Ofisi ya CAG ilikuwa wapi ktk huu ufisadi nchi nzima?

Ofisi ya CAG ilikuwa wapi ktk huu ufisadi nchi nzima?

shaurimbaya kuna kitu kakisema. CAG kiukweli na uhalisia hana uwezo wa kuaudit idara na taasisi ama wizara na bodi zote za serikali kutokana na less resources (staff, fund, time) coz auditor kutoa reliable opinion anahitaji time frame ya kumtosha, staff tena skilled and competent staff, fund ya kutosha na kufuata code of ethics zote. Kibaya most of them ofisi ya CAG haina kwa sass mwezi huu wa 10 kuna auditing firm zishapewa kazi kutokana na competence yako kwenda kuaudit baadhi ya taasisi,idara, bodi na baadhi ya wizara na halimashauri. MUTTAZ hope umelielewa hili.
 
Labda na mimi niongezee kwa uelewa wangu mdogo. Kila audit inakuwa na objective yake. CAG akikagua mara nyingi objective yake ni to enable the auditor to report that the financial statements audited shows true and fair view. Vilevile ikumbukwe auditor anakaa muda mfupi sana kama mwezi moja kwenye hiyo entity. Auditor anategemea sana internal controls ambazo zimewekwa na organisation yenyewe. Management inapoamua kuabuse hizo controws auditor anaweza asigundue. Na mara nyingi auditor wanafanya sampling. Kazi ya auditor inaishia kwa kutoa report. CAG ameshatoa report nyingi ambazo hazijafanyiwa kazi.
 
Bandari ilikuwa maduduuu, mafunza, majipu...

C.A.G nae jipu kabisa... Mungu mkubwa Mh. Rais Magufuli kaokoa Tanzania na madudu yote hayo.. na isitoshe CAG alilalamika sana eti kupunguziwa hela ktk budget za auditing, damn, wakati hamna kitu bure kabisa, CAG nae ni inbuilt jipu... jipu la ndani kwa ndani tu...!! JPM ndio kila kitu..!! Hatutaki mchezo mchezo tena... Hapa Kazi tu... na bado
 
kaka acha ubishi.. kuna normal kama cag ambazo kihasibu wanaita internal audits.. cag ndio mmiliki wa internal audits zote za serikal na taasisi zake.. so ndio anaweza aka outsource kampun yoyote ifanye kwa niaba yake..

halafu pia kuna scandal audits na external audits.. ambazo kama epa.. cag anatangaza tenda kwa niaba ya rais.. kampuni zinaomba kwa kushindanishwa.. mchakato wa tenda...

atakeshinda tenda anakuja kufanya hiyo kazi insepedent.. CAG hausiki hata kidogo anakaa pembeni tu.. na report ikitoka anapewa rais.

so usilete uongo kwenye epa kulikuwa na staff yeyote wa CAG au CAG alikuwepo na timu yake akiwasaidia wazungu hao walioshinda tenda.. huo ni uongo
Kiongozi internal audit section haipo chini ya cag bali ipo chini ya internal auditor general ambaye anapatikana pale Hazina wizara ya fedha! Kiufupi internal auditors na wahasibu wapo chini ya wizara ya fedha na wahasibu wapo chini ya acgen ie accountant general na usemavyo kuwa internal audit anaoutsosi cag inaonyesha nikwa jinsi gani unadandia vituz usivyo na upeo na uelewa navyo!
 
Kazi ya CAG ni kuriport sio kufunga na kushtaki watu,au kuja kwenye public through media kusema huyu kapiga pesa
angalia riport zote ufisadi umeanikwa tatizo PAC na LAAC ndizo kamati bungeni zenye mamlaka ya kuchokonoa audited report na kuipa muongozo serikali angalia Sasa waliokwenye hizo kamati ni kichekesho kingereza hawajui, kiswahili Ndio tatizo wavivu kusoma. Sasa kabla ya kulalamika tuchukue muda kupitia audited report na tuelewe nani wenye kuanzisha mchakato Wa kushughulikia frauds zilizo ndani ya report. Pasipo bunge imara CAG hana meno na anafanya kazi bure
 
Majukumu ya CAG yameainishwa na katiba.

==>Jukumu la kwanza- Kwa mujibu wa Ibara 143(1), CAG anawajibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka mfuko mkuu wa Hazina ya Serikali baada ya kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya matumizi ya fedha za mfuko wa hazina kwa mujibu wa ibara ya 136 ya Katiba. Jukumu hili lipo nje ya mjadala huu.

==> Jukumu la pili - Kufanya ukaguzi na kutoa ripoti
Ibara 143 (2) (c) inamtaka CAG kukagua hesabu za Serikali Kuu, Mamlaka za Mitaa, Mahakama, na Bunge na kutoa taarifa zake. Ibara 143(2) inamtaka CAG angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabu zinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hesabu za Mahakama zote za Jamhuri ya Muungano na hesabu zinazosimamiwa na Katibu wa Bunge. Ukaguzi huu unahitwa ukaguzi wa fedha na niwalazima (statutory financial audits) na wanaoufanya ni wakaguzi wa mahesabu (Financial auditors). Kwamaoni yangu hapa ndio msingi wa hoja ya mada hii.

Hivyo ni vizuri kufaham kuwa kwenye ukaguzi wa kawaida (financial audit) lengo la CAG/makguzi ni kutoa maoni kuhusu mamba (hali) ya fedha kama inasema ukweli au la. kawaida ufanyika kwa sampli na lengo lake siyo kugundua wizi ingawa kitaalam mkaguzi wa fedha anahitajika kuwa mwenye taadhali kubwa kugundua kama kuna wizi unaoweza kuathiri vitabu vya mahesabu.

Hivyo kuna tofauti kubwa kati ya ukaguzi huu na ule wa uchunguzi. Ukaguzi huu wa pili ni lazima unajikita kwenye kubaini kama kuna wizi, chanzo/vyazo na wahusikia wakuu na ufanywa na wakaguzi wa kiuchuzi (forensic auditors) tofauti na ule wa fedha unaofanywa na wakaguzi wa mahesabu (financial auditors). Hivyo kazu zote maalam kama ulizizitaja ufanywa na wachunguzi lengo likiwa kukusanya ushahidi husio na shaka kwa ajili ya matumi ya kimahakama ikibidi.

==> Hupo mjadala wa nini hasa jukumu la mkaguzi (CAG) katika kubaini wizi. Katika ukaguzi wa kawaida anatarajiwa ajipange (plan) ili kama kuna wizi aweze kubaini lakini siyo jukumu lake mahususi. Kimsingi jukumu hili ni la menejimenti ingawa mkaguzi wa hesabu akiona anatakiwa kuliweka kwenye taarifa yake (to report). Naomba fuatilia "link" kwa faida yako.http://ir.stthomas.edu/cgi/viewcontent.cgi?article=1056&context=ocbacctpub [Auditors' responsibility for fraud detection- there are quite number of other literatures on this, please read].

==
> Ninavyofaham mimi masuala yote yanayojitokeza kwenye kaguzi za hesabu na maalum (za uchungiz) ujumuishwa kwenye taarifa ya CAG ya mwaka -pitia nao.go.tz. Masuala yanayowekwa kwenye taarifa hizi inatarajiwa menejimenti za taasisi husika kufuatilia kwa kina na kuchukua hatua.

==> Suala la je, kwanini hakubaini? suala hili linategemea "context" , lakini kwa maoni yangu ningejiuliza kama ukaguzi hakufanyika kabisa hali ingekuwaje?

Naomba kutoa mchango wangu kwenye suala hili. I stand to be corrected. Apologies in case I failed to hit the bull.

N.B. Soma sheria ya ukaguzi ya mwaka 2008 na miongozo ya kiukaguzi kuhusu suala hili la jukumu la mkuguzi wa mahesabu kwenye masuala ya wizi.
 
Wewe bila shaka hujui kusoma reports na yumkini Hata uelewa wako nomdogo sana! Yaani kama kazi ya CAG huioni na umuhimu wa CAG huuoni Hata kuuhisi Basi wewe nimiongoni mwa walaji wa nchi hii! Nawewe sidhani kama nimwanaccm mwenzangu Bali nimamluki! CAG na ofisi yake ndo imeanzisha dhana ya uwajibikaji hapa nchini wewe unabeza kweli kwakweli nabii sirahisi akubaliwe kwao!

Hivi kwa takribani miaka saba hadi kumi ilopita ofisi ya CAG utailinganisha na ofisi ya TAKUKURU Kweli? Mzee wa watu Utouh katuonyesha dhana halisi ya uwajibikaji na matumizi ya rasilimali za nchi Leo hii unajitokeza mbulula una diliki Hata Kutoa povu kuikashfu ofisi ya CAG bila shaka utakuwa umekurupushwa usingizini au hapa jamii forum mtu anakuwa expert kwa kuanzisha thread yake haijalishi niyakitaalamu au ya kinafiki na kishirikina!

Bila uwepo wa cag kweli tungekuwa huruma na rasilimali za nchi zilivyokuwa zinaliwa nakutafunwa, bila CAG tungejua pale TPA Mafuta yanapita bila kupimwa?, bila CAG tungejua mambo ya EPA, ESCROW, Madudu ya TANESCO, Wafanyakazi hewa, Mashirika ya Umma yalivyokuwa yanaliwa, UDA tungeijua niyanani, PRIDE tungejua niyanani? I wish ningekuwa Mhasibu sio Siri namm ningeenda kusaidiana na CAG kuimulika nchi yetu ili iwe safi na nyeupe!
Mapungufu kila mtu anayo ila usiangalie mabaya tu Bali weigh out kati ya mabaya yake na mazuri yake na ukifanya hivyo utaona mazuri nilukuki ukilinganisha na mabaya! Nabaada ya kuyaona hayo mabaya fuatilia uone ninani Mwenye kuyakumbatia je nicag au serikali!?
Nimeangalia msg hizi mbili toka kwako, nikaishia kusikitika tu! Kama uko ofisi ya CAG vile! Lakini uandikaji na upangaji wa hoja ni wa chini kiasi kwamba, kama unatafuta kazi nitakusaidia uwe park boy. Yaonekana hujawahi kuutesa ubongo wako kutafuta ufumbuzi wa matatizo magumu.

Hapa hatuongelei Utoh, wewe unasema muacheni mzee wa watu, watu gani ambao huyo Utoh ni mzee wao?

Hebu tuelezeni Ofisi zenu zimejengwa kwa shilingi ngapi? Kuna mtu kaonyesha nanyi munanunua rim moja ya karatasi kwa dola 200! Hatuhitaji taarifa za chini kiasi hicho unachoeleza hapa. Huna haja ya kuandika eti kuna pesa kadhaa zimeibiwa so what? Sema Fulani ktk ofisi za bunge amesaini nyaraka za malipo ya matibabu ya mbunge hewa kutibiwa India. Ukiona wizi wa wazi kiasi hicho lete forensic audit report.

CAG siyo mtu wa kutishia nyau ili wahusika wapandishe dau la kumpoza. Mwishowe unaleta wish za kuwa mhasibu ili umusaidie CAG, unakwenda kumsaidia nini wakati unasema kazi anaiweza? Rubbish!
 
Mapungufu kila mtu anayo ila usiangalie mabaya tu Bali weigh out kati ya mabaya yake na mazuri yake na ukifanya hivyo utaona mazuri nilukuki ukilinganisha na mabaya! Nabaada ya kuyaona hayo mabaya fuatilia uone ninani Mwenye kuyakumbatia je nicag au serikali!?
Wewe sasa unajisemea lolote ili tu kutetea CAG. Lini tukaanza ku-balance mabaya na mazuri kutafuta mafanikio ya utendaji wa kiofisi? Kwa kuwa una mahaba naye ndo unaleta vigezo vipya?
Tunaulizana juu ya umuhimu wa ofisi ile ktk hali ya sasa ambayo inaonyesha uozo ukitolewa na ofisi nyingine nje ya CAG! Ofisi inafanya nini? Jiulize mwaka huu itafanya nini maana kila kitu sasa hata kamati ya bunge inaonyesha makubwa kuliko hata huyo CAG!
 
Mm napingana na nyie wote hapo huu bilashaka labda kuna issue mmeelekezwa kuitoa lakini ukiangalia haya yote uyaonayo watumishi hewa cag alisharipoti kitambo sana tena kama sikosei alikuwa utouh ila serikali haikuchukua hatua stahiki kwa muda muafaka, issue za loan board utouh alishaziripot, halmashauri nyingi zimejirekebisha kutokana na report za ukaguzi za cag huko nyuma hali ilikuwa mbaya sana, kumbukeni cag aliwahikagua soko la Kariakoo na ubungo terminal tena ulikuwa niukaguzi maalum lakini hadi hii Leo report yake haikutolewa serikali! Kwa ufupi ninachokiona niserikali kuwa kimya au kuchelewa kufanyia kazi mapendekezo ya report ya CAG! Navilevile tuangalia pia primary duty ya cag sio kudetect errors and fraud yeye primary duty yake ni Kutoa independent opinion! Ndivyo tulivyofundishwa huko vyuoni au wenzetu mmepita vyuo gani hewa au? Na nibora tuwaachie wataalum watoe maoni yao kuliko sisi tusionaupeo na ukaguzi Kutoka mapovu kiasi hiki!
Nyie ndiyo wachumia tumbo wenyewe tunaosikiaga, wana wa maslahi! Ulichokieleza hapo inaonekana una mwanga flan ama ni "staff" wa kada hiyo. Lakini kwa mstaarabu haipendezi kuchangia kama ulishakula hadi kujisahau kufuta mdomo. Utatupotosha.
Tutegemee ni nini utakacho-comment wewe? Si ni hicho ulichokiandiaka! Hivi wizi wa waziwazi unaofanywa na halmashauri mchana kweupe, hata wasio na taaluma ya uhasibu wanaujua! Sasa huwaje wanapokuja wakaguzi toka ofisi ya CIG na kutoa hati safi kwa halmashauri husika? Huwa kuna kitugani kinasababisha wezi waonekane wasafi na hawajakwapua chochote? Kama siyo primary duty yao, hiyo ya kugundua "madudu" na kuweka
"uozo" hadharani,huwa ni duty ya nani hasa?
Tatizo lililokuwepo Tz kwa ivisasa ni mtu kusomea taaluma si kwa ajili ya manufaa kwa nchi, bali ni kwa ajili ya manufaa binafsi ya "kupiga'ela",kama utetezi wako unavyoonekana kuegemea.
 
Back
Top Bottom