Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,491
Watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiwa wanaendelea kupiga kambi nje ya Ikulu ya Mtukufu Rais Mpendwa wa Watu aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya wapiga kura ambaye chama chake kinapendwa na kukubalika na wananchi wengi na ambaye ni Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Chaguo la Mungu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Siku chache zijazo, mmoja wao atafia kwenye lango la Ikulu.
Hii ni leo
Wiki iliyopita
Ina maana kuwa katika Taifa letu, katika safu nzima ya uongozi, kuanzia wale waliotangulia na wale ambao wanashikilia nafasi zao hadi hivi sasa, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kutumia kiungo kiitwacho Ubongo kutatua mara moja na daima tatizo la wastaafu hawa wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Ushauri:
Kwa vile Ikulu, ofisi ya Waziri Mkuu na idara nyingine zote hazina watu wenye uwezo wa kufikiria utatuzi wa tatizo kama hili na ambao wameamua kutolijali wala kukosa usingizi kwalo basi hatuna budi wazalendo kutaka serikali ifanye kitu ambacho angalau tunajua inaweza.
Serikali iagize wataalamu toka Ubelgiji au Sweden wawape ushauri wa jinsi gani ya kuweza kufikiria njia ya kumaliza tatizo la wazee wetu hawa ambao waliitumikia nchi yao kwa uaminifu na sasa wanasota juani kudai (siyo kuomba) haki inayotokana na jasho lao.
Ikiwezekana serikali itoe mwaliko kwa nchi kama Uingereza au Marekani wawatangazie kama kuna mtu anayeweza kuja kufikiria kwa niaba yao jinsi ya kulimaliza jambo hili kabla wazee wetu hawa wote hawajatuacha kabla ya kupokea fidia ya jasho la utumishi kwa nchi yao.