Ole Sendeka amtwanga konde M/kiti UVCCM!

Hawa jamaa wa Arusha watageuzwa kuwa wajinga kama wale wa Mbeya. Watatumiwa na wanasiasa mufilisi kuendeleza maugomvi wee huku maendeleo yanadorora.

Lowassa alipewa nafasi mpaka kuwa PM, alishindwa kuitumia vizuri kuliletea taifa letu maendeleo na badala yake akawa anajitajirisha yeye tu. Kuna umuhimu gani wa yeye kuendelea malumbano ya kisiasa yasiyo leta tija kabisa huko Arusha?

Huyo mbunge kapiga mtu na kashitakiwa, kweli kuna haja ya watu wote hao kwenda kule eti kumuunga mkono? Mkuu Matejoo ame summarise vizuri sana hapo juu. KUna watu wanafikiri wanamiliki vita dhidi ya ufisadi, hata wakikosea, wasiguswe. Huyo mbunge kupiga mtu ngumi kuna uhusiano gani na vita vya ufisadi?

Hayo maugomvi yameucost sana mkoa wa Mbeya, jifunzeni na nyie msiende huko huko.

Mpaka tufike 2010, mikoa yote itakuwa inawaka moto.
 
Mkuu naona umechanganya madawa hapa.
Mwanakijiji alikua "mjumbe" tu na kuweka jamvini makala iliyoandikwa kwenye moja ya magazeti mapya yalioibuka na spidi ya kummaliza R. Mengi(wengine walisema ya Manji). Hayakua makala ya Mwankijiji mwenyewe.
Thanks kwa ufafanuzi. Na labda ndio maana hakujibu mashambulizi.
 
Pasco,

Hiyo makala unayoisema haikuandikwa na Mzee Mwanakijiji, yeye alisaidia tu kuanzisha hiyo thread. Makala ilikuwa ni ya mtu mwingine kabisa.

Mengi ameshambuliwa hapa JF mara nyingi sana, je mara ngapi ameshatushitaki?

Hata hiyo makala unayoisema, tumia search tool na utaipata. Huenda imeondolewa kwenye siasa na kupelekwa kule kwenye celebrities.
Thanks for observation.
 
Mkuu Matejoo
Good analysis hakuna cha kuongeza wala kupunguza

Asante Mkuu Ngongo. Kwa tunaothamini nafasi ya JF katika jamii tunajitahidi kufanya tafiti na chambuzi za kuaminika even if it means going against public opinion. Waliosoma historia wanajua taharuki iliyoletwa na "Water Gate" skendo kule Marekani. It is almost the same na hali tuliyonayo hivi sasa Tanzania. Rationality inaweza kututoka tukaharibu zaidi kuliko kujenga. We need to be careful with those waanzisha wimbo wa ufisadi. Not every one of them is genuine. Wanatumia "taharuki" kujinufaisha.
 
Kweli nimeamini kuwa "Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi". Hili swala ukilichunguza bila ushabiki na bila emotions utajifunza mambo mengi sana.

1.. Ole Sendeka hawaelewani na Lowassa. Kwa sababu hii kila mpinzani wake somehow anakuwa attached na Lowassa. Hata ugomvi huu usingetokea, Sendeka bado angeunganisha upinzani dhidi yake na "hujuma" za kufikirika za Lowasa.

2. Vita dhidi ya mafisadi inatumiwa vibaya na baadhi ya watu kuwaweka watanzania katika hali ya taharuki na kusahau kutafakari. Kila mtu anayekwenda kinyume na "Sendeka-Kimaro-Kilango-Mwakyembe" SEKIKIMWA Syndicate, hata kwa maswala binafsi, anaonekana kuwa mpinzani wa vita dhidi ya mafisadi, something which is untrue and very unfortunate. Inahitaji vyombo vya sheria visivyo endeshwa kwa emotions la sivyo haki haitakaa itendeke nchini. Kupambana dhidi ya ufisadi hakumpi mtu kinga dhidi ya uovu wake na uvunjaji wa sheria. Hata hivyo, katika hali ya taharuki iliyoikumba nchi (its quit natural, any historian will tell you so) ni vigumu kupata public opinion tofauti. Vyombo vya sheria visifuate public opinion, vifuate haki.

