Ombi kwa NACTE: Tunaomba mtuongeze japo siku tano za kufanya maombi ya Shahada

Walker Water

JF-Expert Member
Aug 23, 2022
785
2,954
Dirisha la tatu na mwisho kwa mwaka huu la kutuma maombi ya shahada ya kwanza ndiyo limefungwa jana.

Tunaomba NACTE watuangalie kwa jicho la huruma wengine, tunaomba watuongezee japo siku tano au hata wafungue dirisha la usajili kwa siku mbili za mwanzoni mwa mwezi wa kumi.Naomba hivi kutokana na watu wengi kushindwa kutuma maombi kutokana na kuchelewa kupata AVN,na pia kuchelewa kutoka kwa vyeti vya stashahada.Asante,natumaini kilio chetu kitasikika ili tuweze kutimiza ndoto zetu kwa mwaka huu.
 
Watakuja majiniazi wakuulize umechelewa wapi? AVN si ungetafuta tu punde walipofungua dirisha?

Cheti kimechelewa vipi? Na siku hizi kwani mnaweka vyeti kwanza?
 
Incomplete ziliwahusu ndomana wakachelewa.... ndugu zangu chezeeni miaka yote ila sio mwaka wa mwisho wa diploma!
 
Watakuja majiniazi wakuulize umechelewa wapi? AVN si ungetafuta tu punde walipofungua dirisha?

Cheti kimechelewa vipi? Na siku hizi kwani mnaweka vyeti kwanza?
Makosa yapo mkuu na vikwazo ni vingi,hata mpira unadakika za nyongeza,si bora zaidi na hili nalo linalohusu maisha ya watu watuongeze!
 
Tunashukuru Mungu kwa TCU kusikia kilio chetu na kuongeza siku tano,pia shukrani ziwaendee Jamii forum na wadau wote mliosaidia kupaza sauti zenu.
IMG_20221004_074804.jpg
 
Back
Top Bottom