Okwi aibwaga Yanga

Okwi aibwaga Yanga

naona leo una moody yakujibu kila comment inayohusu simba na okwi
Sina kawaida ya kubagua nyuzi yoyote mkuu, ukiniona kimya ujue nimekubaliana na hoja iliyotolewa kama ambavyo Yanga wamekubali leo.
 
Kwa Akili Yako Ulijua Asingeruhusiwa Kucheza Simba? Hakuna Watu MAFIA Nchi Hii Kama Friends Of Simba Na Wanajua Wanafanya Nini. TFF Waliogopa Baada Ya Evodius Mtawala Kutoa Siri Kwa Okwi Na Kumkabidhi Okwi Barua Yake Ya Kusitishiwa Mkataba Na Yanga Ambayo Hata Hivyo Ilifichwa Na Viongozi Wa TFF Na Najua Wengi Humu Tunamjua Kwani Huwa Anajitokeza Kama KAKAKUONA Vile Na Lengo Lake Na Baadhi Ya Viongozi Wenye Mahaba Na Yanga Waliomo TFF Walitaka Kuikalia Hiyo Barua Hadi Muda Wa Usajili Upite Kisha Ndipo Wajifanye Wanaitoa Kwa Kumpa Okwi Jambo Ambalo Kisheria Lingemfunga na Kumzuia Okwi Asiweze Kuihama Yanga Na Kuendelea Kukipiga Na Wana Jangwani. Mwanasheria EM Aliamua Kujitoa Kafara Na Kuonyesha Mapenzi Yake Ya Dhati Kwa Wekundu Wa Msimbazi Simba Sports Club Kwa Kutoboa Siri Hiyo Kubwa Kwa Viongozi Wa Simba Na Hadi Akawakabidhi Documents Zote Husika Huku Akiwashauri Nini Cha Kufanya Kisha Ndipo Huyu Kiongozi Wa TFF Aliposhikwa Na Hasira Na Kuamua Kumuondoa TFF EM ILA Akasahau Kuwa Bwana EM Hakutoka Tu Na Siri Za Okwi Na Yanga Bali Ana Siri Nyingine Nzito Za Uozo Wa TFF Na Laiti Leo Okwi Asingeidhinishwa Kukipiga Msimbazi EM Angemwaga Pumba Kwenye Kuku Wengi. Na Kwa Habari Nilizozinyaka Kutoka Kwa Credible Source Ndani Ya TFF Ni Kwamba TIMU YA JAMHURI KIHWELO YA MWADUI IMEAMRIWA KUPANDISHWA HADI LIGI KUU YA VODACOM NA SASA VIONGOZI WA TFF WANAHAHA JINSI YA KULIWEKA HILO SAWA KWANI WAKISEMA WAIPANDISHE MWADUI FC BASI TIMU KAMA KANEMBWA na AFRICAN LYON NAZO ZITALALAMIKA KWANI HATA NA ZENYEWE ZILIKUMBWA na UONEVYO WA AINA HIYO HIYO Wakati Rais ALIYEMALIZA MUDA WAKE LCT! TFF Wanatamani Sasa Ardhi Ipasuke ILI Wafiche AIBU na KASHFA Hii Kwani Kuna Mengine Ya Aibu Zaidi Na Muda Si Mrefu YATAFUMUKA.
Hivi ule msukule wa Yanga unaopenda kulia uwanjani unaifahamu hii? Ukifanikiwa kuiona hii safari lazima utajitundika kitanzi aiseeee....
 
Tokea kuumbwa kwa ulimwengu mpaka sasa Fisi anaendelea kusubiri mkono wa binadamu uanguke...
Nilidhani kauli yangu ile ingetosha kuzindua kwamba si busara kutamatisha swala ambalo bado liko kwenye mchakato. Huenda hatima ya yote, fisi akawa ndiyo mtu na mtu akageuka fisi. Niruhusu tulijadili hili litapofikia tamati, sio likiwa bado njiani.
 
Munataka kukata rufaa tena? Hivi hizo hela kwa nini musipeleke kuke Dogo dogo centre kwa wahitaji watoto yatima? Munashupalia kitu ambacho hamukihitaji ili iweje?
Kwa nini hela hizo musiongeze marupurupu ya wachezaji wenu?
unakosea sana kudhani mimi ni Yanga kwa sababu tu msimamo wangu kwa hili la Okwi umeelekea upande wa Yanga. Ila umesema sahihi kwamba Yanga huenda wakakata rufaa. Na ndio maana binafsi sioni haja ya kulijadili hili kwa sasa mpaka mchakato wa rufaa utakapomalizika.
 