3. "Reigand Ole Mengi" amepata sehemu ya "kulipa fadhila" alizotendewa na Sendeka. Pia ni njia ya kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa hakuwa "pamoja" na Lowassa enzi za ufalme wake, something which only GOD can prove. Mengi ni mfanya biashara, just like any other businessman. Kusoma alama za nyakati ni moja ya mbinu za kubakia kwenye soko. Kwenda mahakamani in person ni ushabiki uliopita mipaka. Ni kujishushia heshima, ukizingatia Sendeka ana nguvu, umri, uzoefu na hata pesa nyingi kuliko Millya.

4. Hapa Millya ni Daudi anayepambana na Goliath. Ole Sendeka yuko na Mengi, (with his whole media) one one hand na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzanite, wabunge wenzake na "anti-Lowassa" network on the other. Millya ameshika "manati" ambayo ni haki yake kama Mtanzania huru anayetafuta haki na ukweli kuwa kapigwa kibao na kutishiwa kwa bastola. One does not need PhD in Quantum Physics to predict the results.

5. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari haiwezekani kwa sasa kutenganisha swala hili na ugomvi kati ya Lowassa na Sendeka. Some how, Millya lazima ataonekana ku "tumiwa" na mafisadi. Hii inadhihirisha kuwa vita vya tembo zinazoumia ni nyasi. Millya anaweza kukosa haki zake kwa kuwa "wakubwa" wanagombana. Yeye ni nyasi tu katika hili. Tusubiri tuone.

Mawazo yako yamejaa chuki... yame-base kwenye nadharia zaidi. Ulikuwepo wakati Millya na Sendeka wanagombana??? Wacha kutoa hoja za chuki.....
 
"...wala usimlaumu Sendeka, ni mtu muhimu katiaka vita dhidi ya ufisadi..."

This kind of thinking is what puts me off completely! Vita dhidi ya ufisadi gani? Amefanya nini so far zaidi ya kutoa maneno ya kuuma na kupuliza? Can somebody put on the net an audio device of whatever Ole Sendeka has ever said watu wenye akili zao wachambue content? Kwanini watu mnakuwa wepesi wa kupokea mbwa mwitu il hali mnapaswa "kuzipima kila roho?"

Supposing that this guy was mpambanaji dhidi ya ufisadi as some of you have poorly been swept to believe, ni mwenda wazimu peke yake ndiye angesapoti kitendo cha Mbunge mzima, kumtwanga makonde kijana mdogo na hata kumtishia kwa bastola kisa amemsema katika presentation yake ya haki za ardhi. (Indirectly even!) Uvumilivu wa Kitanzania uko wapi?? This is a mystery!

Tupambane na ufisadi. Lets do it 24 hours 7 lakini kwa kufanya hivyo tusihalalishe u "Dito Pile" dhidi ya vijana wenzetu na watanzania kwa ujumla. Kama ambavyo urais siyo kinga dhidi ya ufisadi, kuongea against mafisadi siyo kinga dhidi ya matendo maovu ya kuua demokrasia na kuonea vijana wanaochipukia katika siasa kisa eti wametangaza kugombea ubunge. How PATHETIC????

Kijana yeyote wa kitanzania atakayenunuliwa na mafisadi ili kujaza tumbo lake kama huyu James Milya, Deus Balile na hata vibabu kama Salva Rweyemamu, Muhingo Rweyemamu , Kingunge, Makamba ni sumu ya maendeleo ya Taifa la Tanzania na laana hazitaacha kuwaandama..............
 
Mawazo yako yamejaa chuki... yame-base kwenye nadharia zaidi. Ulikuwepo wakati Millya na Sendeka wanagombana??? Wacha kutoa hoja za chuki.....

Mkuu macho_mdiliko, twende polepole mkuu. At its basic, kufikishwa mahakamani kwa Sendeka kunatokana na makosa niliyoyataja. Kama mimi na wewe hatukuwepo, haitoshi ku "towesha" hizo allegations. However, I must admit that he is inocent untill proved guilty by the court. Kama nimetumia hyperbole nisamehe. Sina nia ya kutoa hoja za kuchuki. I am trying to show you upande ambao labda hupendi kuusikia kwa kuwa sote tuko kwenye tararuki and rationality is not our best friend at the moment. This is quit natural.
 
Kijana yeyote wa kitanzania atakayenunuliwa na mafisadi ili kujaza tumbo lake kama huyu James Milya, Deus Balile na hata vibabu kama Salva Rweyemamu, Muhingo Rweyemamu , Kingunge, Makamba ni sumu ya maendeleo ya Taifa la Tanzania na laana hazitaacha kuwaandama..............

Mkuu macho_mdiliko sikatai. Lazima tuweke maslahi ya watanzania mbele na siyo matumbo yetu. Mimi nafikiri cha muhimu ni kuwa waangalifu ili wote tunaodhani wamenunuliwa basi tuwe karibu na uhakika as much as possible na tunayo yasema. Tusifikiri kila aliye kinyume na SEKIKIMWA syndicate hata kwa maswala binafsi amenunuliwa. Itafikia mahali kila anayejipatia "hati miliki" ya vita dhidi ya ufisadi (kwa maneno yake) anapewa immunity dhidi ya kila kitu hata kudaiwa deni binafsi na jirani yake kutatafsiriwa kuwa ni "hujuma" kwa vile "wanapambana na ufisadi". Like during the famous water gate scandle, wabakie wachache miongoni mwetu watakao tafuta rationality even after the "big guys" are out and people wish they could be "crucified" in public. Hii kesi ya Millya inahitaji rationality zaidi kuliko taharuki na hasira zetu zitokanazo na wakati tulionao. At least that is what I would do ningekuwa kwenye dawati la haki e.g. mahakama au polisi. Mtu yeyote asionewe na mtu mwingine asikose haki kutokana na upepo uvumao katika jamii. Justice should be reliable!!
 
Mkuu macho_mdiliko, twende polepole mkuu. At its basic, kufikishwa mahakamani kwa Sendeka kunatokana na makosa niliyoyataja. Kama mimi na wewe hatukuwepo, haitoshi ku "towesha" hizo allegations. However, I must admit that he is inocent untill proved guilty by the court. Kama nimetumia hyperbole nisamehe. Sina nia ya kutoa hoja za kuchuki. I am trying to show you upande ambao labda hupendi kuusikia kwa kuwa sote tuko kwenye tararuki and rationality is not our best friend at the moment. This is quit natural.

Pamoja na yote yaliyoainishwa katika thread hii, Mh. Sendeka hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani. Tusipende kurukia hitimisho na kuhukumu kabla ya mtuhumiwa kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya hakimu au jaji kwenye mahakama iliyo huru.

Wengi wetu humu tumekuwa subjective na kasumba ya kwenda mbali na kuhukumu kupitia habari za magazeti. Kama tutaendeleza utamaduni huo wa kutoa hukumu nje ya mahakama ni mwanzo wa kuua nguzo ya utawala wa sheria na credibility ya baraza letu hapa yaweza kuwa katika mashaka.

Shadow.
 
Kweli nimeamini kuwa "Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi". Hili swala ukilichunguza bila ushabiki na bila emotions utajifunza mambo mengi sana.

1.. Ole Sendeka hawaelewani na Lowassa. Kwa sababu hii kila mpinzani wake somehow anakuwa attached na Lowassa. Hata ugomvi huu usingetokea, Sendeka bado angeunganisha upinzani dhidi yake na "hujuma" za kufikirika za Lowasa.

2. Vita dhidi ya mafisadi inatumiwa vibaya na baadhi ya watu kuwaweka watanzania katika hali ya taharuki na kusahau kutafakari. Kila mtu anayekwenda kinyume na "Sendeka-Kimaro-Kilango-Mwakyembe" SEKIKIMWA Syndicate, hata kwa maswala binafsi, anaonekana kuwa mpinzani wa vita dhidi ya mafisadi, something which is untrue and very unfortunate. Inahitaji vyombo vya sheria visivyo endeshwa kwa emotions la sivyo haki haitakaa itendeke nchini. Kupambana dhidi ya ufisadi hakumpi mtu kinga dhidi ya uovu wake na uvunjaji wa sheria. Hata hivyo, katika hali ya taharuki iliyoikumba nchi (its quit natural, any historian will tell you so) ni vigumu kupata public opinion tofauti. Vyombo vya sheria visifuate public opinion, vifuate haki.

3. "Reigand Ole Mengi" amepata sehemu ya "kulipa fadhila" alizotendewa na Sendeka. Pia ni njia ya kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa hakuwa "pamoja" na Lowassa enzi za ufalme wake, something which only GOD can prove. Mengi ni mfanya biashara, just like any other businessman. Kusoma alama za nyakati ni moja ya mbinu za kubakia kwenye soko. Kwenda mahakamani in person ni ushabiki uliopita mipaka. Ni kujishushia heshima, ukizingatia Sendeka ana nguvu, umri, uzoefu na hata pesa nyingi kuliko Millya.

