Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja

Mkuu huko sekta binafsi kulikuwa na malipo mazuri sana, kama wewe ni mtu wa serikali unaweza usilifahamu hili vizuri.
Kutofahamu huko kunatokana na ukwepaji kodi, kazi zingine muajiriwa anaambiwa wewe unalipwa consultation fee sio mshahara.
Mwingine anaambiwa wewe utalipwa commission asilimia kadhaa ya fedha uliyo iingizia kampuni. Unakuta hayo ni mamilioni mengi sana.
Hapo muajiri anakwepa gharama za pension na majukumu mengine ya muajiri.
Sekta binafsi mtu mwenye elimu ndogo tu alikuwa analipiwa hadi parking lot na mafuta ya gari kwa dola kadhaa kwa mwezi lakini hana mshahara rasmi analipwa commission au consultancy fee tu.
Hao watu walikuwa na wao wanaanzisha vikampuni vyao binafsi ndio wanatoa ajira kwa hao deiwaka wa mishahara midogo.
Wanafungua biashara ndogondogo na kuajiri hata wasio soma. 'Chain' ilikuwa inaenda hivyo.
Kitu cha muhimu sasa serikali inapata kodi zake na wenye kistahili pension wanatunziwa haki yao.
Kitu kingine kikubwa hizo ajira za sekta binafsi zilikuwa nyingi na toauti kuliko hizi za serikali za miradi mikubwa zinatoa ajira chache tena kwa kada flani chache hasa za ujenzi. Hizi za sasa hazitoi haueni kwa ajira zisizo rasmi kama zile nyingi za sekta binafsi.
Nafikiri kama kusingekuwa na udanganyifu hapo zamani tungeweza kupata 'figure' kamili za jumla pesa kiasi gani zilikuwa zinalipwa waajiriwa sekta binafsi na sasa jumla kiasi gani wanalipwa waajiriwa wa ktk miradi mikubwa ya maendeleo. Hii ingetupatia picha halisi, japo shida na ukosefu wa pesa mitaani ni picha tosha kuonesha pesa zinazo ingia mitaani kupitia ajira za kwenye miradi mikubwa ni chache kulinganisha na za ajira za sekta binafsi za kipindi cha miaka 3 iliyopita kurudi nyuma..
Sijui wewe unasoma mambo namna gani jamani. Unarudia lile lile nililokanusha. Unalinganisha ajira za sekta binafsi na serikali, wakati mimi nakwambia ni ulinganisho baina ya ajira za sekta binafsi na zile za kwenye makampuni yanayojenga hiyo miradi mikubwa.

Halafu unaposema kuwa hiyo miradi mikubwa zinatoa ajira chache, unakuwa unapingana na takwimu ambazo ziko wazi kabisa kwenye hiyo chati ya NBS!

Kuelewa maandiko ni tabu??
 
Sio kwamba sijakuelewa ila wewe hujaelewa au hujaona mantiki ktk hoja zangu.
Kuna sehemu hapo nimekuambia udanganyifu ulikuwa mkubwa sana miaka iliyopita.
Idadi unayo iona sasa ya ajira binafsi na ajira zitokanazo na miradi mikubwa ya maendeleo ya serikali ndio takwimu ambazo zina uhalisia kutokana na ukali na umakini wa serikali ya sasa.
Na hizo takwimu za miaka ilyopita kama 2013/14 hazina uhalisia sababu waliajiriwa wengi na serikali haikuwa na taarifa sahihi.
Hiyo ilisababishwa na waajiri na wakati mwingine waajiriwa kuomba wasiwekwe kwenye mfumo rasmi wa pension na ulipaji kodi ya PAYE.
Nikakupa mifano ya watu kulipwa commissions na consultancy fee.
Nina ushahidi wa watu wengi sana kuajiriwa sekta binafsi huku walikuwa hawalipi kodi na makato ya pension funds. Hawakuingizwa ktk kumbukumbu za serikali hawakulipa mikopo ya elimu ya juu. Ukiachana na hao wa wasomi elimu ya juu wengine wengi wa elimu ya stashahada hadi wasiosoma kabisa lakini walistahili kuingizwa ktk rekodi za serikali na kulipa kodi hawakuingizwa taarifa ktk mifumo ya serikali.
Hiyo idadi unayo iona hapo ktk chati ya miaka ya 2015 kurudi nyuma ni robo ya watu halisi walio ajiriwa miradi mikubwa sekta binafsi na miradi mikubwa ya maendeleo inayotoa pesa serikalini.
Shida ni wewe kutonielewa sio mimi kuto kukuelewa.
Pia hao sekta binafsi wengi walikuwa wanaingiza pesa nyingi sana tofauti na iliyokuwa inajulikana ktk rekodi za serikali.
Ushahidi wa haya niyasemayo ni ile taarifa iliyopo ktk flash disk ya Mh. Raisi aliyokuja nayo kwenye kikao chake na wafanyabiashara wakubwa toka kila wilaya. Benki ipo ripoti tofauti ya hesabu za ukaguzi na ya TRA.

Ushahidi wa pili ni ile taarifa ya HESLB ya wadaiwa sugu iliyotoka karibuni. Wadaiwa waliofikishwa mahakamani ni chini ya 8 wakati hali halisi kwenye makabrasha yao wapo wengi. Hawa 8 ni wale tu waliokuja kunaswa baada ya kuingia ktk mifumo ya serikali sasa baada ya ajira mpya au waajiri kuwaingiza sasa. Kiuhalisia wapo wengi huku mitaani waliokuwa wanalipwa mamilioni na hawapo ktk walipaji wa mikopo au kodi za serikali wala hawakuwepo ktk kumbukumbu za wizara ya kazi na ajira.
Wengi walioweza wameenda nchi za jirani kama DRC, n.k.
MY POINT IS 'HIZO TAKWIMU ZA ZAMANI SIO HALISI' sababu NBS vyanzo vyao vya takwimu ni toka ktk mifumo rasmi ya serikali ambayo haikupewa taarifa zote na halisi toka sekta binafsi.
Hiyo chati nusu ina tawimu halisi na nusu nyingine sio kamili ni zenye mapungufu. Serkali ilikuwa imelala.
Kwa kutumia chati hiyo kutafsiri kilichomo ni kweli upo sahihi yote usemayo lakini huku mtaani kuna takwimu halisi zisizo ongopa ktk maisha halisi ya wengi.
 
Sio kwamba sijakuelewa ila wewe hujaelewa au hujaona mantiki ktk hoja zangu.

Kuna sehemu hapo nimekuambia udanganyifu ulikuwa mkubwa sana miaka iliyopita.

Idadi unayo iona sasa ya ajira binafsi na ajira zitokanazo na miradi mikubwa ya maendeleo ya serikali ndio takwimu ambazo zina uhalisia kutokava na ukali na umakini wa serikali ya sasa.

Na hizo takwimu za miaka ilyopita kama 2013/14 hazina uhalisia sababu walijiriwa wengi na serikali haikuwa na taarifa.

Hiyo ilisababishwa na waajiri na wakati mwingine waajiriwa kuomba wasiwekwe kwenye mfumo rasmi wa pension na ulipaji kodi ya PAYE.

Nikakupa mifano ya watu kulipwa commissions na consultancy fee.

Nina ushahidi wa watu wengi sana kuajiriwa sekta binafsi walikuwa halipi kodi, na makato ya pension fund. Hawakuingizwa ktk kumbukumbu za serikali hawakulipa mikopo ya elimu ya juu na wwngine wengi wa elimu ya stashahada hadi wasiosoma lakini walistahili kuingizwa ktk rekodi za serikali na kulipa kodi.

Hiyo idadi unayo iona ya miaka ya 2015 kurudi jyuma ni robo ya watu halisi walio ajiriwa miradi mikubwa na hasa wa sekta binafsi nyingine.

Shida ni wewe kutonielewa sio mimi kuto kukuelewa.

Pia hao sekta binafsi wengi walikuwa wanaiingiza pesa nyingi sana tofauti na iliyokuwa inajulikana ktk rekidi za serikali.

Ushahidi wa haya niyasemayo ni ile taarifa iliyopo ktk flash disk ya Mh. Raisi aliyokuja nato kwenye kikao chake na wafanyabiashara wakubwa kila wilaya. Benki ipo ripoti todauti ya hesabu za ukaguzi todauti na ya TRA.

Ushahidi wa pili ni ile taarifa ya HESLB ya wadaiwa sugu iliyotoka karibuni. Wadaiwa waliofikishwa mahakamani ni chini ya 8 wakati hali halisi kwenye makabrasha yao wapo wengi. Hawa 8 ni wale tu waliokuja kunaswa baada ya kuingia ktk mifumo ya serikali sasa baada ya ajira mpya au waajuri kuwaingiza sasa. Kiuhalisia wapo wengi huku mitaani waliokuwa wanalipwa mamilioni na hatupo ktk walipaji wa mikopo au kodi za serikali wala hatukuwepo ktk kumbukumbu za wizara ya kazi na ajira.
Wengi walioweza wameenda nchi za jirani kama DRC, n.k.

MY POINT IS 'HIZO TAKWIMU ZA ZAMANI SIO HALISI' sababu NBS vyanzo vyao vya takwimu ni toka ktk mifumo rasmi ya serikali ambayo haikupewa taarifa zote na halisi toka sekta binafsi.

Hiyo chati nusu ina tawimu halisi na nusu nyingine sio kamili ni zenye mapungufu. Serkali ilikuwa imelala.

Kwa kutumia chati hiyo kutafsiri kilichomo ni kweli upo sahihi yote usemayo lakini huku mtaani kuna takwimu halisi zisizo ongopa ktk maisha halisi ya wengi.

Sawa; nimekuelewa na samahani! Ila sasa uchumi huo wa kudanganya namba ndio tunaoupinga sasa
 
Sawa; nimekuelewa na samahani! Ila sasa uchumi huo wa kudanganya namba ndio tunaoupinga sasa
Ni kweli kabisa.
Huo uchumi mbaya na mbovu sana.
Tungewndelea kuwa nchi masikini sana na tofauti ya masikini na matajiri ingekuwa kubwa sana.

Huduma za afya, maji safi na elimu kwa masikini ilikuwa ni kama anasa sio mahitaji ya lazima.
 
Mapimbi kabisa....yanachungulia halafu hayo yanasepa. Hakunaga uchumi unakua uku una shed jobs like hell. Shedding jobs means trouble. Majitu majinga sana, sifia sifia upuuzi tu.Tumepoteza exports,biashara zimefungwa,wawekezaji wamekimbia na donors wamekata misaada bado watu wanategemea miracles...subirini videos za mtu amevaa magwanda ili m comment.
Kuchumia tumbo yataka moyo maana lazima wajitoe ufahamu then wauvae unafiki na ubinafsi.
Tuna safari ndefu sana tuendako hasa unapokuwa na watu wa namna hii.
Wanachosahau ni kuwa "There is no permanent situation"
 
Unatakiwa usome hiyo report vizuri. Siamini kama ajira zimepungua kwa maana kutoka mfano 200 kuja 100 bali ongezeko la ajira halikuwa kama mwaka jana; mfano mwaka jana ajira ziliongezeka kwa 300 na mwaka huu zimeongezeka kwa 50. Someni takwimu kwa furaha msisome mkiwa na mawazo ya kwamba ajira zimeshuka
Namba hazidanganyi you have to call aspade a spade, eti soma takwimu kwa furaha mbona unaleta siasa kwenye namba?
 
