niweze kusaidiwa, maana ni kweli nahitaji mkopo huo. Kwa hiyo kama kuna uwezekano wa kupata mkopo sehemu pengine wanahitaji hati nitaomba mwenye msaada wa namna ya kupata Title deed anisaidie. Natanguliza shukrani.


  Natanguliza shukrani wadau katika maendeleo.
   
 2. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mimi ninachoweza kukushauri ni kwamba, kwanza, tueleze unataka kuwekeza kwenye sekta gani, na kifupi to, biashara unayotaka kufanya inahusu nini. Baaaas.

  Then tutakuwa katika hali nzuri ya kukushauri. Kupata mkopo sio issue.
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kuwa na title deed ni hatua ya mwisho kabisa kama unataka kupata mkopo kutoka vyombo vya kifedha. La kwanza kabisa ni kuwa na andiko (feasibility study/business plan) ambayo inaeleza kwa ufasaha wazo lako la biashara,linaonyesha kwamba wewe mwenyewe una uwezo (technical skills/business experience) za kutekeleza wazo hilo, fursa za kimasoko (market opportunities), n.k. Lengo la andiko ni kumshawishi mkopeshaji kwamba wazo lako ni zuri kibiashara na halina matishio (risks) nyingi kwa mkopeshaji. Baada ya mkopeshaji kushawishika ndipo anatoa masharti ambayo lazima uyatimize ili kupatiwa mkopo. Moja ya masharti hayo ni hilo la kuwa na mali za kumlinda mkopeshaji kama utashindwa kurudisha mkopo na riba yake (collateral).
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unajua ndugu yangu mkopo si jambo la kuibuka tu unatakiwa kujipanga!
  Mimi ninachoweza kukushauri ni kwamba, kwanza, fikiria nini unataka kufanya,fikiria unataka kuwekeza kwenye kitu gani, na hicho kitu uwe umeisha kifanyia upembuzi yakinifu.
  Mkopo usipojipanga vizuri unaweza kukufanya ukanywa sumu!
  Mwisho washirikishe wadau zaidi wakusaidie kimawazo
   
Loading...