Ombi la Lema kwa Zitto na kauli ya Werema - Unganisha dots...

It is completely contradictory to what zito's advocate said last few days.Betrayers should never be left unworked upon.
 
Ni nani anayemlalamikia Zitto??????????????????????????????????? na kwa sababu gani????????????????????????

Mleta mada anataka kumsafisha Zitto na kueleza jinsi Zitto alivyo na mkakati makini.

Nina hakika Zitto amebebwa na UWT kwenye hili.( Hii ishu sio ya Zitto na Zitto anacheza ngoma ambayo yeye mwenyewe sie anayeipiga) Zitto kakwama na waliombeba wanatafuta njia ya kupita ambayo hawakuwa nayo. All they want to do is to try to rebuild Zitto's credibility that is at the moment shattered !
 
Kwahiyo Zito ameogopa kuitaja hiyo list kwakuwa na Ndesamburo yupo. Unajitia aibu ndugu yangu kumtetea Zito.

Na wewe unajitia aibu kwa kujiaminisha kuwa hakuna vijisenti vilivyofichwa ughaibuni
 
Hawa watu "wazito" ambao ZZK "anawaogopa" ni wakubwa kiasi gani kushinda wale
waliowahi kutajwa pale Mwembeya
nga na CDM?
Kwani Lema yeye hawezi kufanya utafiti anasubiri tu vya kupewa au ndo mnavyo
sema shule shida. mimi mgeni napita tu.
 
mwambie ataje sasa.
ngojera zimezidi. usitufanye wapumbavu, kama unayo taja tuanze
kuwachukia wao badala ya wewe.

hivi kwenye m4c wakati chama chenu kinahubiri kuhusu mabilion ya uswiz mlikua mnaota. Au na nyie mlikua mnadanganya umma ili mjizolee umaaruf
 
Kwani Lema yeye hawezi kufanya utafiti anasubiri tu vya kupewa au ndomnavyo
sema shule shida. mimi mgeni napita tu.

Tunamwomba Zitto atutajie majina msizuge, unafki malipo ni hapa hapa duniani
Wenzake pesa wanafanyaga biashara kuzipata sasa yeye alidhani kuiuza Chadema kutamsaidia! Haya magamba wanamgeuka sasa teh teh teh.

Na huku kwenye mageuzi tunamtosa, msaliti aliyeshindwa mpambano akaamua kusaliti!!
 
Mwambie kwanza Mbowe atoe hadharani mkanda wa bomu la Soweto ambao alisema kuwa anao. Hakika Nyani haoni kundule

Mpaka leo nafsi yangu inaniuma kutokana na bomu lile kwani ndugu yangu amekuwa kilema kutokana na tukio lile MPAKA SASA SIJUI SUALA LILE LIMEFIKIA WAPI !!!
 
Tumewasamehe serikali kuhusu mabilioni,tunamhukumu zitto as if yeye ndo mwenye jukumu hilo. Tumekubali mahela yetu yakae nje kwa kuitetea govt na kumsulubu zitto! Inaumiza kidogo!
 
Sikutegemea na wala sitarajii kuona na kusikia Godbless Lema anaunga mkono juhudi za Zitto. Lema ni mmoja wa watu wanaofaidi matunda ya ufisadi kupitia kwa mkubwa wake Mbowe

Ndugu kumbuka Lema aliongea haya mambo siku nyingi sana,alisema kama Zito atashindwa ampatie yeye majina kwa siri na atayataja!,sikumbuki ilikuwa Dodoma au Arusha mwenye kumbukumbu anisaidie hapa si ndo kasimani!!?
 
Zito kwisha amebakia kuunga unga maneno na tamaa za kipepo na matisho kwamba atakaye mbip hata mende hatapona.

Ya Ludo na Mwigu against Lwaka mling'aka sana na hatimaye mkono wa Zito umeonekana kuhusika kushinikiza Lwakatare atoswe ili mbwa wapate nafasi ya kuua.

Sisi tunaomba ikiwa Mbowe anazo fedha nje semeni

Mbowe atakosaje pesa huko kama baba ake alikuwa anafanyabiashara na wt wa huko ulaya hata kabla nyerere hapajui Moshi.Kuwa na pesa nje si tatizo tatizo ni je ulizipataje?Maana kuna akina Ngeleja!!!,mh nchi hii bana hata huyu jamaa sijui atasema kazipataje,ngoja tusubiri
 
ZZK is really genius, amegundua hata akiyataja hakuna litakalofanyika zaidi ya maisha yake kuwa katika risk, ukweli Tanzania imeoza kwa uzembe na ujinga wa serikali na watu wake pia, hivi kama Rais alishindwa kutaja majina ya wauza unga unategemea ZZK afanye nini ktk hili suala lake,hivi kama Waziri kagasheki pamoja na kinga zote alizo nazo alishindwa kuwataja majangiri licha ya kuwafahamu mpaka kwa vyeo vyao unategemea ZZK atafanya kitu gani? Tumeshuhudia kapuya na skendo yake ya kubaka binti vipi kuna hatua zozote zimechukuliwa mpaka sasa?? Sasa hapa mnataka zito ayatakje hayo majina ili iweje ama ili nn kifanyike?? Nasubiri wampeleke mahakamani mana kule ndio sehemu nzuri ya kutoa ushahidi sio bungeni kulipojaa wapuuzi na wachumia tumbo......GO GO ZZK

Nakuungamkono ndugu wampeleke mahakamani ila naogopa kwa sababu alishakataa chini ya kiapo kwamba hana majina wala hajui ac hata moja ya mtz iliyopo nje,ss akiwataja mahakama itamuelewa?
 