Sina kawaida ya kubagua nyuzi yoyote mkuu, ukiniona kimya ujue nimekubaliana na hoja iliyotolewa kama ambavyo Yanga wamekubali leo.
Yanga niwaungwana siku zote ndomana wameendelea kuwa kimya
 
Mkuu nadhani hata huko CAF, FIFA au CAS, Okwi ataibuka kidedea. Ukiniuliza kwanini? Sina Jibu, ila kwa sasa lets have a Cheers.
Kati ya maneno yote hayo hapo juu, lenye uzito ni moja tu: 'nadhani'! Linafuatiwa na mawili mengine : 'Sina Jibu'. Kama nilivyokwishatangulia kunena, binafsi nasubiri mwisho wa safari hii, itakuwa ni kichekesho kuteremka garini wakati safari ikiwa ndio kwanza inaanza.
 
Manj wamemfix wenzake yeye ktk press conference alikuwa ana uhakika na anachosema kumbe wenzake walimzunguka ktk suala la usajili wa okwi kwa
 
Hivi Okwi aliisaidia nini Yanga msimu uliopita?....

Binafsi nimewashangaa sana Simba kwakumuacha Mosoti na kunrejesha Okwi....Kisiga, Singano, Chanongo, Kiongera na Amis Tambwe ni bora kuliko Okwi wa sasa...Ambaye haitwi hata timu ya Taiga...

Sioni hata sababu ya Yanga kumng'ang'ania Okwi...Labda kama wana lengo la kumkomoa kwa sababu tu ameenda Simba...

Sikuona umuhimu wa Simba kumsajili Okwi...Kama Okwi ana mapenzi ya dhati na Simba angeomba kwenda Simba(kutoka SC Villa) badala ya kwenda Yanga...

Tusishangae kusikia Okwi kalianzisha balaa lingine na Simba ifikapo Januari mwakani...

No wonder timu yetu ya Taifa inakuwa jamvi la wageni na wenyeji....Ni kwa sababu ya ubabaishaji wa viongozi wa Yanga na Simba...Hawa wanaweka ushabiki wa kijinga mbele kuliko kuangalia maendeleo ya soka...Viongozi wanasajili kishabiki bila kuangalia mahitaji ya timu/makocha...

Binafsi pamoja na ushabiki damu wa Yanga naipenda Azam FC inavyoendesha mambo yake...Wako so professional... Wanasajili kwa mahitaji ya Kocha, ndio maana sikushangaa walipomsajili Frank Domayo....

Azam mchezaji anasajiliwa na timu lakini Simba na Yanga mchezaji anasajiliwa na mtu(kumbuka mbwembwe za akina Bin Klein, Hans Pope, Seif Magari, Kaburu n.k)...

Azam wanatumia fedha kujenga na kuendeleza timu, Simba na Yanga wanatumia fedha kuwafurahisha mashabiki na baadae wanashindwa kuwalipa wachezaji na makocha...Rejea sakata la akina Wisdom Ndhlovu..Joseph Basena..Shikokoti...Liehwig na wengine..

Azam wanaboresha uwanja wao uchezwe mechi usiku Simba na Yanga wanaendelea na porojo zao za pori la Bunju na 'bahari' ya Jangwani...

Inasikitisha sana..
 
Hivi..!! Kiufundi nani muhimu SIMBA SC kati ya MUSOTI na OKWI..?!? nahis pengo la MUSOTI litaonekana. Tusubiri..!!
 
Okwi hawezi kuitwa timu ya taifa kwa sababu hajacheza mechi zozote za mashindano kwa muda mrefu. Hii haimaanishi si mchezaji mzuri. Subiri afanye mazoezi na mechi mbili tatu ndo utapata jibu lako kwa nini Simba wamemkubali kurudi. Mechi na Gor Mahia nina uhakika hukuiona, ungeiona ungeona dalili za Okwi yuuule. Alipiga krosi ya bao la kwanza baada ya kumzidi beki, na bao la pili alipiga shuti kipa akatema, messi akamalizia. Pamoja na hayo bado kiwango chake hakijifikia kinapotakiwa kutokana na kutokuwa fit.
Kuhusu maendeleo ya timu, nadhani ungeanza kuicheka timu yako ya Yanga inayong'ang'ania kujenga uwanja Jangwani, kuna eneo gani pale. Azam nakusapoti asilimia mia, wao wamepiga hatua na wana mfumo bora zaidi. Ila kama hujui kwa taarifa yako tu, hii siyo simba ya rage yenye ahadi nyingi za mdomoni. Ipe Simba miaka miwili. Anzia ofisini pale uone kinachofanyika..... Time will tell
 
