Okwi aibwaga Yanga

Okwi aibwaga Yanga

Ngarna

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
1,964
Reaction score
824
Emmanuel Okwi leo ameruhusiwa kuchezea Simba bila ya kulipa chochote baada ya kikao cha kamati ya sheria na haki za wachezaji kubaini kwamba hakua na mkataba na Yanga tokea January 2014.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana jana (Septemba 7) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.

Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.

Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.

Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.

Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.

Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.

Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe huyo hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi. Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.

Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.

Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.

Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.

Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi watakapolipa.

Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.

Kamati inasisitiza kwa wanachama wa TFF kuheshimu mikataba.

Chanzo: TFF

Source: HULEEE! BREAKING NEWZZZZZZZZ! MKATABA WA YANGA, OKWI HAUPO, SIMBA WAWAPIGA BAO WATANI! | Shaffih Dauda

[h=2]HULEEE! BREAKING NEWZZZZZZZZ! MKATABA WA YANGA, OKWI HAUPO, SIMBA WAWAPIGA BAO WATANI! Kitaifa[/h]
HMB7074-11-774x320.jpg
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7 mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.
Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.
Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe huyo hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi. Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.
Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.
Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.
Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi watakapolipa.
Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.
Kamati inasisitiza kwa wanachama wa TFF kuheshimu mikataba.
BONIFACE WAMBURA
KAIMU KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5962#sthash.1g3QeIxz.dpuf
 
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeanza kusikiliza kesi inayomhusu mshambuliaji Emmanuel Okwi.
 
Yanga walikurupuka kwa okwi,mchezo waliotaka kufanya ulikua mzuri kumtema mwsho wa dirisha bahati mbaya likasogezwa mbele,good for simba.
 
Safi sana! Poleni watani!
Mchezaji hamumtaki, rufaa ya nini sasa??
 
na kwambia kwa msimu huu lazima Manji ang'atuke: OKWI tulia ufanye kazi yako, walikutamani kwa kutaka kuikomoa Simba, imewatokea puani .
 
Ni vyema tu ikaeleweka kwamba maamuzi haya siyo ya mwisho hata hapahapa Tz. Kuna mamlaka zaidi za maamuzi juu ya swala hili. Binafsi ninasubiri litavyoishia, sio lilivyoanzia.

Mkuu nadhani hata huko CAF, FIFA au CAS, Okwi ataibuka kidedea. Ukiniuliza kwanini? Sina Jibu, ila kwa sasa lets have a Cheers.
 
Emmanuel Okwi leo ameruhusiwa kuchezea Simba bila ya kulipa chochote baada ya kikao cha kamati ya sheria na haki za wachezaji kubaini kwamba hakua na mkataba na Yanga tokea January 2014.

Kwa Akili Yako Ulijua Asingeruhusiwa Kucheza Simba? Hakuna Watu MAFIA Nchi Hii Kama Friends Of Simba Na Wanajua Wanafanya Nini. TFF Waliogopa Baada Ya Evodius Mtawala Kutoa Siri Kwa Okwi Na Kumkabidhi Okwi Barua Yake Ya Kusitishiwa Mkataba Na Yanga Ambayo Hata Hivyo Ilifichwa Na Viongozi Wa TFF Na Najua Wengi Humu Tunamjua Kwani Huwa Anajitokeza Kama KAKAKUONA Vile Na Lengo Lake Na Baadhi Ya Viongozi Wenye Mahaba Na Yanga Waliomo TFF Walitaka Kuikalia Hiyo Barua Hadi Muda Wa Usajili Upite Kisha Ndipo Wajifanye Wanaitoa Kwa Kumpa Okwi Jambo Ambalo Kisheria Lingemfunga na Kumzuia Okwi Asiweze Kuihama Yanga Na Kuendelea Kukipiga Na Wana Jangwani. Mwanasheria EM Aliamua Kujitoa Kafara Na Kuonyesha Mapenzi Yake Ya Dhati Kwa Wekundu Wa Msimbazi Simba Sports Club Kwa Kutoboa Siri Hiyo Kubwa Kwa Viongozi Wa Simba Na Hadi Akawakabidhi Documents Zote Husika Huku Akiwashauri Nini Cha Kufanya Kisha Ndipo Huyu Kiongozi Wa TFF Aliposhikwa Na Hasira Na Kuamua Kumuondoa TFF EM ILA Akasahau Kuwa Bwana EM Hakutoka Tu Na Siri Za Okwi Na Yanga Bali Ana Siri Nyingine Nzito Za Uozo Wa TFF Na Laiti Leo Okwi Asingeidhinishwa Kukipiga Msimbazi EM Angemwaga Pumba Kwenye Kuku Wengi. Na Kwa Habari Nilizozinyaka Kutoka Kwa Credible Source Ndani Ya TFF Ni Kwamba TIMU YA JAMHURI KIHWELO YA MWADUI IMEAMRIWA KUPANDISHWA HADI LIGI KUU YA VODACOM NA SASA VIONGOZI WA TFF WANAHAHA JINSI YA KULIWEKA HILO SAWA KWANI WAKISEMA WAIPANDISHE MWADUI FC BASI TIMU KAMA KANEMBWA na AFRICAN LYON NAZO ZITALALAMIKA KWANI HATA NA ZENYEWE ZILIKUMBWA na UONEVYO WA AINA HIYO HIYO Wakati Rais ALIYEMALIZA MUDA WAKE LCT! TFF Wanatamani Sasa Ardhi Ipasuke ILI Wafiche AIBU na KASHFA Hii Kwani Kuna Mengine Ya Aibu Zaidi Na Muda Si Mrefu YATAFUMUKA.
 
Yanga wamwachie okwi acheze mpira, kwanza kiwango chake kimeporomoka sana!
 
Huu mpira wetu mgumu kuelewa siasa zake...hivi sisi tunaweza nini???
 
Mkuu kwani evodius kafukuzwa tff.?
 
kuhusu okwi kuzungumza na timu ya misri tff kufuatilia suala hilo huo ni unafiki kwa sababu kamati hiyo imeikataa mkataba yanga na okwi
 
Back
Top Bottom