Una maana katika hali ya kawaida Rejao huwa hana upeo wa kuyafahamu mambo mbalimbali?Kama mpaka Rejeo amenotice kuwa something is wrong then there must be a very serious problem there!!
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (*Alhamisi Machi 8, 2012) *imetoa
... uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi
nzima tangu jana (*Jumatano Machi 7, 2012).
Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari
Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia
Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama
walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.
Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja
na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine,
kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa
haraka.
Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya
kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha
Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo
huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka
kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.
Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:
Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji
R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari
Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:
i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari
pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi
2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama
kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa
Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na
kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9,
Mach 2012.
ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa
(Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa
kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo
huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;
iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama
cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za
Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa
haraka.
(mwisho)
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012
Siku hizi kazi za ofisi ya PM zimekuwa za kimahakama au ndio kuzuia PM asiachie madaraka,pinda jiuzulu umeiabisha.
something is wrong...
Tanzania yangu Ee Mungu!
Kwanini Unayaruhusu?
Yatusononeshe moyoni
Kwani umeyaruhusu?
Ikiwa tangazo hili halijaeditiwa basi madaktari wanayo haki ya kuishitaki mahakama pamoja na waziri mkuu kwa kuwahadaaa wananchi pamoja na madaktari. What a shame................. Kwanza haina hana nembo.
Jamani hii HUKUMU ama ZUIO lime serviwa kwa nani? Hakuna hukumu inatolewa hewani ama kwenye vyomboo vya habari. Hapa naona tunaambiwa wadaiwa ni MAT na Jumuiya ya Madaktari na mdai ni Serikali kwa hiyo uamuzi huu/amri hii ungepelekwa kwa Viongozi hivyo vyama ili kutekeleza amri ya mahakama. Na uamuzi huo ulitakiwa utolewe na mahakama ukiwa na seal ya mahakama ili uweze kuheshimiwa na siyo Ofisi ya Waziri Mkuu (Mdai) kutoa amri kwa Mdaiwa. Tungepata tamko lenyewe la mahakama tuone linasemaje. Kwa hiyo hapo juu hakuna tamko wa hukumu ya mahakama ni maneno tu yameandikwa na hiyo Ofisi (kama ni kweli).
Kama wanavyodai kwamba kikwete ni mzuri isipokuwa watendaji wake ndio wanamuangusha, basi katika muktadha huo huo tuseme waziri mkuu ni mtendaji mzuri isipokuwa wasaidizi wake ndio wanamuangusha?
Kwamba hiyo "hukumu" kutoka "mahakama kuu divisheni ya kazi ofisi ya waziri mkuu", waziri mkuu mwenyewe hakushirikishwa katika kuiandaa, wala hakuiona na wala hakushirikishwa katika kufikia uamuzi wa kuitengeneza na namna ya kuitoa kwa public pamoja na watuhumiwa madaktari!!??
This is simply a sign of "frustrated government".
...what is not wrong with this government!?...something is wrong...