Yanga niwaungwana siku zote ndomana wameendelea kuwa kimya
Ni kweli hata pale juzikati walipopigwa 5-0, 3-1 walikuwa kimyaaaa. Na hata pale Okwi alipotua Msimbazi Manji aliwaita Waandishi na kukaa kimya bila kuwaambia chochote.
 
Nilipita pale juzi nikakuta Kambale wazuri tu wanauzwa mtaani, nadhani ni product ya uwanjani kwetu ile.....
 
Ni kweli hata pale juzikati walipopigwa 5-0, 3-1 walikuwa kimyaaaa. Na hata pale Okwi alipotua Msimbazi Manji aliwaita Waandishi na kukaa kimya bila kuwaambia chochote.

sawa kabisa umepatia kumbe wewe mfuatiliaji mzuri sana
 
Mtaa wa pili bhana, leo ndo wanamuona Mosoti wa maana sana..

Kwanini kabla General Okwi ajatua Msimbazi mlikuwa hamsemi yote hayo?..

Tulileta beki toka Burundi, kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mosoti mkawa kimya..

Leo tumemtema Musoti, mnaanza kudai eti Mosoti alikuwa muhimu Simba, mara mnadai kuwa "time will tell"..

Mtaa wa pili hii huruma yenu kwetu mmeanza lini? Mbona hamko hivyo nyinyi?..
 
Halafu wameanza lini kufuatilia wellfare ya Msimbazi mbona Msimbazi hawana muda nao? Wasianze kujipendekeza kipigo kikali kiko palepale ukichanganya na mbaya wao karudi Msimbazi ndiyo balaaa kabisaaa....
 
Yanga haoooooo FIFA...
Yanga wanachekesha sana. Kamati yao ya sheria ndo inafikiria madudu hivi, au ndo mfa maji.... Sasa kama kisheria mkataba wao na Okwi ulishavunjika kwa kushindwa kutekeleza kipengele namba 8 cha mkataba, wanataka hayo madai yao mengine dhidi ya Okwi yasikilizwe kwa msingi upi? Okwi kajitetea kuwa walishindwa kutimiza matakwa ya mkataba kwa kushindwa kumlipa, hivyo mkataba umevunjika. Hawakuwa tena na uhusiano wa kimkataba na Okwi wakati mnapeleka malalamiko yenu. Na mkataba wao na Okwi ndo msingi wa malalamiko yao yote.

Sijui mchezaji wetu kaongea na klabu ya Misri wakati akiwa na mkataba, kasaini simba akiwa na mkataba na Yanga, sijui hajamtumikia mwajiri wake Yanga hivyo tunamdai fidia na kutaka mkataba uvunjwe. Haya madai yote hayawezi kusikilizwa, kwa sababu huo mkataba mnaoungelea haupo, mlishauvunja wenyewe jamani tusichoshane, msiwachoshe TFF wala FIFA. Mbona kila kitu kiko wazi sana, au mi mnazi wa upande wa pili ndo maana naona hivyo??? Hahaa, furaha ndogo ndogo hizi zinasongesha muda kiulaini..
 
Umenena vyema sana mkuu. Tarehe 12 october ni bora wasije tu taifa, mana gharika watakalokutana nalo kamwe hawatalisahau.
 
Yanga haoooooo FIFA...
Yanga wanachekesha sana. Kamati yao ya sheria ndo inafikiria madudu hivi, au ndo mfa maji.... Sasa kama kisheria mkataba wao na Okwi ulishavunjika kwa kushindwa kutekeleza kipengele namba 8 cha mkataba, wanataka hayo madai yao mengine dhidi ya Okwi yasikilizwe kwa msingi upi? Okwi kajitetea kuwa walishindwa kutimiza matakwa ya mkataba kwa kushindwa kumlipa, hivyo mkataba umevunjika. Hawakuwa tena na uhusiano wa kimkataba na Okwi wakati mnapeleka malalamiko yenu. Na mkataba wao na Okwi ndo msingi wa malalamiko yao yote.

Sijui mchezaji wetu kaongea na klabu ya Misri wakati akiwa na mkataba, kasaini simba akiwa na mkataba na Yanga, sijui hajamtumikia mwajiri wake Yanga hivyo tunamdai fidia na kutaka mkataba uvunjwe. Haya madai yote hayawezi kusikilizwa, kwa sababu huo mkataba mnaoungelea haupo, mlishauvunja wenyewe jamani tusichoshane, msiwachoshe TFF wala FIFA. Mbona kila kitu kiko wazi sana, au mi mnazi wa upande wa pili ndo maana naona hivyo??? Hahaa, furaha ndogo ndogo hizi zinasongesha muda kiulaini..
Yanga nawafananisha na mwanafunzi mbumbumbu aliyetoka chumba cha Mtihani na majigambo ya kufaulu kibao lakini badaye ilibainika alipata zero (0%) kwenye mtihani kwani hakuandika chochote.
Akihofia bakora za nyumbani mwanafunzi huyo atajaribu kufoji majibu sahihi ambayo hayakuwepo kabla na kurudi kwa mwalimu ili angalau apate maksi. Mwanafunzi huyo hata akikata rufaa kwa Afisa Elimu Taifa atakuwa anajisumbua tu, sifuri liko pale pale.....
 
Yanga si wageni kwenye hili wajameni, nikinukuu gazeti la Mwanaspoti......"Tuna mifano mingi ya karibuni ukiwamo ule wa Mrisho Ngassa, ambaye Yanga walilazimika kuilipa Simba ili wampate sababu ikiwa ni hiyo hiyo ya kumchukua bila kuheshimu mkataba.Ilikuwa hivyo hivyo kwa Mbuyu Twite, Yanga walimchukua bila kuheshimu makubaliano ya mchezaji huyo na klabu yake na Simba.Wachezaji wengine ambao Yanga walilazimika au wanatakiwa kuwalipa baada ya kukiuka mikataba ni Stephen Malashi, Mmalawi, Wisdom Ndlovu na Mkongomani Aime Lukunku."
 
Sorry kwa post ndefu lakini nadhani in vitu muhimu kwenye post hii.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UAMUZI WA KIHISTORIA WA KAMATI YA SHERIA NA HADHI YA WACHEZAJI YA TFF KATIKA SHAURI LA YANGA NA EMMANUEL OKWI

UTANGULIZI
Kwa niaba ya mteja wetu, Emmanuel Arnold Okwi, napenda kutoa maelezo kuhusu Uamuzi wa kihistoria katika soka la Tanzania ambao umefanywa na Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF. Uamuzi huo ni wa kihistoria kwa misingi ifuatayo:

MOSI: Ni mara ya Kwanza katika historia ya soka la Tanzania ambapo Kamati inakaa kujadili haki ya mchezaji dhidi ya klabu kubwa na hatimaye kuamua kwa manufaa ya mchezaji, tena pasipo kupiga kura kwa misingi ya upenzi na unazi. Kamati ya Mwanasheria Mashuhuri na mwenye Msimamo Bw. Richard Sinamtwa iliamua kustafsiri kanuni kwa kufuata ushahidi uliopo na kwa haki kabisa pasipo kujiingiza katika mtego wa kupiga kura kama ambavyo tumekua tukiiona huko nyuma.

PILI: Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti ilitumia busara ya hali ya juu kwa kukataa ombi la Yanga la kutengua uteuzi wa Bw. Hans Pope katika Kamati hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga ilileta hoja ya kumkataa Bw. Hans Pope kwa misingi ya mgongano wa kimaslahi na kumtaka mwenyekiti atoe uamuzi juu ya suala hilo. Endapo mwenyekiti angetoa maamuzi ya kumuondoa Hans Pope, basi angejiingiza katika uvunjaji wa Katiba ya TFF kwasababu yeye sio mamlaka ya uteuzi wa Hans Pope katika Kamati hiyo. Mwenye mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo Yanga walipaswa kuelewa hilo na si kuishinikiza kamati, hususan Mwenyekiti, amuondoe Hans Pope kwenye Kikao.