Kwa tafsiri rahisi ni kuwa kwa sasa Serikali yetu ni tajiri kuliko watu wake ndio maana inamudu kuijenga nchi kama tunavyoona au?
Ni mikopo, na tutalipa mpaka vitukuu vyetu waliopo Serikalini wanakopa na pia wanachukua 10% kwenye miradi hiyo tutakao umia ni sisi ambao hatupo Serikalini wenyewe wanafaidika na 10% ya kila mradi au ununuzi wa ndege
 
NBS Report “Tanzania in Figure 2018”
Agosti 10, 2019

Kwa kifupi.
  • Ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018.
  • Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.
Dar es Salaam. Ripoti mpya ya takwimu za Tanzania imeeleza kuwa ajira zinazotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kwa asilimia 42.6 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, jambo linalotoa changamoto kwa vijana na wadau wa maendeleo kubuni njia mbadala za kuondoa tatizo la ajira nchini.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Tanzania in Figure 2018” iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Juni 2019, inaonyesha kuwa ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018.

View attachment 1181109

Hiyo ni sawa na anguko la asimilia 42.6 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika sekta hiyo inayotegemewa kuajiri watu wengi nchini.

Hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na kupungua kwa shughuli za biashara katika kipindi ambazo zilikuwa zinakabiliwa mazingira yasiyoridhisha kwa wawekezaji ikiwemo urasimu katika upatikanaji wa vibali na utitiri wa kodi na tozo.

Hata hivyo, katika bajeti ya mwaka 2019/2020, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali imekusudia kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa kodi na tozo zinazowaumiza wawekezaji.

Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali nazo zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

View attachment 1179274

Wakati ajira rasmi serikalini na sekta binafsi zikipungua, ajira zilizotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara, majengo na reli ziliongezeka na kuifanya sekta hiyo kuongoza kwa kuajiri watu wengi zaidi mwaka mmoja uliopita.

Licha ya kuongezeka kwa mahitaji ya ajira Tanzania, kiwango cha watu wasio na ajira kimeendelea kupungua katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mathalani, kiwango hicho cha ukosefu wa ajira nchini kimepungua kutoka asilimia 10.3 mwaka 2014 hadi asilimia 9.7 mwaka 2018.

SOURCE: Nukta

My Take: Namba huwa hazidanganyi.

======

UPDATES: 14 AUG 2019

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Jamii Forum yenye kichwa cha habari “NBS yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, Serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja."

Habari hii imepotosha kuhusu kupungua kwa ajira Serikalini na hivyo jamii inaombwa kuipuuza kwa kuwa haina ukweli wowote.

IKulu wamezifunga NGOS 148.

Hawa jamaa ndio real ya definition ya mwenye shibe
 
Uchumi unakua kwa kasi sana!

Awamu bora kabisa ya Tano!

Buuaaaaaah
 
Viongozi wetu wanapopinga takwimu zinazoonesha kushuka kwa uchumi ni kutokana na imani yao kwamba kwavile wanatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu, basi uchumi ni lazima upande.

Ni kweli kwamba miundombinu ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi, lakini wanasahau kwamba athari chanya katika uchumi haiwezi kuonekana sasa ambapo miradi hiyo iko katika hatua za utekelezaji.

Serikali inapasa kuzingatia kuwa inachotekeleza sass ni uwekezaji tu. Haiwezekani kupata mavuno ya uwekezaji wakati uwekezaji bado hajakamilika (lag phase). Matunda ya uwekezaji huu yanaweza kupatikana hapo baadae (exponential phase).

Kwahiyo wanapoambiwa uchumi umeshuka au ajira zimepungua wasikatae kwasababu mitaji yote ya serikali imeelekezwa katika eneo moja tu la ujenzi na sio uzalishaji.

Shughuli za uzalishaji pekee ndizo zinazopelekea ukuaji wa uchumi na ajira. Mathalanie, serikali imewekeza nini katika sekta za uzalishaji kama
1. kilimo, uvuvi na mifugo,
2. Madini na gesi asilia,
3. Utalii,
4. Viwanda na biashara?

ingekuwa vizuri endapo serikali ingekuwa ina-balance uwekezaji katika miundombinu na shughuli za uzalishaji.
Huu ni ushauri wa mwaka. Big up comrade
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom