Ogopa nyumba za bei chee Chamazi-Mbagala

Ogopa nyumba za bei chee Chamazi-Mbagala

Mimi nimeiona hii nyumba Kwa jicho la tofauti..
Nataka kuiga huu ujenzi Ila ntaboresha kwenye kila pembe ntaweka mirunda mingi mithili ya nguzo kuipa uimara nyumba.
Pia udongo ntaotumia ntaufanya kuwa mnene ili kura ziwe nene kuhimili uzito wa paa.
Nikijachapia cement nje na ndani, lip ntaifanya soft sana.

Asante sana nimeshapata namna ya kujenda nyumba za shamba.

Actually nyumba ya Babu yangu iko hadi leo na ndani imekandikwa udongo, juu kuna bati nje na ndani kumefunikwa na cement.
 
Wakenya co watu wazur kabsa

god is good
 
Hizi nyumba zilikua zinajengwa sehem ya migodini wale waliokua wanataka kulipwa fidia...happy nje inapanda migomba ishakomaa....unaambiwa mzungu alishtuka akasubiri mvua zinyeshe ndo akaenda kagua..noma
 
Hapo alichokosea yeye ni hiyo miti iliyosimama, ilitakiwa kuwekwa miti yenye unene wa kutosha (approx. 12-15cm diameter) ili kuhimili uzito wa paa, pia udongo usiwe wa kuporomoka, humo mbavuni analaza bamboo, halafu udongo unajazwa wa kutosha uwe na phases kama 3 hivi.

NB: Iwe kwa matumizi yake binafsi asidalalie watu kwa bei ya tamaa.
 
Sasa mbona kama wanachokwepa ni matofali tu amabayo kwa nyumba ya kawaida hayazidi 3000 ambayo ni mil3-3.5 labda na kujenga nini mbona inakuwa kama hamna kitu.

Finish ya hiyo nyumba hapo ni balaa.
 
Sasa mbona kama wanachokwepa ni matofali tu amabayo kwa nyumba ya kawaida hayazidi 3000 ambayo ni mil3-3.5 labda na kujenga nini mbona inakuwa kama hamna kitu.

Finish ya hiyo nyumba hapo ni balaa.
Sio tofali TU mkuu.
Zege,Nondo,kokoto nyingi Sana zimeokolewa maana nyumba Haina beam.

Hata Garama za ufundi wa nyumba ya tofali Ni kubwa kulinganisha na tope.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wanaojua gharama za ujenzi wa nyumba,Finishing ya hii nyumba kwenye kuta zake Mpaka ije kwenye format hii tunayoiona,Ni garama Sana ukilinganisha Kama angejengea tofali.Kwanza Naona MTU ukijenga nyumba ya tofali YENYE ukubwa Kama hii ya miti tunayoiona,ya tofali ndo ndo RAHISI ZAIDI halafu inadumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah afadhali umenishutua nilitenga bajeti kabisa nilitaka kuzinununua kama hizo mia tano
 
Back
Top Bottom