Ombi: Ili haki itendeke Joseph Mkundi aondolewe kwenye Kamati ya kuchunguza Ajali ya MV Nyerere

Hivi kamati ya nini??

Hivi sababu za kuzama kwa kivuko si zilikuwa wazi. Nazo ni kivuko kibovu na kilijaza abiria kupita kiasi. Hizo nyingine ni porojo tuu
 
Hilo lisaccos lenu linapukutika kila siku ndio maana una jazba. Siwezi kukusaidia aisee.
na wewee una jazba kwa kuwa makarai na nyumbu wanatoka upinzani wakifika kwenu wanaonekana lulu. shukuruni sana lisaccos letu limetengeneza viongozi hadi mmewaona na kuwashawishi ili wahamie kwenu
 
Hamna hoja yoyote hapa zaidi ya siasa majitaka, mnamuonea wivu hadi kuwa kwenye tume tu ? Ukerewe hakuna Mbunge, yeye ndio mwakilishi mstaafu wa karibuni, je hiyo ni dhambi akiwakilisha wana Ukerewe au mnataka aje Mbowe au mwana CDM ?
labda atwambie tofauti na huyo, yeye anapendekeza nani awe mbadala...
 
Hamna hoja yoyote hapa zaidi ya siasa majitaka, mnamuonea wivu hadi kuwa kwenye tume tu ? Ukerewe hakuna Mbunge, yeye ndio mwakilishi mstaafu wa karibuni, je hiyo ni dhambi akiwakilisha wana Ukerewe au mnataka aje Mbowe au mwana CDM ?
akiwekwa meya, watasema kwa vile ni ccm
 
Baada ya ajali ya MV NYERERE na hasa baada ya kukamilika kwa shughuli za ukusanyaji maiti na uokozi , Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa aliunda tume ya kuchunguza chanzo cha ajali hiii mbaya kabisa iliyoua namia ya wananchi , naogopa kuweka idadi halisi ya waliokufa kwa ajili ya kuheshimu SHERIA YA TAKWIMU , Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi , Amina .

Mmoja wa wajumbe wa tume hii anaitwa JOSEPH MKUNDI , ambaye Waziri Mkuu alizitaja sababu za kuteuliwa kwake ndani ya kamati hii kuwa ni pamoja na yeye kuwa mkazi wa eneo hilo na pia ni Mwakilishi wa wananchi , kwa maana ya mbunge wa eneo la ajali na kwamba bila ya shaka uwepo wake utaleta imani ya wananchi kwa tume husika , amekuwa akilipigia kelele suala la kivuko hicho ndani na nje ya bunge kwa muda mrefu .

Kwa bahati mbaya kabla hata ya kazi ya tume kushika kasi Ndugu JOSEPH MKUNDI ameamua kujiuzulu ubunge na hivyo KUPOTEZA sifa kuu ambayo ilimfanya Waziri Mkuu amteue kuwa mjumbe ndani ya kamati , na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari pamoja na kujivua ubunge ametaja pia kujivua vyeo vyote alivyokuwa navyo awali , ninao uhakika kwamba moja ya vyeo alivyokuwa navyo ni pamoja na ujumbe wa tume hii , nashauri aondolewe.

Naomba kuwasilisha .
Ukikosa ukweli unaweza kubeba na uongo
 
Huyo amepumzika tu ubunge kwa muda, anarudi tena muda sio mrefu ila itakuwa kwa tiketi ya CCM
Angekuwa mtahiniwa tungeita anasafisha cheti.
Natarajia atarejea kwa idadi ya kura nyingi kuliko za awali.

Sijui kama ni ukatili kwa wananchi au ni mapenzi kwa chama alikohamia,au msemo wa aliyekuwa Mbunge wa Serengeti umeyimia!!!

Pamoja na haki alizonazo zote,lakini hili linatia shaka uwakilishi wake huo kwenye kamati iliyoundwa.
 
Hamna hoja yoyote hapa zaidi ya siasa majitaka, mnamuonea wivu hadi kuwa kwenye tume tu ? Ukerewe hakuna Mbunge, yeye ndio mwakilishi mstaafu wa karibuni, je hiyo ni dhambi akiwakilisha wana Ukerewe au mnataka aje Mbowe au mwana CDM ?
Anawakilisha masaburi yako?
 
Siwezi kushangaa hoja yako ya kibri cha namna hii. Kwani ni lazima uonyeshe ushirikiano wa kuhakikisha watanzania hawajui udhaifu wa baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ambavyo vipo kwa ajili ya kutafuna ruzuku badala ya kutafuta mbinu za kuwasaidia watanzania.

Mtu asiyejua lolote anaweza akadhani hiyo ruzuku ni pesa ya maana kumbe ni uchafu mtupu. Ingekuwa wanapata 5b@mwezi ningeona tunajadili pesa ya maana sio hiyo chenchi.
 
mimi ni bavicha mchovu, lakini nikija huko kwenu nalamba uteuzi fasta, hivyo nyie huko ndio choka mbaya au tuaweza kusema mbwa kachoka kabisa
Katambi kawa DC huku Magonjwa mtambuka akiendelea kupiga deki Lumumba !
 
Back
Top Bottom