Ogopa nyumba za bei chee Chamazi-Mbagala

Ogopa nyumba za bei chee Chamazi-Mbagala

Ujenzi mbagala chamanzi ni nafuu sana. Mchanga upo Ndani ya kiwanja mbao zinaingia kimagendo viwanda vya cement vipo karibu mafundi bei nafuu Ramani ya nyumba unamuomba Jirani tu Julipi hata dala. Nyumba ya vyumba 3 Jojo, choo ndani sitting room na dianing hazidi 40mln.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimeiona hii nyumba Kwa jicho la tofauti..
Nataka kuiga huu ujenzi Ila ntaboresha kwenye kila pembe ntaweka mirunda mingi mithili ya nguzo kuipa uimara nyumba.
Pia udongo ntaotumia ntaufanya kuwa mnene ili kura ziwe nene kuhimili uzito wa paa.
Nikijachapia cement nje na ndani, lip ntaifanya soft sana.

Asante sana nimeshapata namna ya kujenda nyumba za shamba.

Actually nyumba ya Babu yangu iko hadi leo na ndani imekandikwa udongo, juu kuna bati nje na ndani kumefunikwa na cement.
Mkuu nunua tu tofali, sijajua point yao hapo wanakwepa nini otherwise na finishing materials viwe fake. Kujenga nyumba upande wa tofali hauna gharama kivile. Mziki ni kwenye finishing...
Ujenzi huu nategemea sehemu ambayo tofali ni ghali na si mbagala... labda kuna kitu kingine hapa sijakipata.
 
Licha ya gharama, kwangu napendelea funny house, yaani kimzaha mzaha nyumba ya muangalizi wa shamba imependeza mara nami nashawishika kuhamia shamba.

Mwanzoni nilikiwa na plani ya tofali za kuchoma, Ila sasa hivi hata tofali za kuchoma nimeziweka pembeni.

Ntajenga hii hii Ila kwenye paa ntamodifai kupunguza uzito kwenye nyumba.
 
Hizi nyumba zipo maeneo mengi tu ya Tanzania tena hizi ni bora zaid ya zkle za vijijini tuache kujidai tunasahau makwetu. Hivi nyumba kama hiyo ukiuziwa kwa ml 20 na kiwanja hasara ioo wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom