Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Hao wametumwa kwenda kumwongezea umaarufu.Nyani ,
Mambo mengi yanayofanyika Afrika ayaingii akilini kabisa na mtu ukiyafuatilia sana unaweza kuwa Schizophrenia....Cha kushangaza zaidi mwaka 2010 hao wazee wote wanaodai mafao yao watampigia kura Kikwete...
Nyani ,
Mambo mengi yanayofanyika Afrika ayaingii akilini kabisa na mtu ukiyafuatilia sana unaweza kuwa Schizophrenia....Cha kushangaza zaidi mwaka 2010 hao wazee wote wanaodai mafao yao watampigia kura Kikwete...
Ninavyoona mimi hili hata si tatizo la Ikulu.. hili ni tatizo la Bunge, ningekuwa mimi ni hawa wazee ingekuwa ni kupiga kampeni Bungeni na kuwatishia wabunge kuwa wasiposupport haki yao basi wazee hawa watatumia nafasi yao kuwapiga vita. Tatizo ni kuwa wazee wenyewe sitoshangaa kuwa wengi ni wanachama wa CCM hivyo hawaoni kuwa matatizo yao yameunganamana na chama tawala na wabunge wao.
Tatizo ni kuwa wazee wenyewe sitoshangaa kuwa wengi ni wanachama wa CCM hivyo hawaoni kuwa matatizo yao yameunganamana na chama tawala na wabunge wao.
Watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiwa wanaendelea kupiga kambi nje ya Ikulu ya Mtukufu Rais Mpendwa wa Watu aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya wapiga kura ambaye chama chake kinapendwa na kukubalika na wananchi wengi na ambaye ni Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Chaguo la Mungu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Siku chache zijazo, mmoja wao atafia kwenye lango la Ikulu.
Hii ni leo
Wiki iliyopita
Ina maana kuwa katika Taifa letu, katika safu nzima ya uongozi, kuanzia wale waliotangulia na wale ambao wanashikilia nafasi zao hadi hivi sasa, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kutumia kiungo kiitwacho Ubongo kutatua mara moja na daima tatizo la wastaafu hawa wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Ushauri:
Kwa vile Ikulu, ofisi ya Waziri Mkuu na idara nyingine zote hazina watu wenye uwezo wa kufikiria utatuzi wa tatizo kama hili na ambao wameamua kutolijali wala kukosa usingizi kwalo basi hatuna budi wazalendo kutaka serikali ifanye kitu ambacho angalau tunajua inaweza.
Serikali iagize wataalamu toka Ubelgiji au Sweden wawape ushauri wa jinsi gani ya kuweza kufikiria njia ya kumaliza tatizo la wazee wetu hawa ambao waliitumikia nchi yao kwa uaminifu na sasa wanasota juani kudai (siyo kuomba) haki inayotokana na jasho lao.
Ikiwezekana serikali itoe mwaliko kwa nchi kama Uingereza au Marekani wawatangazie kama kuna mtu anayeweza kuja kufikiria kwa niaba yao jinsi ya kulimaliza jambo hili kabla wazee wetu hawa wote hawajatuacha kabla ya kupokea fidia ya jasho la utumishi kwa nchi yao.
Wiki
Hofstede nakubaliana na wewe,Mkjj ninakuhakikishia kuwa 90% ya wana CCM wanajiunga na chama wakitarajia kupata upendeleo fulani na hasa msaada lakini si waabudu wa kweli wa DINI ya CCM. Kwani wanajua kabisa kuwa CCM ndio iliyowafanya wafikie hatua hii ya umasikini kwa wachache kujilimbikizia mali, ila ukijitenga nao utakosa hata nafasi ya kumuomba muheshimiwa shs 1000 ya mafuta ya taa, sasa kipi bora ni kujifanya unamsapoti ili akuruzuku kwa hela zako mwenyewe alizokuibia.
Mkuu nadhani katika ushauri laini lakini ambao ni powerful niliowahi kuuona hapa tangu niingie (ingawa ni mgeni), huu ni ushauri mzito sana, nadhani lingekuwa jambo ambalo kwanza ni la amani, pili halihitaji nguvu, lakini impact yake ingekuwa mbaya sana upon ccm. Hatuna mtoto au mjukuu wa mmoja wa hawa wazee tuwashauri hilo mkuu???Mimi naamini hawa wazee wakiamua kutangaza kuwa wameamua kuzirudisha kadi za CCM na kuziacha hapo Ikulu itakuwa ni big news kuliko wao kudai fedha zao, na ninawahakikishia kina Makamba na Chiligati watakimbia kuzungumza nao. Kumbukeni Ibara ya 15:1
[B said:Mzee Mwanakijiji;253065[/B]]Watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiwa wanaendelea kupiga kambi nje ya Ikulu ya Mtukufu Rais Mpendwa wa Watu aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya wapiga kura ambaye chama chake kinapendwa na kukubalika na wananchi wengi na ambaye ni Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Chaguo la Mungu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Siku chache zijazo, mmoja wao atafia kwenye lango la Ikulu.
Hii ni leo
Wiki iliyopita
Ina maana kuwa katika Taifa letu, katika safu nzima ya uongozi, kuanzia wale waliotangulia na wale ambao wanashikilia nafasi zao hadi hivi sasa, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kutumia kiungo kiitwacho Ubongo kutatua mara moja na daima tatizo la wastaafu hawa wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
[B said:La kuhuzunisha ni kuwa serikali ilikabidhiwa hizi fedha iwafikishie hao wastaafu zaidi ya miaka 30 iliyopita. Pamoja na kwamba zilikuwa ni fedha zao zilizotokana na makato kwenye mishahara yao wakati wakitumikia hiyo jumuiya, serikali kwa makusudi yasiyoeleweka iliamua kuzitumia kinyume na ilivyotarajiwa. Ukweli ni kuwa serikali iliamua kuwaibia hawa wananchi wake mchana kweupeee.
Ule uwezo wa kuibana serikali ndio hawa wazee hawana na si kweli kwamba wana ubia wowote na serikali ya CCM. Wabunge wengi wa CCM wa sasa inawezekana walishiriki kikamilifu katika kutafuna fedha hizo kutokana na nyadhifa walizokuwa nazo wakati huo. Hata hivyo ombi liende kwa wachache wao ambao wameonyesha kuwatetea wananchi walivalie njuga kuwasaidia hawa wazee.
MzMwkjj. naomba kusemea juu ya picha Hizi kwa kutoa mfano ufuatao:Wasanii huchora picha fulani hivi,halafu huwaachia watizamaji/Mlengwa kufanya tafsiri juu ya yatakayo onekana katika picha hizo.Watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiwa wanaendelea kupiga kambi nje ya Ikulu ya Mtukufu Rais Mpendwa wa Watu aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya wapiga kura ambaye chama chake kinapendwa na kukubalika na wananchi wengi na ambaye ni Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Chaguo la Mungu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Siku chache zijazo, mmoja wao atafia kwenye lango la Ikulu.
Hii ni leo
Wiki iliyopita
.