Ole wako mwanadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ole wako mwanadamu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Consigliere, Apr 27, 2011.

 1. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,025
  Likes Received: 7,414
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati Nimuangaliapo mwanadamu huwa ninasisimuka sana. Ninasisimuka nimuangaliapo mwanadamu katika umoja wake na zaidi pale wanapokuwa katika wingi wao.


  Sisisimuki kwa sababu ya jinsia zao au maumbo yao… hapana, bali ninasisimuka kwa ajili ya kile nisichokijua na nikijuacho kuhusu yeye au wao, ninasisimka kwa yale nisiyoyajua kuhusu yeye kwasababu uzoefu unaonyesha kuwa japo una uhakika kuwa hamfahamiani na hamjawahi kuonana hapo kabla lakini cha ajabu ni kuwa tayari kwake yeye unaweza ukajikuta ni lengo lake, ninasisimka kwasababu kuna wakati najua mwanadam anajaribu kufanya jambo ambalo anaamini litamsaidia, wakati yeye mwenyewe hajitambui na wala hana takwimu za mahitaji yake ni kiasi gani. Maisha ya binaadam yametawaliwa na migogoro na maamuzi, migogoro ya ndani ya kichwa chake pia ile ya mtu na mtu na jamii na jamii, upande wa maamuzi ni juu ya nini kifanyike na kifanyike vipi.

  Huwa ninatumia muda kila ninapoupata kumfikiria mwanadamu pamoja na mazingira anayoishi, mwanadamu huyu ambaye anajinadi kuwa na uelewa wa juu zaidi ya viumbe wengine, uelewa ambao ni matokeo ya utashi alionao, utashi ambao unamtofautisha na kumuweka juu ya viumbe wengine, kwa sababu unampa uwezo wa kupambanua mambo, utashi unaomfanya maisha yake yatawaliwe na migogoro, kwa sababu ni kupitia migogoro hii ndiyo hufikia maamuzi sahihi juu ya nini kifanyike na kwa wakati upi.

  Nikiiangalia jamii tunayoishi ninajiuliza yuko wapi yule mwanadamu mjivuni mwenye akili na kitu cha ziada kiitwacho utashi. Utashi umezaa maarifa ambayo yamepelekea uvumbuzi wa mambo mbalimbali yenye lengo la kuyafanya maisha ya mwanadamu huyu yawe rahisi, mazuri na salama.

  Je ni kweli maisha yamekuwa rahisi, mazuri na salama? Ili tuweze kukubaliana au kutokubaliana katika hili yatupasa kwanza tupate tafsiri ya maneno haya ( rahisi, mazuri na salama) kuanzia hapo tuanze mjadala, na mimi kwa makusudi kabisa naongeza mgogoro mwingine… kila mmoja atafsiri kwa namna yake maneno haya, halafu kuanzia hapo mimi nitaundeleza mjadala huu, kuona kama mwanadamu amefanikiwa au la….

  Urahisi uko wapi wakati tunashuhudia watu wanashindwa kuyamudu maisha yao ya kila siku, wakifanikiwa ni pale tu wanapoweza kuyapoza makali ya tumbo, ni mazuri kwa kiasi gani wakati huduma za kijamii hususan zitolewazo na ofisi za umma ni kama hazipo kwa sababu wazifanyao ni kama vile wamelazimishwa au wapo kwenye mgomo fulani hivi, ni salama kwa kiwango kipi wakati uhalifu unazidi kuongezeka, na pengo kati ya aliyenacho na asiyenacho linaongezeka. Hapa usalama utatoka wapi.

  Wazazi/walezi wamesahau wengine wamelazimika kuyaacha majukumu yao kiasili kwa familia, wote tunafikiria namna ya kuongeza kipato, na kuwasahau watoto na hivyo wakitumia muda mwingi chini ya uangalizi wa wasichana wa kazi (naweza nisilaumu sana katika hili kwa sababu ni matokeo ya mfumo wa kiuchumi wa dunia, ambao ni matokeo ya migogro), na mara umri unapoongezeka wanaanza kujitafutia maadili na tabia kutoka kwa wenzao au kupitia mitandao ya internets, Video games na Televisions, hapo tutegemee matokeo yake yatakuwa ni nini? Ni lazima tutapata wanadam lakini wasio na utu ndani yake, ndiyo ninaa maanisha asiye na utu, ikumbukwe kuwa binaadamu ni maumbile na ule uwezo wake wa kibaiolojia, ila hali ya kuwa na utashi ndiyo inaumba utu ndani yake.

  Hayo ndiyo yanayonifanya nisisimke sana kila nimuangaliapo mwanadam. Mwanadamu mwenye mipango mingi inayoonekana kuwa ni mizuri lakini inaleta mwisho mbaya.

  Je ni kitu gani kinamfanya mwanadamu ajikute hapo alipo, na kila anapojaribu tena hali iishie kuwa hivyo? Wote tunakubaliana kuwa mpaka mwanadamu anapofiki kuanzisha michakati ya kujikomboa ni kwa sababu anakuwa ameona tatizo na hivyo anajenga dhamira ya kuondokana nalo. Swali linakuja kwa nini kila akitatua tatizo moja yanaongezeka au kujitokeza mengine mengi?

  Mimi nadhani hii ni kwa sababu kila tatizo ni sehemu ya tatizo kubwa na pia tatizo lenyewe limejengwa na mengine madogodogo mengi.

  Lakini sababu nyingine ninayoipa nguvu mara tatu zaidi ya ile ya kwanza yaani asilimi sabini na tano (75%) ni kwamba:

  JINSI TUNAVYOLIONA NA KULICHUKULIA TATIZO NDIYO TATIZO:
  Hivyo tunahitaji kuwa makini katika kuyabaini na kuyaanisha matatizo kabla ya kuanza kuelekea kwenye hatua ya utatuzi.

  Na ili kuweza angalau kuyatatua matatizo yetu kwa kiwango cha kuridhisha, tutumie nguvu mbadala na ile tuliyoitumia katika hatua ya uvumbuzi wa tatizo husika

  Hapa nina maana kuwa, akili na nguvu iliyotumika katika katika kulibaini au kugundua tatizo si sahihi nguvu hiyo hiyo ikatumika katika kulitatua.

  Ndiyo maana kuna kanuni zipo kwa ajili ya ugunduzi wa tatizo ufumbuzi hadi utekelezaji wake, kwa kifupi ni kuwa baada ya kuona tatizo unafuata utafiti na baada ya utafiti kinachofuata ni utekelezaji (Program)
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Thread yako umeiandika kana kwamba wewe sio mwanadamu.Anyway umeanisha ukweli mwingi
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  Nimependa thread yako na jinsi ulivyosisitiza kubadilika kwa mwanadamu katika ulimwengu wa sasa ambapo dunia imekua kijiji. Umekata tamaa mno katika maelezo yako juu ya mwanadam, kana kwamba hakuna wenye utashi na wanaoweza simama wenyewe. Huku ukikataa kua maisha hayajawa rahisi, mazuri na salama.

  Nazingatia katika eneo la Rahisi, Mazuri na Salama

  Haya mambo sio rahisi kiasi hicho, naomba utambue kwamba urahisi wa maisha sasa hivi ndo unaleta matatizo yoote hayo ambayo umeainisha katika thread yako kwa baadhi ya wanadamu.

  Vitu vimerahisishwa mno mpaka wakati mwingine mtu ana lemaa kwa kila kitu, unashida na Fulani basi unampigia simu una haja ya kumfuata – wengine wanapigiana na wako wote nyumba moja wakati huo huo; msomi kapewa assignment katika level ya chuo hataki kusoma vitabu aelewe na kutafakari mwenyewe badala yake ana google kisha ana copy na kupaste.

  Watoto saizi michezo badala ya kwenda kucheza mpira amebwagiwa playstation hapo na kila aina ya game unategemea hio product ya watu hao inakua aina gani?

  Ni kweli hivyo vitu vinafaa lakini kwa kiwango, tusipoangalia tunaelekea siko. Hivyo tunapozungumzia urahisi nafikiri tusi egemee urahisi wa watu kuishi bali urahisi wa mambo mengi kurahisishwa na jinsi yanavyopelekea kuharibu maisha huo urahisi ukiendekezwa.


  Tunapozungumzi uzuri kwa upande wangu ni ile hali ya kusema walau wengi tunajua nini kinaendelea duniani (utandawazi), jinsi gani tunaruhusu na tunakubali kunyonywa na pia jinsi gani tunamapungufu na madhaifu katika maamuzi na uendeshaji wa sekta muhimu hapa nchini.

  Utashi wa kutatua matatizo utatoka wapi na hali viongozi wa jana ni wasomi wa juzi, viongozi wa leo ni wasomi wa jana, wasomi wa leo ni viongozi wa kesho… makundi yote hayo matatu yalikua yakililia haki ya kila raia wa Tanzania wakati wakiwa katika kundi la usomi.

  Lakini hayo hayo makundi (wasomi) wanapopata nafasi ambayo wanaweza mtumikia mtanzania na kumbadilisha maisha yake anasahau machungu yake na anakua hapo kwa manufaa ya wachache pamoja na familia yake. Uzuri hapo unakuja kua tunajua yote haya - hapo kale wazazi walikua hawana bahati ya kuelewa nini kinaendelea ndani na nje.

  Sisi tunajua NDIO lakini haina maana yoyote sababu ukweli unabaki palepale kua watanzania sisi sio wazalendo. Naangalia wapiga kelele humu nchini ni wale wenyewe hatuna kitu cha uhakika ili kuendesha maisha yetu haya ya kudimba.


  Ninapozungumzia usalama sina haja ya kwenda mbali, tukiendelea hivi tulivyo sisi Watanzania, wanajamiii, wasomi, viongozi na kukosa uzalaendo kuna USALAMA KWELI?
   
 4. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,025
  Likes Received: 7,414
  Trophy Points: 280
  Umesema kweli na kwa uhakika. Mchanganuo wako ni dhahiri
   
 5. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  WHY DO YOU THINK PEOPLES GIVEN UP ON GOD?

  Kwa maana watu wengi wapo busy na utafutaji/ubunifu wa ulahisishaji wa maisha kuliko kumtegemea Mungu.
  Sina shaka na maelezo yako hapo juu, ila ninachoweza kuongezea nikwamba, toka mwanaadamu astaarabike amekuwa akijisogeza karibu sana na shetani.

  Tangu alipo jitambua kule Eden kwamba yupo uchi na kuanza kutafuta njia ya kujihifadhi ndo ulikuwa mwanzo wa ubunifu wa kubuni mambo mengi ili kumpa nafuu binaadamu.

  Katika ubunifu huo alijikuta anabuni mpaka silha za maangamizi lengo ikiwa ni kujikinga na wanaadamu wabaya.

  Japo silaha zimekuwa zikitumika hata kwa watu/viumbe wasio na hatia.
   
 6. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,025
  Likes Received: 7,414
  Trophy Points: 280
  Watu wana Give up on God kwa kuwa wamekuwa na matarajio makubwa na ya moja kwa moja toka kwa mungu, badala ya kujiangalia sisi wenyewe na mapaji aliyotujalia, na kuona ni namna gani tunaweza tukwa vyanzo na msaada wa mahitaji yetu, badala yake wote tumeinua vichwa juu, au tumesujudu tukipeleka maombi na vilio vyetu kwake.
  Ni kama tumefungwa mitazamo yetu, hatutumii utashi wala akili zetu ipsavyo, wala viungo vyetu wala nguvu za misuli yetu kikamilifu.
  Matarajio na malalamiko ni makubwa kuliko uwajibikaji.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hii kitu niliisoma mahala, sikujuwa kama ndio wewe... Not bad... keep it up bro.
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  Never connected up the dots Consig...... One of my very first posts at JF - Just after 15 days of my time here... Umenikumbusha mbali. Be good Mkuu.
   
 9. T

  Tiger JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa mtazamo wako muanzisha mada, unafikiri ni kipindi/zama gani hapa duniani mwanadamu aliwahi kuishi bila changamoto(challenge/problems), ni kipindi gani hapa duniani ambacho mwanadamu hakuathirika na majanga ya asili kama matetemeko ya nchi, magonjwa,njaa/ukame, mafuriko nk.
  Vipi kuhusu vita je, ni wakati gani hakukuwahi kuwa na vita?
  Unaonaje mafanikio tuliyoyafikia mpaka sasa kuhusu, afya,kilimo,usafiri, viwanda,mawasiliano n.k
  mambo mengine ya kuwa busy yanatokana na maendeleo yetu wenyewe na si kosa la mwanadamu ila maumbile ya asili ya ulimwengu tunaoishi.
  "The fitest shall survive"- no exception.
  Muache "mother nature" afanye kazi yake, pengine kwa idadi yetu ya sasa(bilioni 7) maisha yangekuwa magumu zaidi kama tusinge ishi hivi tunavyo ishi.
  Nawasilisha.
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mada nzuri nzito na inatafakarisha!!

  "... Hapa nina maana kuwa, akili na nguvu iliyotumika katika katika kulibaini au kugundua tatizo si sahihi nguvu hiyo hiyo ikatumika katika kulitatua..."

  Msaada!!:

  ... Ni Nguvu gani sahihi kutumika kutatua tatizo baada ya AKILI kuhusika katika ugunduzi wa tatizo husika!!?
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,025
  Likes Received: 7,414
  Trophy Points: 280
  Akili moja ni ya kidadisi /kugundua, wakati nyingine ni ya kupendezesha na kutengeneza kanuni na mifumo ili kufikia hatua nyingine

  Akili ya mvumbuzi husukumwa/huongozwa na udadisi wakati mwingine mvumbuzi huwa hajisumbui kufanya prove, thats why Galileo Galileo leo hii ana heshima kubwa katika ulimwengu wa Sayansi kwa sababu aliweza kuvumbua na kuthibitisha uvumbuzi wake, tofauti na wengi ambao waliishia katika uvumbuzi tu then wakarudi kwenda kuvumbua mengine.
  Ndiyo maana leo hii tukiangalia NGO's na INGO's zetu utagundua kuwa waliofanya tafiti na kupelekea ziwepo siyo wale wanaoziongoza sasa.
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,651
  Trophy Points: 280
  Ngoja niwe mkweli hapa!Mwanadamu hana AKILI,kwa maana ya kujijua na kujua kile kilichomleta hapa duniani,dont tell me ulikuja kumuabudu Mungu coz Mungu hahitaji kuabudiwa,kama anahitaji amepoteza sifa ya kuwa Mungu.Mungu hana uhitaji wowote.Unafikiri maisha yana maana?Au unafikiri hayana maana?Kama ni ndiyo au hapana,why?Kwanini mvua inanyesha baharini?Hivi mwanadam ni lini atajijua na kukijua kinachomzunguka?May be kauli hii iliyosema NOTHING IS BLACK OR WHITE ina ukweli mkubwa!
   
 13. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,025
  Likes Received: 7,414
  Trophy Points: 280
  Nashindwa kuelewa kama unahitaji majibu ama vipi......? Nikionacho hapo umeshika ramani ya hoja na kuishia kupima vipimo lakini umeshindwa hata kuchimba mashimo ili uweze kujenga hoja yako........Try again naamini una kitu kizuri cha kujadili, ila unahitaji utulivu, ile usiongozwe na haraka.
  Just try again
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,651
  Trophy Points: 280
  Inawezekana uko sahihi,ngoja nije!
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Umeongelea akili mbili kama mwanadamu alivyo na mikono miwili! Wa kulia na wa kushoto! Ni juu ya muhusika kutumia mikono yote au kutumia mmoja!

  HAPA nataka kuziona akili hizo mbili kama zana za kazi na pia niogezee kuwa zana hizo mbili moja niite AKILI na zana ya pili niite UFAHAMU!

  Yaani AKILI nikimaanisha INTELLECT na UFAHAMU nikimaanisha CONSCIOUSNESS!

  Uvumbuzi unaweza kukamilishwa na nyenzo ya intellect peke yake lakini ili kukamilisha uhakiki wa kilichogunduliwa Consciousness inahitajika! Kwa sababu mbalimbali mwandamu anweza kutumia mkono mmoja nadani yake yaani Akili peke yake na akaacha Ufahamu wa juu ambao ni kama nuru ya kuwezesha kuproove kile akili ilichogundua!

  Galileo hakuwa kilema wa undani wa kibinaadamu ..altumia mikono yake yote miwili ndani yake ....Akili na ufahamu!

  Kwa kweli jamii inahitaji mchakato wa matatizo kutatuliwa kwa ukamilifu wa kibinaadamu kupitia Mikono timamu ya mwilini na mikono kamili ndani ya mwanadamu!

  Ni Hakika AKILI peke yake haiyawezi matatizo ya mwandamu wa leo wa zamani au ajaye !!!

  Nategemea viogozi wetu watakuwa sio wavivu na kunielewa hadi kutumia Akili zao na Fahamu zao katika kulifiksha taifa hili mahali pema kimaendeleo!!
   
 16. Atabase Agaya

  Atabase Agaya Senior Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  A superb thread!:alien:
   
 17. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,025
  Likes Received: 7,414
  Trophy Points: 280
  You sounds one with a big kind of brain....sina cha kuongeza katika hii post.
   
 18. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,650
  Likes Received: 3,299
  Trophy Points: 280
  Hapo mwanzo mungu alipo ziumba mbingu na nchi [dunia]na kumkabidhi mwanaadamu kati ya majukumu aliyo mpa ni pamoja kuijaza [kuzaana]na kuistawisha. Mpaka hapo binaadamu huyo haku pewa jembe wala panga wala chochote ambacho ni hand made. Ila alipewa akili na utashi .uliokuwa tayari kutumika, katika majukumu hayo mapya, akili isiyo na mipaka [isiyoweza kuelezeka kiu sahihi] na utashi usioleta jawabu moja kwa maswali yote yanayo na yatakayo msibu binaadamu huyo wala matokeo yatakayo kidhi haja ya utashi wake,na hivyo kufanya mzunguko huo.usio na mwisho unaoeleweka from the starting point. Utashi unamsukuma kujaribu kuyarahisisha mazingira ya maisha yake yakila siku bila kuwa na uhakika wa kiwango cha wepesi anaotaka kuufikia,ili kuyafanya maisha yake kuwa mazuri. Bila ya kuwa na definition ya uzuri anao utafuta. Na hivyo kumfanya kutofikiri positively kuhusu usalama uliopo au utakaokuwepo katika harakati zake hizo. Ndio ni katika cicle hiyo maisha yetu yanapo safiri kutoka eneo moja kwenda jingine. Akiongozwa na utashi unaotegemea hisia zitokanazo na tamaa ya kupata vitu hivyo ulivyoviainisha hapo juu. Wepesi. Uzuri[ubora]pamoja na usalama. Bila ya kuwa na kiwango halisi cha uhitaji wa vitu hivyo [kimoja kimoja]
   
 19. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ONet!

  Nafikiri nina cha kuchangia katika tafakari yako!

  Lakini nengeomba kwanza unifafanulie maana ya UTASHI! Kwa nini?

  Ninaamini kuwa Undani wa Mwanadamu una Nyezo mbili za kazi kama alivyo mwanadamu wa nje aliye na Nyezo ya Mkono wa Kushoto na Mkono wa kulia.

  Ninachotaka Kuona hapo kama Utashi unaweza kuwa kitu hichohicho nilichookita UFAHAMU kwenye maelezo yabgu hapo juu! Kwani kimsingi umeonyesha kuwa Mwanadamu ana nyenzo mbili kama ambavyo mimi pia nakubalina!

  Wewe umeziita AKILI na UTASHI. Mimi nimmeziita AKILI na UFAHAMU!

  Ninaamini hizi nyezo mbili bila kutumika kikamilifu ni kumfanya mwandamu wa ndani yetu KILEMA kama ambavyo Mwanadamu wa nje anaweza kuwa Kilema kama hakutumia mikono yake miwili Kutimiza majukumu ya kumuendeleza kijamii na kimaisha!
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Thanks for the compliment Sir, typically honored by this!

  Lakini hapo kwenye BRAIN!

  Ninaamini kuwa ni kimoja katia ya AKILI au UFAHAMU/UTASHI au vyote viwili! Yaani umependa kuniambia kuwa Mimi sio KILEMA wa Ndani ... kuwani natumia sahihi zana mbili zinazopatikana ndani ya mwanadamu !(ONet.. anasema tulikabidhiwa na Mungu) Na kama signature yako inavyoonyesha kuwa huamini zana moja inaweza kutufikisha kwenye kilele cha ukombozi!

  Nitajitahidi kutafuti vipimo ili niweze kujipima na kutambua Viwango vya AKILI na UFAHAMU wangu .... Kama ni Lazima! Ila nimeshukuru kwa Utambuzi wako!!
   
Loading...