Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,657
- 19,635
Sijui wewe unasoma mambo namna gani jamani. Unarudia lile lile nililokanusha. Unalinganisha ajira za sekta binafsi na serikali, wakati mimi nakwambia ni ulinganisho baina ya ajira za sekta binafsi na zile za kwenye makampuni yanayojenga hiyo miradi mikubwa.Mkuu huko sekta binafsi kulikuwa na malipo mazuri sana, kama wewe ni mtu wa serikali unaweza usilifahamu hili vizuri.
Kutofahamu huko kunatokana na ukwepaji kodi, kazi zingine muajiriwa anaambiwa wewe unalipwa consultation fee sio mshahara.
Mwingine anaambiwa wewe utalipwa commission asilimia kadhaa ya fedha uliyo iingizia kampuni. Unakuta hayo ni mamilioni mengi sana.
Hapo muajiri anakwepa gharama za pension na majukumu mengine ya muajiri.
Sekta binafsi mtu mwenye elimu ndogo tu alikuwa analipiwa hadi parking lot na mafuta ya gari kwa dola kadhaa kwa mwezi lakini hana mshahara rasmi analipwa commission au consultancy fee tu.
Hao watu walikuwa na wao wanaanzisha vikampuni vyao binafsi ndio wanatoa ajira kwa hao deiwaka wa mishahara midogo.
Wanafungua biashara ndogondogo na kuajiri hata wasio soma. 'Chain' ilikuwa inaenda hivyo.
Kitu cha muhimu sasa serikali inapata kodi zake na wenye kistahili pension wanatunziwa haki yao.
Kitu kingine kikubwa hizo ajira za sekta binafsi zilikuwa nyingi na toauti kuliko hizi za serikali za miradi mikubwa zinatoa ajira chache tena kwa kada flani chache hasa za ujenzi. Hizi za sasa hazitoi haueni kwa ajira zisizo rasmi kama zile nyingi za sekta binafsi.
Nafikiri kama kusingekuwa na udanganyifu hapo zamani tungeweza kupata 'figure' kamili za jumla pesa kiasi gani zilikuwa zinalipwa waajiriwa sekta binafsi na sasa jumla kiasi gani wanalipwa waajiriwa wa ktk miradi mikubwa ya maendeleo. Hii ingetupatia picha halisi, japo shida na ukosefu wa pesa mitaani ni picha tosha kuonesha pesa zinazo ingia mitaani kupitia ajira za kwenye miradi mikubwa ni chache kulinganisha na za ajira za sekta binafsi za kipindi cha miaka 3 iliyopita kurudi nyuma..
Halafu unaposema kuwa hiyo miradi mikubwa zinatoa ajira chache, unakuwa unapingana na takwimu ambazo ziko wazi kabisa kwenye hiyo chati ya NBS!
Kuelewa maandiko ni tabu??