Inanishangaza kuona baadhi ya Watanzania wakiwa hawaelewi chochote kuhusu hii kashfa ya fedha za Uswisi so far hawaelekei kuelewa malengo ya watu wanaopeleka fedha huko Swiss kwa uelewa wao mdogo wanadhani wanaopeleka fedha huko ni Wanasiasa Mafisadi tu wasichokielewa ni kuwa hata Wafanyabiashara hupeleka fedha huko Uswisi lengo likiwa ni kukwepa kulipa kodi Nchini kwasababu kwa sheria za Nchi yetu mtu anapoweka pesa benki na zikafikia kiwango cha kutozwa kodi kule kule benki basi zitatozwa sasa basi baadhi ya Wanasiasa na Wafanyabiashara hutoroshea fedha zao katika baadhi ya Nchi ambazo benki zao hazitozi kodi (tax haven) kama vile Uswisi.So inashangaza kuona watu hapa wakimtetea mtu kama vile Mbowe eti hawezi kuwepo katika orodha ya watu walioficha fedha zao Uswisi.Mimi nakubaliana kabisa na mleta mada kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya vigogo wa Chadema kushirikiana na mafisadi wa CCM kummaliza Zitto kisiasa kwa usalama wao wenyewe,Muda si mrefu watamtoa katika Kamati ya Mashirika ya Umma.
 
Maskini watanzania mafisadi wanawajulia.... wameshahamisha mjadala. Hayajadiliwi mamilioni anajadiliwa zitto sasa.
 
Bonge la bandiko mkuu, naamini vijana wote tuliotimamu tumekuelewa na tupo bega kwa bega na ZZK japo naamini bado wapo wengi tu waliolishwa unga wa ndele wasioweza kufikiri nje ya box, wapo vijana wa ndiyo mheshimiwa, ndiyo mzee, wapo vijana waliojaa udini, ukanda na ukabila n.k ambao wana viburi vya asili katika uelewa! lakini usijali tupo wengi tu tunaomwamini ZZK na tupo naye hadi tone la mwisho!

Hapo kwenye red: I wish you could have been serious. Hizi bangi mnazovuta nyuma ya keyboards zenu zitawapeleka pabaya. AG kasema Zitto kwa kiapo chake mwenyewe amekiri hana majina ya watanzania walioficha fedha nje ya Tanzania. Kauli ya mwanasheria mkuu wa serikali ni kauli ya serikali kisheria, wewe unatangaza ati utakuwa naye hadi tone la mwisho, kwa hiyo unatangaza uasi dhidi ya serikali? Unatishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nani wewe?

Huyo Zitto wenu angekuwa na majina asingekubali kula kiapo badala yake angeshinikiza serikali iangalia taratibu na sheria za kimataifa juu ya suala ya umiliki wa fedha nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuridhia na kusaini mikataba ya kimataifa unaoruhusu mabenki ya nchi husika kutoa taarifa ya wateja wao pindi serikali ya nchi nyingine inapoomba kupewa taarifa hizo.
 
Lema anatafuta umaarufu kwa gharama yeyote ndio maana alidiriki hata kujisambazia picha akidhalilishwa.
 
Duh kwa utetezi huu naamini kuwa jamaa alikuwa ni mnafiki.

Sababu kubwa kutotaja majini ni kuwa anaogopa maisha yake ahahahahaaaaaaaaaaaa,yaani hakujua kuwa ni hatari tokea day one?Kwa hiyo anatuambia kuwa yeye ni mwoga,hatufai? Watu wameongelea ufisadi makubwa tuu mbona...

Kama anania ya dhati si aje aweke bila yeye kujulikana(unidentified ID) ameweka hapa ;majina ,account # na kiasi kisha watatokea majasiri wa ku confront wahusika?Issue kibao zimewekwa hapa namana hii.....

Jamaa ni mnafiki namba moja,unashindwa kukaa na wenzako kwenye chama unajitafutia umaarufu binafsi...hakuna mtu perfect ila usaliti na sifa binafsi ni mbaya sana kwenye jumuia.Hilter alikuwa anawatumia wasaliti kutoka jeshi jingine kupata data fulani ila mwisho anawaua ..maana anajua pia wanaweza msaliti yeye wakipata sababu yeyote ya ku justify usaliti wao.
 
Back
Top Bottom