Ogopeni vyakula vinavyouzwa supermarkets

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,704
Napenda kushauri watanzania wenzangu, tusipende kutumia bidhaa za supermarket sana, iwe maji, sukari, maziwa, kuku n.k

Nimegundua bidhaa nyingi zinakuwa mbovu lakini sisi tunaamini supermarket ndiko wanakouza bidhaa bora. Bidhaa nyingi zinakuwa zimepitwa muda wa matumizi yake wanafanya kubadilisha label hii inatokana na sababu ya kuwa wanaleta stock kubwa ambayo haishi kwa muda unaotakiwa.

Naongea jambo ambalo nimeshuhudia na TFDA wanalijua hili lakini hawachukui hatua kutokana na kwamba nchi iko corrupted na supermarkets nyingi zinamilikiwa na wafanya biashara ambao ni rafiki wa viongozi wa nchi hii au viongozi pia ni wana hisa.

Ni bora kununua bidhaa kutoka masoko yetu ya kiswaz au gengeni au haya maduka ya kawaida maana wale hawana uwezo wa kuagiza stock kubwa kubwa.

Mwenye kusikia na aasikie.
 
What about upande wa bidhaa feki..maana uswahilini ndio kumejaa bidhaa feki..hasa maziwa ya watoto
 
mkuu nimekusoma hapa asante kwa taarifa hii

Mwenye kusikia na aasikie...
 
yaani hakuna pa kukimbilia ndugu yaani kotekote kuna faida na hasara pia ila naona uswahiliini ndiko kuzur zaidi
What about upande wa bidhaa feki..maana uswahilini ndio kumejaa bidhaa feki..hasa maziwa ya watoto
 
Ni ulimbukeni tu,Kuna bidhaa za kununua supermarket,kuku wote wazuri wa kienyeji katika masoko yetu,mtu anaenda kununua kuku supermarket ambaye amewekwa katika majokofu miezi 6?...ama kweli ushamba mzigo...
 
siwezi kuliacha embe la jero tandale kisa embe la buku mbili shoprite

huu ni ukweli hutaki unaacha
 
Back
Top Bottom