NBS Report “Tanzania in Figure 2018”
Agosti 10, 2019
Kwa kifupi.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Tanzania in Figure 2018” iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Juni 2019, inaonyesha kuwa ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018.
Hiyo ni sawa na anguko la asimilia 42.6 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika sekta hiyo inayotegemewa kuajiri watu wengi nchini.
Hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na kupungua kwa shughuli za biashara katika kipindi ambazo zilikuwa zinakabiliwa mazingira yasiyoridhisha kwa wawekezaji ikiwemo urasimu katika upatikanaji wa vibali na utitiri wa kodi na tozo.
Hata hivyo, katika bajeti ya mwaka 2019/2020, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali imekusudia kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa kodi na tozo zinazowaumiza wawekezaji.
Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali nazo zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.
Wakati ajira rasmi serikalini na sekta binafsi zikipungua, ajira zilizotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara, majengo na reli ziliongezeka na kuifanya sekta hiyo kuongoza kwa kuajiri watu wengi zaidi mwaka mmoja uliopita.
Licha ya kuongezeka kwa mahitaji ya ajira Tanzania, kiwango cha watu wasio na ajira kimeendelea kupungua katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mathalani, kiwango hicho cha ukosefu wa ajira nchini kimepungua kutoka asilimia 10.3 mwaka 2014 hadi asilimia 9.7 mwaka 2018.
SOURCE: Nukta
My Take: Namba huwa hazidanganyi.
======
UPDATES: 14 AUG 2019
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Jamii Forum yenye kichwa cha habari “NBS yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, Serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja."
Habari hii imepotosha kuhusu kupungua kwa ajira Serikalini na hivyo jamii inaombwa kuipuuza kwa kuwa haina ukweli wowote.
Agosti 10, 2019
Kwa kifupi.
- Ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018.
- Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Tanzania in Figure 2018” iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Juni 2019, inaonyesha kuwa ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018.
Hiyo ni sawa na anguko la asimilia 42.6 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika sekta hiyo inayotegemewa kuajiri watu wengi nchini.
Hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na kupungua kwa shughuli za biashara katika kipindi ambazo zilikuwa zinakabiliwa mazingira yasiyoridhisha kwa wawekezaji ikiwemo urasimu katika upatikanaji wa vibali na utitiri wa kodi na tozo.
Hata hivyo, katika bajeti ya mwaka 2019/2020, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali imekusudia kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa kodi na tozo zinazowaumiza wawekezaji.
Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali nazo zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.
Wakati ajira rasmi serikalini na sekta binafsi zikipungua, ajira zilizotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara, majengo na reli ziliongezeka na kuifanya sekta hiyo kuongoza kwa kuajiri watu wengi zaidi mwaka mmoja uliopita.
Licha ya kuongezeka kwa mahitaji ya ajira Tanzania, kiwango cha watu wasio na ajira kimeendelea kupungua katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mathalani, kiwango hicho cha ukosefu wa ajira nchini kimepungua kutoka asilimia 10.3 mwaka 2014 hadi asilimia 9.7 mwaka 2018.
SOURCE: Nukta
My Take: Namba huwa hazidanganyi.
======
UPDATES: 14 AUG 2019
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Jamii Forum yenye kichwa cha habari “NBS yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, Serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja."
Habari hii imepotosha kuhusu kupungua kwa ajira Serikalini na hivyo jamii inaombwa kuipuuza kwa kuwa haina ukweli wowote.
Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS) yakanusha kupungua kwa ajira Serikalini
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII YA KUPUNGUA KWA AJIRA SERIKALINI Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Jamii Forum yenye kichwa cha habari “NBS yakiri ajira sekta binafsi...
www.jamiiforums.com