Oliver N’Goma: Icole (Shule)

Tonydigital

Senior Member
Oct 6, 2014
186
245
Nyimbo: Icole
Maana: Shule (School)
Album: Bane
Kutolewa: 1990
Mtunzi: Oliver N’Goma
Mwandaaji / Producer: Manu Lima

Kibao hiki ni cha tatu katika Album yake ya Bane iliyotoka rasmi mwaka 1990.

Oliver “NOLI” anajaribu kuelezea mchango wa shule/elimu katika maisha yake mpaka hapo alipofikia. Ikumbuke kuwa mnamo miaka ya 1980’s Oliver alienda masomoni Ufaransa kujiendeleza katika mambo ya media kama “camera man”

“Shule, nilikuchukia kwa sababu ulinifanya niende mbali, ulinitenganisha na watu wangu wa karibu niliowapenda na kunipelekea katika mazingira mageni na magumu kuzoea.
Ulinipeleka mbali na jua la nyumbani ( hapa anazumgumzia mazingira ya joto ya nchi yake ya Gabon).
Lakini sasa natambua na kushukuru ninapata mengi mazuri kupitia shule na endapo nisingezingatia nisingekua hivi nilivyo leo.
Shule imenifanyia mambo mengi mazuri na pia ninashuhudia wengi wakifanikiwa kupitia wewe.
Ni dhahiri kuwa katika magumu tunayopitia mwishoni huja furaha.

IMG_9798.jpg


Oliver N’Goma “NOLI” 23.03.1959 - 07.06.2010
 
Thank you isidingo55
Been listening to his songs, and highly in love with them (without really knowing what they mean).
Siasa ya Africa tu ndiyo unatudharaulisha, lakini Africa ni tamu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom