MUTTAZ
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 296
- 237
Wewe bila shaka hujui kusoma reports na yumkini Hata uelewa wako nomdogo sana! Yaani kama kazi ya CAG huioni na umuhimu wa CAG huuoni Hata kuuhisi Basi wewe nimiongoni mwa walaji wa nchi hii! Nawewe sidhani kama nimwanaccm mwenzangu Bali nimamluki! CAG na ofisi yake ndo imeanzisha dhana ya uwajibikaji hapa nchini wewe unabeza kweli kwakweli nabii sirahisi akubaliwe kwao!Nimeanzisha uzi huu ili kila aliye na utaalamu, atueleze ni jinsi gani ofisi ya CAG inavyofanyakazi zake.
Bodi ya mikopo kulikuwa na madudu, vyuoni madudu, wizarani madudu.
Mambo ya ndani madudu: Lugumi, Vitambulisho, Uniform, ....
Huko wizara ya Kilimo: tusubiri skandali za vocha na ruzuku
Iliyokuwa wizara ya Sayansi: TCRA madudu, sijui COSTECH kukoje? Na vyuoni kwao kule Mandela madudu.
Waiziri mkuu na tamisemi zao madudu na sukari yao madudu tupu!
Wakati haya yanatokea, CAG alishajiwekea kitu kinaitwa value for money. Kwa mfano wa wanafunzi hewa, nilitegemea awakague vyuoni na bodi ya mikopo kuona kama matumizi yao yanaendana na idadi ya wanafunzi. Value for money.
Majengo yanayojengwa na mifuko ya jamii na daraja mashuhuri la Kigamboni, nilitegemea aone madudu yao pia.
Najiuliza ofisi hiyo ina mapungufu gani ya kitaalamu kiasi kwamba sasa ndo mambo yanafumuka nje ya ripoti yao?
Hivi kwa takribani miaka saba hadi kumi ilopita ofisi ya CAG utailinganisha na ofisi ya TAKUKURU Kweli? Mzee wa watu Utouh katuonyesha dhana halisi ya uwajibikaji na matumizi ya rasilimali za nchi Leo hii unajitokeza mbulula una diliki Hata Kutoa povu kuikashfu ofisi ya CAG bila shaka utakuwa umekurupushwa usingizini au hapa jamii forum mtu anakuwa expert kwa kuanzisha thread yake haijalishi niyakitaalamu au ya kinafiki na kishirikina!
Bila uwepo wa cag kweli tungekuwa huruma na rasilimali za nchi zilivyokuwa zinaliwa nakutafunwa, bila CAG tungejua pale TPA Mafuta yanapita bila kupimwa?, bila CAG tungejua mambo ya EPA, ESCROW, Madudu ya TANESCO, Wafanyakazi hewa, Mashirika ya Umma yalivyokuwa yanaliwa, UDA tungeijua niyanani, PRIDE tungejua niyanani? I wish ningekuwa Mhasibu sio Siri namm ningeenda kusaidiana na CAG kuimulika nchi yetu ili iwe safi na nyeupe!