Omba omba wa Leo kanishangaza

Omba omba wa Leo kanishangaza

Leo mida ya saa 4 asubuhi nilikuwa nimepaki gari manispaa ya temeke ,akaja mtu wa makamo kavaa kawaida sana akaniomba nauli ya kwenda kawe nikamjibu sina ,baada ya muda roho ikajistukia nikashuka nikamfuata nikampa elfu 2 zilikuwa buku buku akaenda nikapata hamu ya kutaka kujua kuwa ni mkweli au la nikijifanya kama naondoka nikarudi bila ya yy kuniona .
Japo la kwanza alipofika pale stand alikuta kuna vipofu akatoa hela akawapa nahisi ni ile buku 1 na pili kweli alipanda gari la kawe tofauti na omba omba wengi walivyo huyu waleo ni wakipekee
My take akikujia mtu anataka kitu kama unaweza msaidie ,haijilishi km ni mkweli au muongo Kwa kuwa wapo wengine wa kweli na hauwezi kuwajua
Na katu usimnyime anaeomba akale.
Kwa kweli ukitaka kuniibia hela wala usinikabe, we njoo tu uniambie unataka hela ukale, basi nikivuta picha jinsi njaa inavyoumaga yaan nashindwa kujizuia, nitakupa tu hiyo hela..
 
HAkuna lolote, huyo alishakustukia kuwa unamfwatilia, kuua soo akacheza kama pele kwa akili kubwa sana zaidi ya ma greater thinker kadhaa ya humu jf
 
Leo mida ya saa 4 asubuhi nilikuwa nimepaki gari manispaa ya temeke ,akaja mtu wa makamo kavaa kawaida sana akaniomba nauli ya kwenda kawe nikamjibu sina ,baada ya muda roho ikajistukia nikashuka nikamfuata nikampa elfu 2 zilikuwa buku buku akaenda nikapata hamu ya kutaka kujua kuwa ni mkweli au la nikijifanya kama naondoka nikarudi bila ya yy kuniona .
Japo la kwanza alipofika pale stand alikuta kuna vipofu akatoa hela akawapa nahisi ni ile buku 1 na pili kweli alipanda gari la kawe tofauti na omba omba wengi walivyo huyu waleo ni wakipekee
My take akikujia mtu anataka kitu kama unaweza msaidie ,haijilishi km ni mkweli au muongo Kwa kuwa wapo wengine wa kweli na hauwezi kuwajua
Na katu usimnyime anaeomba akale.
tenda wema nenda zako Mungu ndiye mlipaji
 
Kwa kweli ukitaka kuniibia hela wala usinikabe, we njoo tu uniambie unataka hela ukale, basi nikivuta picha jinsi njaa inavyoumaga yaan nashindwa kujizuia, nitakupa tu hiyo hela..
Ndo hivyo we toa bana ni bora utoe hata kama umedanganywa kuliko kumnyima aliye na njaa kwa kumuhisi muongo kumbe yuna njaa kweli
 
We mshamba tu. Kwani lazima utaje gari ? Kwenye ukoo you are number one to own a used car. Ptyuuuuui mshamba kajogoo
Na we mshamba pia kwenye sentesi yako lazima uchomeke kiingereza au kwenye ukoo wenu we ndo wakwanza kumaliza kidato cha nne?
 
kumbe una gari, hongera kwa kumiliki usafiri....

umefanya jambo jema umemsaidia, nae ameweza kusaidia mwingine.

Nilidhani parking ya gari lake ina relationship na anachotaka kutuambia kumbe ni utambulisho
 
kumbe una gari, hongera kwa kumiliki usafiri....

umefanya jambo jema umemsaidia, nae ameweza kusaidia mwingine.
Tatizo ni lenu na ushamba wenu, sasa akisema amepaki gari wewe unawaza anajionyesha yani show off kumbe sio... Wakati sahivi magari ni mengi usipokua na hata vitz basi acha kufanya hiyo kazi unayoifanya acheni ushamba, elewa content vingine achana navyo
 
Sasa kuna chuma ulete,,ukimpa tu imekula kwako,,juzi nimekutana na mmoja mikocheni anatiambia anaomba nauli katoka mlimani city kwa mguu mpka mikochen so nimpe aende kkoo,nikamwambia sikupi naogopa

Hivi kwann wanaonaga rahis kuomba mtu nauli kwann wasiende kwa daldala wamuombe kinda,,kuna tofauti gani, hapo ndo wananitiaga mashaka
Next time jaribu kumpima....mwambie kama unataka nauli twende tukasimamishe gari nikulipie ...akimbwera tu ujue tapeli uyo
 
Kuna wengine wameshafanya ndio kazi yao. Kuna mama mmoja aliwahi kuniomba nauli mara 2 kwamba anakaa chanika. Mara ya kwanza nilimpa, mara ya pili nikamkumbuka nikamchan live . Basi aliniporomeshea matusi nusura nimzabe makofi. Alikua anapenda kukaa vituoni moroco, kinondoni b na manyanya siku hizi simuoni sijui kahamia kituo gani
 
hapo sijaona cha kushangaza mpaka ufikie kuleta uzi humu...labda ulitaka watu tujue kuwa nawe ni miongoni mwa watanzania wachache wenye kumiliki magari
 
Makonda amekataza kuwasaidia bn..we hujamsikia mkuu kan
 
Ni kweli kuna wengine wanakua wamepungukiwa pesa kama sh mia kwenye nauli au kununua kitu muhimu kama dawa ,anaweza kukuomba na ukadhan tapel kumbe kweli ana shida ya maana
 
Sasa mkuu buku mbili tu umemfuatilia mpaka stend Je ungempa buku ten si ungemfuatilia mji mzima
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom