Ok.. somebody explain this (Picha)

Mwalimu Nyerere alisema"....Kuna biashara gani Ikulu.... Ukiona mwenzenu ananunua kura kwa ajili ya kuingia Ikulu muogopeni kama Ukoma.... Ikulu ni mahala patakatifu. Ukiwa Ikulu ukapita barabarani elewa kila unayemuona na kila mwenye shida matatizo yake yanakuhusu.... kuna biashara gani Ikulu?????"

Aliyoyasema sasa yako wazi Nyerere ni Nabii
 
Watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiwa wanaendelea kupiga kambi nje ya Ikulu ya Mtukufu Rais Mpendwa wa Watu aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya wapiga kura ambaye chama chake kinapendwa na kukubalika na wananchi wengi na ambaye ni Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Chaguo la Mungu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Siku chache zijazo, mmoja wao atafia kwenye lango la Ikulu.

1216826425_wasitaafu_ikulu.jpg

Hii ni leo

1216042751_3web.jpg

Wiki iliyopita

Ina maana kuwa katika Taifa letu, katika safu nzima ya uongozi, kuanzia wale waliotangulia na wale ambao wanashikilia nafasi zao hadi hivi sasa, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kutumia kiungo kiitwacho Ubongo kutatua mara moja na daima tatizo la wastaafu hawa wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Ushauri:
Kwa vile Ikulu, ofisi ya Waziri Mkuu na idara nyingine zote hazina watu wenye uwezo wa kufikiria utatuzi wa tatizo kama hili na ambao wameamua kutolijali wala kukosa usingizi kwalo basi hatuna budi wazalendo kutaka serikali ifanye kitu ambacho angalau tunajua inaweza.

Serikali iagize wataalamu toka Ubelgiji au Sweden wawape ushauri wa jinsi gani ya kuweza kufikiria njia ya kumaliza tatizo la wazee wetu hawa ambao waliitumikia nchi yao kwa uaminifu na sasa wanasota juani kudai (siyo kuomba) haki inayotokana na jasho lao.

Ikiwezekana serikali itoe mwaliko kwa nchi kama Uingereza au Marekani wawatangazie kama kuna mtu anayeweza kuja kufikiria kwa niaba yao jinsi ya kulimaliza jambo hili kabla wazee wetu hawa wote hawajatuacha kabla ya kupokea fidia ya jasho la utumishi kwa nchi yao.

Very ironical and sarcastic especially the very first paragraph.
Hizi picha zinaonyesha na kudepict hopelessness and despair.Sababu ni viongozi ambao hawajali maslahi ya umma zaidi ya matumbo yao na watoto wao.
 
I guess kuwa Mkuu wa kaya huwa hasikilizi ushauri wa mtu bali mambo mengi huwa anaamua mwenyewe na kama anamshirikisha mtu basi atakuwa labda mke wake. Tujaribu kuangalia ni mambo mangapi yamefanywa hapa nchini na yakatolewa ushauri ambao ulihitaji utekelezaji tu lakini hakuna kilichofanyika, mfano: ripoti ya uchunguzi juu ya ufisadi ndani ya EPA, tume ya Dr. Mwakyembe, kamati ya kupitia mikataba ya madini, zote hizi zilitoa mapendekezo lakini hakuna kilichofanyika. Kuna msemo unaosema "MBWA MZEE HAFUNDISHWI SHERIA MPYA".
 
Ushauri:
Kwa vile Ikulu, ofisi ya Waziri Mkuu na idara nyingine zote hazina watu wenye uwezo wa kufikiria utatuzi wa tatizo kama hili na ambao wameamua kutolijali wala kukosa usingizi kwalo basi hatuna budi wazalendo kutaka serikali ifanye kitu ambacho angalau tunajua inaweza.

Serikali iagize wataalamu toka Ubelgiji au Sweden wawape ushauri wa jinsi gani ya kuweza kufikiria njia ya kumaliza tatizo la wazee wetu hawa ambao waliitumikia nchi yao kwa uaminifu na sasa wanasota juani kudai (siyo kuomba) haki inayotokana na jasho lao.

Ikiwezekana serikali itoe mwaliko kwa nchi kama Uingereza au Marekani wawatangazie kama kuna mtu anayeweza kuja kufikiria kwa niaba yao jinsi ya kulimaliza jambo hili kabla wazee wetu hawa wote hawajatuacha kabla ya kupokea fidia ya jasho la utumishi kwa nchi yao.
[/B

Nadhani ni ushauri mzuri sana huu mwanakijiji, Lakini pia kwa kuongezea Iundwe tume ya Wataalamu na bajeti yao iwe ni fedha kidogo tu zisizozidi milioni mia nne tu hivi.Wakae Bagamoyo pale paradiso resort kwa majuma mawili na kupeleka ripoti kwa Mheshimiwa Rais baada ya miezi mitatu kisha raisi naye akae na wachambuzi wake kwa muda mdogo tu usiopungua miezi miwili ili kuona ni jinsi gani mapendekezo ya ripoti yatakavyofanyiwa kazi.
 
Time will tell, ipo siku wataamua kutakana kuvuka lile lango hata kama kunatakiwa mwaliko.

Bora kukopesha mapesa na nyingine wapeane kuliko kumalizana na watu hawa, kwani nani anawajua katika ile dini yao?
 
Jk Amezidi Kuwa Kimya.......alimpa Hiyo Dhana Yake ..alimdanganya SIO KILA JAMBO LITAAMULIWA NA UKIMYA??SIO KWELI KABISAAA
 
The Beginning of the End of misery?


Serikali yawakumbuka wastaafu EAC


na Irene Mark, Dodoma


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameiagiza Wizara ya Fedha na Uchumi, kutangaza majina yote ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), waliolipwa na ambao hawajalipwa, lakini hundi zao zipo tayari.

Pinda, alitoa agizo hilo jana mjini Dodoma, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge.

Kauli ya waziri mkuu ilitokana na swali la Mbunge wa Wawi na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid (CUF), aliyetaka kujua sababu za serikali kutofanyia kazi malipo ya wastaafu wa iliyokuwa jumuiya hiyo.

“Waziri Mkuu, mwaka 2003, wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliahidiwa na serikali kwamba wangelipwa mafao yao yote. Leo, Watanzania wanashuhudia wastaafu hao wakilala Ikulu. Kwa nini serikali haijalifanyia kazi suala lao?” alihoji kiongozi huyo na kuishauri serikali kuunda kamati ya Bunge kusaidia suala hilo.

Katika majibu yake Pinda, alisema kwa sehemu kubwa, Serikali ya Awamu ya Nne imelishughulikia suala hilo, na kwamba ameiagiza Wizara ya Fedha na Uchumi kutoa matangazo ya malipo yaliyofanyika.

“Nimemwambia Waziri wa Fedha tutoe kwenye magazeti majina ya wastaafu waliolipwa, hundi zaidi ya 6,000 zilizoharibika kwa sababu wahusika hawajazifuata na nyingine 200 zipo tayari.

“Mimi nadhani, jambo hili linafanyika kwa masilahi fulani. Watu wanachangiwa fedha ili wawe wasemaji wa wastaafu wale…na kwa kweli sifurahii kuwaona wanalala Ikulu pale,” alisema Pinda.

Kuhusu kuundwa kwa kamati ya Bunge itakayoshughulikia suala la wastaafu hao, waziri mkuu alipokea ushauri wa mbunge huyo na kusema, serikali ipo tayari kufanya hivyo lakini muda utakapofika.

Hivi karibuni wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa katika ziara ya siku tisa mkoani Tanga, wastaafu wa iliyokuwa jumuiya hiyo kutoka sekta zake mbalimbali waliweka kambi nje ya lango kuu la kuingilia Ikulu wakishinikiza kulipwa fidia yao.

Aidha, waziri mkuu huyo pia alisema ni lazima kuwekeza kwenye gesi ili kuondokana na kupanda kwa bei ya mafuta kunakoathiri ukuaji wa uchumi na kusababisha kupanda kwa bei za vyakula.

Pinda, alisema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Muhonga Ruhwanya (Chadema), aliyetaka kufahamu serikali inakabilianaje na changamoto ya kupanda kwa bei ya mafuta inayoathiri sekta ya usafirishaji.

Katika hilo alisema, serikali inaiomba EWURA, huku akisisitiza uwekezaji kwenye nishati mbadala ya gesi.

“Natamani siku moja hata magari yatumie gesi. Hii nadhani itatusaidia sana kuondokana na gharama za mafuta,” alisema.

Aidha, mbunge huyo aliishauri serikali kuongeza kodi kwa wawekezaji ili kiwango kinachopatikana kipelekwe kama ruzuku kwenye mafuta na kuwapunguzia mzigo wananchi.

Hata hivyo, waziri mkuu alipokea ushauri huo na kuahidi kulifikisha wazo la mbunge huyo kwa Waziri wa Fedha na Uchumi lakini wakishindwa watalieleza Bunge sababu.

“Ni wazo zuri. Tutalipeleka kwa Waziri wa Fedha na tukishindwa tutarudi kwenu waheshimiwa wabunge na kusema kwa nini tumeshindwa,” alisema Pinda.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), alimtaka waziri mkuu kueleza iwapo Serikali ya Awamu ya Nne itaweza kutekeleza baadhi ya mambo katika Ilani ya CCM ya mwaka 2005, likiwamo la kusambaza huduma ya maji ifikapo mwaka 2010.

“Ilani ya uchaguzi inasema hadi kufikia mwaka 2010, asilimia 90 ya wakazi wa mjini watapata maji safi na salama na asilimia 65 kwa wakazi wa vijijini, waziri mkuu unadhani lengo hili litafanikiwa?” alihoji Serukamba.

Katika majibu yake, Pinda alimtaka mbunge huyo na wananchi wote kuvuta subira ili kuona litakalotokea, ingawa anaaamini lengo hilo linaweza kufikiwa kwa kiwango kikubwa.
 
Wastaafu EAC kukutana na Luhanjo leo

na Esther Mbussi


WAFANYAKAZI wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo wanatarajia kukutana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kujadili mustakabali wa malipo ya mafao yao.

Wastaafu hao walipewa barua juzi iliyowataka kuwachagua wawakilishi saba kati yao ili waweze kuonana na Luhanjo, leo saa saba mchana.

Walisema nia yao ya kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete ni kutaka kumwambia ukweli kuhusu kuzungushwa malipo ya mafao yao na kusikia kauli yake, kwa madai kuwa wasaidizi wake wamekuwa wakimpa taarifa potofu kila wanapotaka kumwona.

Awali Mwenyekiti wa wastaafu hao, Nathaniel Mlaki, alipinga kuonana na Luhanjo, wakisisitiza kuonana na Rais Kikwete, kwani walishawahi kufanya naye mazungumzo, bila mafanikio.

Wastaafu hao zaidi ya 50, juzi waliweka kambi nje ya lango la kuingilia Ikulu, wakitaka kuonana na Rais Kikwete, lakini walizuiliwa kwa kutofuata taratibu.

Wastaafu hao, walikuwa wamebeba mabango yaliyosomeka: "Ufisadi ulianzia katika mafao yetu" na "Msafisheni Nyerere kwa kulipa deni lake la stahili ya mafao kwa ukamilifu."

Licha ya kuzuiliwa juzi, jana wazee hao walifika tena Ikulu kwa lengo hilo hilo, huku wakiwa na watoto na wajuku zao ili kumwonyesha rais jinsi wanavyopata shida, huku fedha zao zikishikiliwa na serikali.

Jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, kumpatia orodha ya majina ya wastaafu hao waliokwishalipwa na wengine ambao bado hawajalipwa. Pia alitaka majina hayo yatangazwe kwenye vyombo vya habari.
 
Wajameni

Huwa tunalalama sana juu ya utoaji ajira ktk asasi mbalimbali,mara nyingi tumekuwa tukisema waislamu wahapewei fursa ktk ajira,mara ooohhhh watoto wa wakubwa tuuu ndio wanapewa.

Tazama picha kwa umakini,asilimia kubwa (roughly 90%) ya wastaafu hawa,wanatambulika kama waaumini wa dini ya kiisalamu,why?

Wakrsito tutangaze mgogoro wa kulipywa mafao yao hawa mabwana.
 
kwakweli ili taifa lina tia haibu sana kweli serikali iko teyari kutia saini mikataba fake na kuitetea wakati wananchi wake wakiteseka tena wazee kama hawa na raisi naye 2010 akawaombe kura hawa hawa wazee!! its annoying kwakeli
wakati viongozi hawa hawa wanachukua mikopo minono kwenye mashirika bila masharti dah kunasiku wimbo wa taifa ile sehemu ya wabariki viongozi wake itafutwa!!!
 
Wajameni

Huwa tunalalama sana juu ya utoaji ajira ktk asasi mbalimbali,mara nyingi tumekuwa tukisema waislamu wahapewei fursa ktk ajira,mara ooohhhh watoto wa wakubwa tuuu ndio wanapewa.

Tazama picha kwa umakini,asilimia kubwa (roughly 90%) ya wastaafu hawa,wanatambulika kama waaumini wa dini ya kiisalamu,why?

.....Mhh! haya bwana,baadhi ya tafsiri zaanza kujitokeza juu ya picha hizo.
**Mkombosi,may be JK is thinking what you are thinking.
 
Just thinking from different angle!

Assuming you are an accountant of ministry of finance! the mzee wa africa mashariki come without any document or anything else to identify him/her as legal forma eac employee. and say nilikuwa nafanya kazi EAC! well he is real tired and probably about to fall down.

Utafanya nini?
 
Just thinking from different angle!

Assuming you are an accountant of ministry of finance! the mzee wa africa mashariki come without any document or anything else to identify him/her as legal forma eac employee. and say nilikuwa nafanya kazi EAC! well he is real tired and probably about to fall down.

Utafanya nini?

wrong.. accountant wa ministry of finance should not even consider handling this... so the question is based on a flawed assumption.
 
Nyani ,

Mambo mengi yanayofanyika Afrika ayaingii akilini kabisa na mtu ukiyafuatilia sana unaweza kuwa Schizophrenia....Cha kushangaza zaidi mwaka 2010 hao wazee wote wanaodai mafao yao watampigia kura Kikwete...

Acheni wapewe mafao yao...basi !!
 
Just thinking from different angle!

Assuming you are an accountant of ministry of finance! the mzee wa africa mashariki come without any document or anything else to identify him/her as legal forma eac employee. and say nilikuwa nafanya kazi EAC! well he is real tired and probably about to fall down.

Utafanya nini?

Kasheshe,

Ndugu yangu haya madai ya waliokuwa wastaafu wa EAC, ni tofauti kabisa na madai ya wastaafu wa serikali ya Tanzania. Serikali ya Tanzania ilikabidhiwa hizo fedha kwa sababu moja tu - haikuwa rahisi kuwapata wahusika baada ya juvunjika kwa jumuiya na Serikali iliaminiwa kuwa haiwezi kula hela za wananchi wake na pia ndio yenye uwezo wa kuwatafuta na kuwafikia hawa wadai.

Rekodi zote zinazowahusu wastaafu na formula ya kuwalipa ilikabidhiwa serikali pamoja na kiasi walichotakiwa kulipwa - huo ulikuwa ni mwaka 1977 na malipo yangeanza mwaka 1985 baada tu ya zoezi la ugawaji wa mali za EAC kukamilka mwaka 1984. Fedha zilihifadhiwa benki kuu ya Tanzania na haijulikani sababu zilizoifanya serikali ya awamu ya pili isianze kulipa mara moja.

Wastani wa malipo kwa wakati huo haikuwa chini ya dola $10,000 (Tshs.20,000,000) kwa kila moja. Ajabu ni kuwa katika awamu ya kwanza ya malipo mwaka 2005 ( miaka zaidi ya 30 baadaye) waliambulia kupata wastani Tshs. 2,000,000 ($1,000) kwa kila moja tu. Huu ndio unaitwa wizi unaofanywa na dola dhidi ya wananchi wake.
 
wazeebc.jpg



Picha na Father Kidevu.


Imagine huyu ni uncle au babako.
Je, sisi au wenetu wataepuka adha ya namna hii?





SOURCE

.
 
Back
Top Bottom