TATU: Maamuzi ya Kamati yamefungua njia kwa wachezaji wengi ambao mikataba yao inachezewa na vilabu kwa muda mrefu pasipo kuwa na nafuu yoyote ya kisheria kwa wachezaji hao ambao ndio nguzo ya muhimu katika mpira wa Tanzania. Hata hivi sasa kuna wachezaji ambao bado hawajalipwa stahili za mikataba yao ndani ya Yanga. Tunawaomba wajitokeze ili tuwasaidie wapate haki zao za kisheria kama ambavyo imetokea kwa Okwi.

NNE: Pamoja na madai ya Yanga ya kukata rufaa FIFA / CAS, naomba wajue kuwa haki yao ya kukata rufaa inatokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF imetekeleza wajibu wake. Uamuzi huo wa Kamati umejenga msingi muhimu sana katika suala zima la kuheshimu na kutekeleza mikakaba kwa mujibu wa kanuni za FIFA. Endapo Yanga watakata rufaa kama wanavyodai, itakuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha nguzo ya kuheshimu mikataba ya wachezaji inapewa msisitizo unaostahili.

MGOGORO KATI YA YANGA NA OKWI
Mkataba wa Yanga na Okwi, ambao ulisainiwa tarehe 12 Disemba 2014 umekuwa na mapungufu yafuatayo:
1. Mkataba huo umempa majukumu mchezaji kufuatilia ITC na suala zima la yeye kupata vibali vya kucheza. Hii ni kinyume na Kanuni za FIFA ambao zinatamka bayana kuwa jukumu la kufuatilia ITC ni la wanachama wa FA, lakini Yanga walimtwisha Okwi zigo hilo. Okwi alitekeleza jukumu hilo.
Kamati ililiona hilo na kusema wazi kuwa hilo sio sahihi. Ni vema wachezaji wajue kuwa hilo sio jukumu lao.
2. Pili Yanga, kwa mujibu wa mkataba, walikuwa na haki ya kumkata mchezaji theluthi moja ya mshahara wake wa mwezi endapo atakosa mechi tatu au zaidi. Yanga walimkata Okwi Mishahara ya miezi mitano, kinyume na matakwa ya mkataba na pasipo maelelzo yoyote.
3. Yanga na Okwi walikubaliana kuwa mchezaji atalipwa ada ya kusaini mkataba (signing on – fee) ya US$ 100,000, kwa Awamu mbili. Awamu ya kwanza wakati wa kusaini mkataba na awamu ya pili tarehe 27 Januari 2014. Mpaka hivi sasa, Yanga wamelipa US$ 50,000 tu na bado kuna deni la US$ 50,000. Huu ni uvunjaji wa mkataba wa wazi kabisa.
4. Kipindi chote mchezaji akiwa na klabu ya Yanga, hajapewa nyumba kama ambayo walikubaliana. Huu ni ukiukwaji mwingine wa mkataba.

Baada ya Okwi kuanza kudai haki zake tajwa hapo juu, Yanga waliamua kutomlipa mteja wetu mishahara ya miezi mitano kinyume na matakwa ya mkataba kati yao.

MPANGO WA SIRI WA YANGA
Yanga walikuwa na mpango wa siri wa kuvunja mkataba na Emmanuel Okwi ili wamkomoe mteja wetu, ashindwe kucheza mpira, kiwango chake kiporomoke na itumike kama onyo kwa wachezaji wengine ambao wanadai haki zao. Mpango huu ulitekelezw kama ifuatavyo:

a. Tarehe 27 Juni 2014, Yanga waliandika barua kwenda TFF, ikiitaka TFF, pamoja mambo mengine, itambue kuwa mkataba kati yao na Okwi umefutwa. Barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
b. Tarehe 25 Julai 2014, Yanga waliandika barua ya pili kukumbushia barua yao ya tarehe 27 Juni 2014. Barua hiyo ya pili haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
c. Tarehe 20 Agosti 2014 Yanga waliandika barua nyingine tena wakikumbushia hoja zao tajwa hapo juu. Kwa mara ya tatu, barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
d. Yanga waliandika barua nyingine ya nne tarehe 25 Agosti 2014 ikiwa na hoja zile zile za kusitisha mkataba na mteja wetu. Kwa mara ya nne barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.

Baada ya TFF kupanga tarehe ya kikao cha Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji na kutoa barua ya wito tarehe 27 Agosti 2014 ndipo kwa mara ya kwanza mchezaji Emmanuel Okwi akafahamu kuwa Yanga wameomba kuvunja mkataba wake.