4. Hapa Millya ni Daudi anayepambana na Goliath. Ole Sendeka yuko na Mengi, (with his whole media) one one hand na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzanite, wabunge wenzake na "anti-Lowassa" network on the other. Millya ameshika "manati" ambayo ni haki yake kama Mtanzania huru anayetafuta haki na ukweli kuwa kapigwa kibao na kutishiwa kwa bastola. One does not need PhD in Quantum Physics to predict the results.

5. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari haiwezekani kwa sasa kutenganisha swala hili na ugomvi kati ya Lowassa na Sendeka. Some how, Millya lazima ataonekana ku "tumiwa" na mafisadi. Hii inadhihirisha kuwa vita vya tembo zinazoumia ni nyasi. Millya anaweza kukosa haki zake kwa kuwa "wakubwa" wanagombana. Yeye ni nyasi tu katika hili. Tusubiri tuone.

Mkuu Matejoo, BADO hujatoa anlysis ya kuonyesha kuwa Millya hajatumiwa na Mzee Edo.
Conflicts just do not happen out of the blues mkuu.
 
Pamoja na yote yaliyoainishwa katika thread hii, Mh. Sendeka hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani. Tusipende kurukia hitimisho na kuhukumu kabla ya mtuhumiwa kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya hakimu au jaji kwenye mahakama iliyo huru.

Wengi wetu humu tumekuwa subjective na kasumba ya kwenda mbali na kuhukumu kupitia habari za magazeti. Kama tutaendeleza utamaduni huo wa kutoa hukumu nje ya mahakama ni mwanzo wa kuua nguzo ya utawala wa sheria na credibility ya baraza letu hapa yaweza kuwa katika mashaka.

Shadow.
Asante sana Shadow. Nafurahi wana JF tunapokuwa objective kumheshimu kila mtuhumiwa as innocent until proven guilt. Huu ndio utawala wa sheria.
 
Mkuu Matejoo, BADO hujatoa anlysis ya kuonyesha kuwa Millya hajatumiwa na Mzee Edo.
Conflicts just do not happen out of the blues mkuu.

Mkuu Lole Gwakisa kama umesoma analysis yangu vizuri nimesema kwa sasa ni vigumu sana kutenganisha sakata zima na ugomvi kati ya Sendeka na Lowassa. Kwa nini?

1. Baada ya swala kufikishwa mahakamani, "kambi ya Lowassa" inataka kujipatia "kautukufu" kutokana na sakata zima. Kwenye vita dhidi ya ugaidi, waasi etc wanausalama wanaangalia sana kabla ya kukubali kila kikundi cha kigaidi kinachojitangazia "kuhusika" na tukio fulani. Some times hawahusiki ila wanatumia such a bang kujitangaza kuwa wamo! ( I do not underestimate nguvu walizonazo kina Lowassa, but kwa sasa watu wana wakuza mno, even more than their own gods)

2. Ole Sendeka anapenda ionekanane na jamii nzima/umma wa watanzania kuwa Lowassa is behind the whole saga. Hii inampa huruma ya wananchi na legality ya wazito kama kina "Reginand ole Mengi" kumsaidia. Otherwise how would Mengi's conglomerete come against a mere UVCCM reginal chairman?

3. Habari nilizokusanya kabla ya analysis yangu ya kwanza ni kwamba from the very begining Edo hakutaka kabisa kuhusishwa na hii saga na siasa za Simanjiro kwa ujumla. Sababu kubwa wanasema anamuogopa Sendeka kutokana na kauli zake kali. Walipopigana hawa ma yero wawili Edo alikuwa na JK Minjingu i.e hakuwa kwenye eneo la tukio. Millya aliporipoti polisi Monduli mjini, Edo was still away. Chanzo hicho cha habari kinadai kuwa sasa Edo anaweza "kujaribiwa" kuingilia kati kutokana na sababu ya kwanza hapo juu, otherwise the whole thing is really between Millya and Sendeka. Wanataka Edo awepo ili wapate media coverage kubwa, huruma ya wananchi na vifua vya kina Mengi na wafanya biashara. Otherwise kama Chiligati alivyosema haka ni ka-ugomvi kama ka mtu na mkewe. No substance. Remove Edward Lowassa from it, the thing becomes very ordinary! Chiligati saw it from far. Sema hakuweka wazi but you can read between the lines! No Lowassa no kuoneshana misuli!
 
Last edited:
Asante sana Shadow. Nafurahi wana JF tunapokuwa objective kumheshimu kila mtuhumiwa as innocent until proven guilt. Huu ndio utawala wa sheria.

Sure, tusihukumu pre maturely. Tuviachie vyombo husika kufanya kazi zao.
 
Back
Top Bottom