Oliver N’Goma: Barre (Mapenzi ni muda)

Tonydigital

Senior Member
Oct 6, 2014
186
245
Habari wadau !!
Leo tuingalie kibao cha mkali wa miondoko ya zouk afrika; Oliver N’Goma.

Nyimbo: Barre
Maana: Hapana/ Imetosha / Strongly No.
Kutoka: 1995
Album: Adia
Lugha: Lumbu ( Gabon)
Mwandaaji mkuu: Manu Lima
Label: Lusafrica.

Kibao hiki ni nambari nne ( 4 ) Katika album ya pili ya “Noli” iliyotoka mwaka 1995.

Maana: nyimbo hii inazungumzia kisa cha mwanamke aliyechoka mahusiano yake kwa sababu mwenzi wake ( mume) sio mwajibikaji katika familia.
Mara nyingi hupenda kutoka pekee na marafiki zake sehemu mbalimbali za starehe na kumuacha mke wake mara kwa mara mpweke.
Mara zote humwacha mkewe mwemyewe, mke amechoka hivyo anataka kuondoka; kama mapenzi ni pesa na mali tu, yeye yupo tayari kumwaachia vyote hivyo akaanze upya kama asipobadilika maana kila siku anarudi nyumbani Usiku akiwa amechelewa. Kama mapenzi ndio kama haya yupo tayari “mke” kumwacha na mali zake zote. Kwani mapenzi sio utumwa na mateso maana kuna wanaume wengi wazuri wenye tabia nzuri pia. Mwanamke sio chombo cha starehe/ utumwa ambacho kipo tayari kupokea na kuvumilia “hali ya ukomavu wa mme”.
Mwisho mke anasisitiza kuwa mwenzie asipobadilika hatogeuka nyuma katika maamuzi maana ndoa sio utumwa.

RIP OLIVER N’GOMA
“Sho sho sho tkikitcha”
Digital.
 

Attachments

  • 1B37B138-A83E-43C0-88D8-67479C011F0D.jpeg
    1B37B138-A83E-43C0-88D8-67479C011F0D.jpeg
    28.6 KB · Views: 15
Back
Top Bottom