Tarehe 27 Agosti 2014, Emmanuel Okwi aliiandikia Yanga KUKUBALI ombi lao la kuvunja mkataba.

Mambo muhimu ya kujiuliza ni:

Mosi, Kama Mkataba ulikuwa ni kati ya Yanga na Okwi, ni kitu gani kiliifanya Yanga ishindwe kumpa angalau nakala ya barua nne ambazo ilizipeleka TFF?

Pili, Wakati Yanga wanaomba kuvunja mkataba, walikuwa wameshamlipa Okwi stahili zake kwa mujibu wa Mkataba huo?

Tatu, Je visingizio vya kuvunjwa kwa mkataba wa Okwi vina uhusiano na idadi ya majina ya wachezaji wa kigeni wa Yanga?

Ni bayana kuwa Yanga walitafuta kila aina ya kisingizio ili mteja wetu aonekane kuwa ndio amevunja mkataba wakati ni wazi kuwa Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja mkataba huo tarehe 27 Januari 2014 kwa kushindwa kumlipa mteja wetu US$ 50,000 za ada ya kusaini mkataba.

HOJA MBELE YA KAMATI
Mbele ya Kamati Yanga walileta hoja kuwa: Hans Pope ana mgongano wa maslahi kwa kuwa amemsajili Okwi Simba na yeye ni mjumbe wa Kamati hii; Okwi amekataa kuongeza au kupunguza mkataba kama ilivyopendekezwa na Yanga; Okwi ameleta madai yasiyo na msingi ya kutaka apewe nyumba ya kuishi; hajacheza mechi 6 hivyo kuikosesha Yanga ubingwa. Okwi amefanya makubaliano na Klabu ya Wadi Geldi ya Misri wakati ana mkataba na Yanga. Hivyo basi Yanga waliitaka Kamati itamke kuwa mkataba kati yao na Okwi umesitishwa, imfungie Okwi kucheza mpira Tanzania Maisha na ailipe Yanga dola za kimarekani laki mbili.

Tukimwakilisha Okwi, tulitoa hoja kuwa: Mteja wetu amekubali ombi la Yanga la kuvunja mkataba ambalo limo katika barua zake nne; Yanga ndio wamevunja mkataba kwa kushindwa kulipa signing fee US$ 50,000; Mishahara ya miezi mitano US$ 15,000 na kodi ya nyumba US$ 2,800. Madai hayo ni kwa mujibu wa mkataba.

Baada ya Maswali toka kwa Kamati kwa pande zote mbili, Yanga waliomba kufuta barua zao, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na kamati.

Kamati, hatimaye ilifanya maamuzi ya kihistoria katika kulinda haki za kimkataba za wachezaji kama ambayo imeelezwa hapo juu. Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, anapaswa kuipongeza kwa dhati kamati kwa maamuzi ambayo wanajenga mpira wa nchi hii. Vilabu vinapaswa kufahamu kuwa haki za mchezaji lazima ziheshimiwe.

Hoja za Yanga kuwa hakukuwa na madai ya fedha sio sahihi kwasababu Majibu toka kwa Okwi na mabishano ya maneno mbele ya kamati hiyo ilijadili kwa kina madai ya fedha ya Okwi na hata Yanga walikiri kutolipa madai hayo. Hivyo basi si sahihi kusema kuwa eti suala la madai ya fedha halikujadiliwa. (ona kiambatisho MNA1)

Msingi wa malalamiko ya Yanga ni barua ya tarehe 27 Juni 2014, ambayo hakuna sehemu ambayo inatamka suala la Simba. Kama kuna kesi dhidi ya Simba, wasubiri wakati wa kupitia pingamizi za usajili lakini suala ambalo Yanga walilalamikia ni kusitisha mkataba na Okwi na madai ya fidia.

Kamati ya Sheria na Mwenyekiti wake hawana mamlaka ya kujadili uteuzi au uwepo wa Hans Pope kwenye kikao hicho. Mamlaka ya Uteuzi ndio, kwa mujibu wa katiba ya TFF, yenye uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo.

Kwa kuwa rufaa ni haki ya kila mtu, Uamuzi wa kukata rufaa Fifa / CAS ni haki ya kisheria lakini tuwakumbushe Yanga kuwa"UKITAKA HAKI, TENDA HAKI KWANZA".

DK DAMAS DANIEL NDUMBARO (PhD)
Maleta & Ndumbaro Advocates

Mawakili wa Mchezaji
 
Back
Top Bottom