Ombeni mvua wakati wa masika

Samson Ernest

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
404
651
"Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni", Zek 10:1 SUV.

Maelezo ya kina kuhusu andiko hili tunayapata zaidi kwenye kitabu cha Hosea, tutaweza kufahamu zaidi kile ambacho nabii Zekaria alikiimaanisha hapa.

"Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi", Hos 6:2‭-‬3 SUV.

Hapa inaonyesha wazi kuwa toba ya kweli ya watu wa Mungu italeta maisha mapya ya kiroho.

Kisha watakapoanza kumjua Bwana kwa viwango vya juu zaidi, ndipo atakuja kama mvua, akileta maisha na baraka zaidi za kiroho.

Mara nyingi maji katika biblia hutumiwa kama ishara au aina ya Roho Mtakatifu, hili tunaliona kupitia kitabu cha Yohana.

"Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake", Yn 7:37‭-‬38 SUV.

Mvua za majira ya kuchipua ni mvua zinazoonyesha wakati wa kipindi cha kulima na kuotesha mbegu za mazao mbalimbali.

Mvua hizi ni ishara ya kazi za Roho Mtakatifu katika kipindi cha agano la kale.

Mvua za majira ya baridi ambazo hunyesha wakati wa kuvuna; ni ishara ya kazi za Roho Mtakatifu katika kizazi cha kanisa.

Mvua hii ya Roho Mtakatifu inapaswa kunyesha kwa kila mwamini, hatupaswi kuona mvua hii ikinyesha kwa wengine na kuwaletea matunda.

Tunapaswa kunyeshewa na mvua hii ya Roho Mtakatifu na kuzaa matunda ya Kimungu katika maisha yetu.

Mungu akubariki sana
Soma neno ukue kiroho
Samson Ernest
+255759808081
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom