Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,651
- 218,131
Baada ya ajali ya MV NYERERE na hasa baada ya kukamilika kwa shughuli za ukusanyaji maiti na uokozi , Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa aliunda tume ya kuchunguza chanzo cha ajali hiii mbaya kabisa iliyoua namia ya wananchi , naogopa kuweka idadi halisi ya waliokufa kwa ajili ya kuheshimu SHERIA YA TAKWIMU , Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi , Amina .
Mmoja wa wajumbe wa tume hii anaitwa JOSEPH MKUNDI , ambaye Waziri Mkuu alizitaja sababu za kuteuliwa kwake ndani ya kamati hii kuwa ni pamoja na yeye kuwa mkazi wa eneo hilo na pia ni Mwakilishi wa wananchi , kwa maana ya mbunge wa eneo la ajali na kwamba bila ya shaka uwepo wake utaleta imani ya wananchi kwa tume husika , amekuwa akilipigia kelele suala la kivuko hicho ndani na nje ya bunge kwa muda mrefu .
Kwa bahati mbaya kabla hata ya kazi ya tume kushika kasi Ndugu JOSEPH MKUNDI ameamua kujiuzulu ubunge na hivyo KUPOTEZA sifa kuu ambayo ilimfanya Waziri Mkuu amteue kuwa mjumbe ndani ya kamati , na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari pamoja na kujivua ubunge ametaja pia kujivua vyeo vyote alivyokuwa navyo awali , ninao uhakika kwamba moja ya vyeo alivyokuwa navyo ni pamoja na ujumbe wa tume hii , nashauri aondolewe.
Naomba kuwasilisha .