Kupunguza bei ili kuua ushindani ni biashara kichaa

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,945
7,945
Nawasalimu katika jina la Muungano wa Tz

Karibuni katika uwanja wa mawazo ya kibepari na Beberu wenu J

Ipo hivi pale mtaani kwako kulikuwa na duka moja la mangi nae akapata pesa nyingi zilizofanya na wengine waingie kwa kasi katika biashara hio na ndani ya miaka mitatu kukawa na maduka 7 ya Mangi, Ushindani ukawa mkubwa na bei ya bidhaa zikaanza kuporomoka na kuwa nafuu kwenu walaji na mateso makubwa kwa wafanyabiashara mana bidhaa aliyopata faida buku sasa kwa sababu ya ushindani anapata faida mia mbili tena kwa shida.

WaTz wengi pale tunapoona kuna ushindani wa kibiashara huwa tunakimbilia kushusha bei ya bidhaa na matokeo yake faida inakuwa chini mana wewe ukipunguza na mwenzako atapunguza kwa hio mwishoni mnajikuta mnafanya biashara kichaa nan do mana biashara nyingi bongo huanza kwa speed mwisho zinakuwa za ovyo hazina faida watu wanafunga ovyo kwa kushindwa kumudu gharama za biashara husika kwani wao walishusha bei tu bila kufanya hesabu ya other expenses za biashara husika.

Mfano bar nyingi zinazodumu hapa mjini sio zile zinazouza bia na vinywaji kwa bei ya punguzo au ofa, ni zile ambazo utakuta wao wanauza vinywaji kwa 50% above bei elekezi na hii inawapa cushion ya challenge za biashara kama vile bad days na upotevu wa chupa pamoja na madeni ya watu, ila hiz Bar zinazojifanya kuuza bia kwa bei ya punguzo zikishaibiwa chupa, wateja 7 wakakopa + zikapita week mbili za bad business huwa haziwezi tena kuendelea kufanya kazi mana wao biashara yao inawapa faida ndogo licha ya mauzo kuwa makubwa.

Sasa basi nini kifanyike kuzuia hali hii?
#1. Chaguo namba moja ambayo mimi nashauri ni kwanza wafanya biashara ya aina moja eneo husika muungane mtengeneze umoja wenu na mchague viongozi wenu

#2. Kaeni chini kwa pamoja mpange bei elekezi kwa bidhaa zenu zinazotoka sana na muache bidhaa ambazo hazitoki sana kuwa huru kwa kila mtu kupanga bei anayotaka, mfano kipindi nasoma UDOM stationaries zilikuwa zinaenda kwa ushindani huria tu hivo zikapelekea bei ya kurudufu karatasi moja kuwa 25/- ambayo ukipiga hesabu wanakuwa wamepata hasara ila kuna watu walipenda tu kuona mauzo makubwa bila kuangalia faida au lah, nini kikafanyika? Hawa jamaa baadae wakatengeneza umoja wao na kupanga bei elekezi kwa baadhi ya huduma kama printing 100/-, kurudufu ikawa 50/- na hapo wengi wakaona faida, ko wakabaki wanashindana kwenye customer care na bei ya bidhaa ambazo hazitoki sana kama vile madaftar na peni.
Mfano wa pili ni hii mitandao ya simu nao licha ya kuwa sina uhakika ila hawa jamaa nao kuna kila dalili utaona wana genge lao baada ya ushindani mkali na kushusha bando utaona saizi hawa jamaa wanaenda sawa, yan Tigo wakipandisha bei na voda watapandisha tena kwenye range zile zile, na sasa unaona hata promo za matangazo ya mitandao ya simu zimepungua sana ( Hii ni faida ya umoja huu)

#3. Hii ni muhimu Zaidi, Viongozi wawe makini kufuatilia mwenendo wa utimizaji wa makubaliano yenu ya bei ili kuhakikisha hakuna wanaowazunguka na kuuza kwa bei ya chini

#4. Shindaneni kwenye issue nyingine kama vile customer care, location, lugha bora kwa mteja et all

#5. Mrudi kunishukuru baada ya kuanza kupiga faida kubwa kubwa

Natoa ushauri wa biashara kwa gharama nafuu sana na napatikana kupitia namba 0764 803 515
Bye bye mpaka wakati mwingine katika mawazo ya kibepari na Beberu wenu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Wazungu wako mbele kila kitu, walishakuja na Phoebus Cartel miaka ile.
Hapo umesema price setting, OPEC+ wana production control huwezi zalisha mapipa ya mafuta unavyojisikia ukiwa OPEC+ kila mmoja ana quota yake kuna nchi za mapipa milioni 2 kwa siku na za chini ya milioni. Kuna planned obsolescence mnaamua lifespan ya bidhaa ishushwe, hatuwezi kukuuzia ndala za kukaa miezi sita inabidi tuziweke nakshi zionekane bora ila zidumu miezi mitatu zife ununue tena.

Serikali mara nyingi hupambana na business conducts za hivyo
 
Ahsante sana kwa kuweka hii kitu, na hivyo ndo inavyotakiwa an, mkiendelea kufanya biashara kiholela hamtajenga wala kufanya kitu cha maendeleo

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Umoja kwa wafanyabiashara wa chini ni ngumu sana.Matajiri ndiyo huungana na kupanga biashara.Ila kina sie sasa.Tunavunjiana nazi na kutupiana kimavi kwenye biashara.
 
Umoja kwa wafanyabiashara wa chini ni ngumu sana.Matajiri ndiyo huungana na kupanga biashara.Ila kina sie sasa.Tunavunjiana nazi na kutupiana kimavi kwenye biashara.
Umesikia mkuu zipo zisizowezekana na zinazowezekana mkuu, mtaani kuna stationary 3 kwann msiungane, kuna mabucha matatu kwann msiungane, sema biashara kama za kina mama vitafunwa ni ngumu mana utakuta wapo 20 mtaa mmoja na wameshagombana kwenye issue nyingine, ila kama mnafanya biashara serious ya mtaji mkubwa unganeni tu muwanyonye wananchi

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Daa hiki ndiko nakipitia mim huku ktk biashara yangu ya duka la vyakula yaan wenzangu waliotukuta ktk biashara wameingia wanapunguza Bei kweli kweli kutoka kupata faida ya bidhaa moja ya jumla faida 1400 Hadi washindani kuweka kupata faida ya 200 hiyo yote kutaka wapate wateja wengi wauze Sana..kichwa kinauma mtaji wangu wa m60 naona unaelekea mlama
 
Umeandika point MUHIMU sana mkuu yaani vita vya panzi furaha ya kunguni
Yaani nyie mnashushiana bei afu wananchi wanafaidika ujinga gani huoo??
 
Daa hiki ndiko nakipitia mim huku ktk biashara yangu ya duka la vyakula yaan wenzangu waliotukuta ktk biashara wameingia wanapunguza Bei kweli kweli kutoka kupata faida ya bidhaa moja ya jumla faida 1400 Hadi washindani kuweka kupata faida ya 200 hiyo yote kutaka wapate wateja wengi wauze Sana..kichwa kinauma mtaji wangu wa m60 naona unaelekea mlama
Usipate shida !!!!!! , Boresha Huduma yako
Tafuta Udhaifu walio nao , pita humo humo .......
 
Back
Top Bottom