Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,230
Reaction score
3,333
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
Vitukuu vya Seyyid Said,vilitoka vinaongra kiswahili na vimewafunza wanafamilia,ukiachilia mbali raia wa kuomba.
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
Wapo wengi Sana wazanzibari wenye uraia wa Oman. Wana wajomba kaka Dada nk jeshi la Oman wako hadi maafisa wakubwa wa jeshi wanaoongea kiswahili fasaha kabisa. Mfalme wa Oman Ana nduguze kibao Zanzibar pia hivyo kuna mwingiliano mkubwa wa Oman na Zanzibar
 
Vitukuu vya Seyyid Said,vilitoka vinaongra kiswahili na vimewafunza wanafamilia,ukiachilia mbali raia wa kuomba.
Wako wazanzibari wengi ndugu wa mfalme wa Oman ambao wakitaka kuhamia Oman huwa rahisi kwao na wakienda huwa na haki Sawa na raia wa Oman huwapa vyeo vya serikali au ajira, siasa nk hivyo ukiwaona usishangae Wengine ni wazaliwa wa darajani Zanzibar waliohamia Oman kwa ndugu zao tena wamehamia wakiwa na umri mkubwa
 
98% na ndiyo maana tunaambiwa÷
kiswahili ni lugha nasibu iliyoanzia pwani ya Afrika mashariki ambapo wenyeji wa UPWA huo uliitwa "aswahili" au "sawahili".
Sio 98%, na ujue Kiswahili kinatofauti na eneo na eneo, ukikisikia kiswahili cha DRC hakina kabisa maneno ya Kiarabu na kama yapo ni machache sana, kiswahili chao kimejaa Kibantu na maneno ya kifaransa
 
Sio 98%, na ujue Kiswahili kinatofauti na eneo na eneo, ukikisikia kiswahili cha DRC hakina kabisa maneno ya Kiarabu na kama yapo ni kachachesana, kiswahili chao kimejaa Kibantu na maneno ya kifaransa
Kiwashili ni kimoja tu,anaeongea tofauti maana yake hajui kutamka maneno ya kiswahili,hakuna cha DRC wala new york.
 
Kiwashili ni kimoja tu,anaeongea tofauti maana yake hajui kutamka maneno ya kiswahili,hakuna cha DRC wala new york.

Kiswahili sio kimoja kaka, Ni kama kiingereza tu, Uk wana Chao, USA wana chao, Jamaica wana Chao, Nigeria wana Chao,

Shelisheli wana Kiswahili chao, kuna sehemu ya Madagascar pia wana chao, Kenya Nairobi na Mombasa kuna tofauti, DRC wana chao, tembea uone kaka, acha kubisha uko nyuma ya QWERTY
 
Kiingereza ni kimoja pia,hao wengine wameamua kuumiza matamshi ya baadhi ya maneno,ndiyo maana unaambiwa kuna FORMAL ambayo ni ya UINGEREZA hakuna kiingerza cha Naijeria wala kongo,isipokuea INTONATION tu na hiyo inatokana na lugha zao wanazotumia.
Usijidanganye kama kuna kiingereza cha KIHAYA wala KiSUKUMA,ni lafudhi na matamshi tu yaliyoathiriwa na lugha fulani ama za makabila au Mataifa,unawezaje kusema KIINGEREZA cha NAIJERIA wakati umeshasema"KIINGEREZA?"
HII MAANA YAKE NI LUGHA YA UK.
Usiwe mvivu wa kufikiri.
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
Kama umesoma historia ya uhusiano wa Oman na Zanzibar hilo la kawaida sana. Wazanzibar wana nasaba kubwa sana na Waoman.
 
Kiswahili sio kimoja kaka, Ni kama kiingereza tu, Uk wana Chao, USA wana chao, Jamaica wana Chao, Nigeria wana Chao,

Shelisheli wana Kiswahili chao, kuna sehemu ya Madagascar pia wana chao, Kenya Nairobi na Mombasa kuna tofauti, DRC wana chao, tembea uone kaka, acha kubisha uko nyuma ya QWERTY
We acha ushamba,hao jamaica wanapoongea kiingereza kilichoathiriwa na lugha za kwao siyo maana yake ni kiingereza cha jamaica,Hiyo inaitwa PATWA au FATWA kwakuwa wameweka na vionjo tofauti kabisa,vya lugha zao za makabila yao,lakini ukishasema kiingereza maana yake ni LUGHA ya WAINGEREZA.
 
We acha ushamba,hao jamaica wanapoobgea kiingereza kilichoathiriwa na lugha za kwao siyo maana yake ni kiingereza cha jamaica,Hiyo inaitea PATWA au FATWA kwakuwa wameweka na vionjo tofauti kabisa,vya lugha zao za makabila yao,lakini ukishasema kiingereza maana yake ni LUGHA ya WAINGEREZA.

We ushamba umeacha lini?, hivi hata hujui Kiswahili kilivyogawanyika?, Kiswahili kina matabaka kaka, ngoja basi nikufahamishe na uelewe tofauti ya kiswahili cha Tanzania na Kikongo
Cha Tanzania kina mchanganyiko wa Kiarabu, Kibantu, Kiingereza nk, Lakini kiuhalisia maneno Mengi ya Kiarabu yana Kibantu chake, kwa sisi huku Tanzania maneno ya kiarabu bado mengi yanasimama kwenye lugha yetu, lakini kwa Congo maneno almost yote ya Kiarabu hayatumiki na mbadala wake wanatumia maneno ya Kibantu na Kifaransa,
Sasa basi kwa Mkongo akiongea Kiswahili cha kwao kwa sisi Watanzania tunaelewa anachokiongea, lakini sisi tukiongea Kiswahili chetu chenye Kiarabu wanapata shida san kujua tunachoongea
Na hata Congo yenyewe Kiswahili pia kina tofauti, East Congo angalau tunaweza kuongea vizuri, lakini Katanga ni shida kabisa, na Kinshansa almost hakuna Kiswahili

Acha ushamba wewe
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
huyo waziri ni mpemba, ila ni raia wa Oman, ila Omani familia nyingi huwa zinaongea kiswahili, sio official lakini mkikutana watu wanaongea kiswahili
 
Wapo wengi Sana wazanzibari wenye uraia wa Oman. Wana wajomba kaka Dada nk jeshi la Oman wako hadi maafisa wakubwa wa jeshi wanaoongea kiswahili fasaha kabisa. Mfalme wa Oman Ana nduguze kibao Zanzibar pia hivyo kuna mwingiliano mkubwa wa Oman na Zanzibar
Pia mfalme wa Oman asili yake ni znz
 
Back
Top Bottom