ChaMtuMavi
JF-Expert Member
- Oct 15, 2008
- 330
- 8
Mmmmh! Tushukuru hakuwa na cha moto yangekuwa kama ya hayati bro DITTO
Ndugu zangu wapenzi katika kristu, kweli tutafika kama wabunge wanaanza kuwarushia ngumi watu. Sasa ustaarabu uko wapi, halafu sababu zenyewe za kurushiana ngumi...du! kweli makubwa sasa jaribu kufikiri mtu kama huyu kutetea maslahi ya wananchi. Mtu yeyote mwenye uzalendo wa kweli hatakasirika anaokosolewa kwani kwa njia hiyo ndio anajiboresha katika madaraka yake. Kadili yangu mim huyo jamaa hafai kuwa mbunge...kwani hata wananchi watakapomkosoa atawarushia ngumi huyo kiaina, mpigeni chini huyo akalime viazi kama mikono inamuwasha.
Kwa mujibu wa maelezo ya Ole Sendeka ni kwamba alijihami baada ya Millya kutaka kumdhuru.Hata hivyo suala hilo lipo mahakamani litaamuliwa huko.Lingine ni kuwa mafisadi wapo nyuma ya sakata hili kama lilivyokuwa sakata la Nape.Kikao cha mila cha wamasai kiliitishwa na Mmeru/masai Lowassa kuhusu masuala ya Ardhi.Tatizo la Ardhi mfano Monduli Lowassa angeyatatua akiwa Mbunge wa Monduli na alipokuwa Waziri Mkuu.Lakini sasa ndio anataka kutatua masuala hayo sijui alishindwaje wakati ule,halafu ukiangalia Lowassa alichangia kushabikia migogoro ya ardhi iliyojitokeza wakati wa uongozi wake dhidi ya marafiki zake na wapinzani wake kisiasa.Ukiangalia kwa upana Ole Sendeka aliingia mtegoni kuhudhuria kikao kilichokuwa na lengo la kumhujumu,unajua ukitaka kumchokoza Simba ili kujua hazira zake na ukali mzingire akose pa kupitita ndipo utaona muziki wake.Hivyo Sendeka awe makini na mitego kama hiyo,ingawa hakuna asiyejihami akitishwa na Sendeka hakuwahi kusema simanjiro ni yake mbona kwa utendaji wake anaweza kuchaguliwa Mbunge popote na kwa Chama chchote.
Mkulu MatejooKuna watu mediocre sana humu nchini kwetu. Ndiyo maana ni rahisi kwa kila mbwa mwitu kuvaa ngozi ya kondoo na kupeta bila kushtukiwa na mtu yeyote. Yaani maneno tu yametosha kuwatongoza watanzania na akili zao kumuona Ole sendeka kuwa anapambana na ufisadi. Can any sensible person tell me why they regard him as such? Historia yake mnaijua? Huko Simanjiro mana fahamu umafia alioutenda in the past 3 years kiasi cha kuigawa wilaya katika makundi? Yeye alipokuwa mwenyekiti wa CCM wilaya alimfanyia vituko gani Parseko Ole Kone aliyekuwa Mbuge wa Simanjiro by then? Kwa kifupi chama kilichukua hatamu Simanjiro!
Elimu ndogo ya Sendeka si tatizo sana (kama alivyosema mchangiaji kuwa Mahalu ni Prof lakini kauibia) kama haitumii kumjengea infiriority complex na kuvuka mipaka ya utu yaani kufikiri. Kutokana na kielimu chake basi anaogopa kinvuli cha Millya.
Mimi nafikiri tuangalie kila jambo on its own case. Hii ya Sendeka kuijumlisha na uhasama wake na Lowassa ni kupoteza dira. There is nothing like mkono wa mafisadi in this particular thing. Ni kweli mheshimiwa Mbunge ana maadui wengi kutokana na maneno yake makali lakini hii haimpi kinga dhidi ya vitendo vyake viouvu na makosa ya jinai. Kwa mwendo huu itakuwa kila anayekemea ufisadi (kwa maneno) anajijengea aina fulani ya immunity against criminal actions iwe ujambazi, ubakaji, unajisi na kutishia kuua. Wake up my fellow Tanzanians!
Uwepo wa Mengi kumsindikiza Sendeka, ni uthibitisho wa kuunga mkono hoja ya Sendeka kuwa chanzo ni msimamo wake dhidi ya vita vya ufisadi.
Mzee Mengi amejiweka kimbembele kwa Sendeka ili kutangaza personal vendeta na Lowasa aliye nyuma ya Milya.
Tena nadhani (hypothes) ni Mengi ndiye anayemlipia Sendeka gharama za wakili Ngalo mdogo, maana juzi Ngalo alikuwa akisoma kwa kutetemeka huku akijikanyaga kanyaga, kusuudio la Mengi kulishitaki gazeti la TAZAMA kwa kumkashfu. Halafu jana Mengi na Ngalo wakatinga mahakamani kumsindikiza Sendeka.
Ni Sendeka alisaidia kufacilitate Mengi kupata kitalu kikubwa Mererani na kuwashawishi wazee wa Kimasai kumsimika Mengi kuwa Laibon na kumbatiza jina la Reginandi Ole Mengi pale Mererani mwanzoni mwa mwaka 2006. Hivyo huu ni wakati wa kulipa fadhila.
Karibu utabiri wa Mzee Mwanakijiji kuhusu anguko la Mengi, utatimia maana sasa yuko usawa wa front line ya siasa dhidi ya mafisadi.
"...wala usimlaumu Sendeka, ni mtu muhimu katiaka vita dhidi ya ufisadi..."
Amefanya nini so far zaidi ya kutoa maneno ya kuuma na kupuliza?....
Kwa mujibu wa maelezo ya Ole Sendeka ni kwamba alijihami baada ya Millya kutaka kumdhuru...
please mkuu,naomba unikumbushe ni wapi Mzee Mwanakijiji alipotoa huo utabiri!?
Mzee Mwanakijiji alimchambua Mengi kama karanga katika thread ya Anguko la Mengi kama Maxwel. Ilikaa for few days nilipotaka kuchangia sikuiona tena. Sikujua kama ilijifade out ama kulikuwa na mkono wa mtu. Kwa Tabia ya Mengi anavyopenda kusifiwa tuu na anavyofedheheka kuumbuliwa, nadhani angedhamiria kuishitaki JF lakini nadhani mwanasheria wake akamwambia hii ni forum tayari ina disclaimer.
Mzee Mwanakijiji alimchambua Mengi kama karanga katika thread ya Anguko la Mengi kama Maxwel. Ilikaa for few days nilipotaka kuchangia sikuiona tena. Sikujua kama ilijifade out ama kulikuwa na mkono wa mtu. Kwa Tabia ya Mengi anavyopenda kusifiwa tuu na anavyofedheheka kuumbuliwa, nadhani angedhamiria kuishitaki JF lakini nadhani mwanasheria wake akamwambia hii ni forum tayari ina disclaimer.
Kweli nimeamini kuwa "Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi". Hili swala ukilichunguza bila ushabiki na bila emotions utajifunza mambo mengi sana.
1.. Ole Sendeka hawaelewani na Lowassa. Kwa sababu hii kila mpinzani wake somehow anakuwa attached na Lowassa. Hata ugomvi huu usingetokea, Sendeka bado angeunganisha upinzani dhidi yake na "hujuma" za kufikirika za Lowasa.
2. Vita dhidi ya mafisadi inatumiwa vibaya na baadhi ya watu kuwaweka watanzania katika hali ya taharuki na kusahau kutafakari. Kila mtu anayekwenda kinyume na "Sendeka-Kimaro-Kilango-Mwakyembe" SEKIKIMWA Syndicate, hata kwa maswala binafsi, anaonekana kuwa mpinzani wa vita dhidi ya mafisadi, something which is untrue and very unfortunate. Inahitaji vyombo vya sheria visivyo endeshwa kwa emotions la sivyo haki haitakaa itendeke nchini. Kupambana dhidi ya ufisadi hakumpi mtu kinga dhidi ya uovu wake na uvunjaji wa sheria. Hata hivyo, katika hali ya taharuki iliyoikumba nchi (its quit natural, any historian will tell you so) ni vigumu kupata public opinion tofauti. Vyombo vya sheria visifuate public opinion, vifuate haki.
3. "Reigand Ole Mengi" amepata sehemu ya "kulipa fadhila" alizotendewa na Sendeka. Pia ni njia ya kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa hakuwa "pamoja" na Lowassa enzi za ufalme wake, something which only GOD can prove. Mengi ni mfanya biashara, just like any other businessman. Kusoma alama za nyakati ni moja ya mbinu za kubakia kwenye soko. Kwenda mahakamani in person ni ushabiki uliopita mipaka. Ni kujishushia heshima, ukizingatia Sendeka ana nguvu, umri, uzoefu na hata pesa nyingi kuliko Millya.
4. Hapa Millya ni Daudi anayepambana na Goliath. Ole Sendeka yuko na Mengi, (with his whole media) one one hand na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzanite, wabunge wenzake na "anti-Lowassa" network on the other. Millya ameshika "manati" ambayo ni haki yake kama Mtanzania huru anayetafuta haki na ukweli kuwa kapigwa kibao na kutishiwa kwa bastola. One does not need PhD in Quantum Physics to predict the results.
5. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari haiwezekani kwa sasa kutenganisha swala hili na ugomvi kati ya Lowassa na Sendeka. Some how, Millya lazima ataonekana ku "tumiwa" na mafisadi. Hii inadhihirisha kuwa vita vya tembo zinazoumia ni nyasi. Millya anaweza kukosa haki zake kwa kuwa "wakubwa" wanagombana. Yeye ni nyasi tu katika hili. Tusubiri tuone.