chambulilo
JF-Expert Member
- Aug 19, 2013
- 217
- 38
August 2013 nilitembelea mkoa ambao makao makuu ya kanda ya ziwa mashariki (kanda ya cdm) sikuamini pale nilipoonyeshwa ofisi ya makao makuu hayo ya kanda kwani haikuwa haifanani na zile za kata zilizopo mikoa ya kaskazini hususani Kilimanjaro!
Mwenyeji wangu alinieleza kuwa hata hiyo ofisi walipewa tu na msamalia mwema kwani zamani viongozi wake walikuwa wanakutana chini ya mti au bar au majumbani kwao.
Nilijuuliza maswali kibao pasipo kupata majibu;

- Je ruzuku ya chama inafika kaskazini tu kwingine haifiki?
- Mkoa huu ulimpa BABU SLAA zaidi ya kura laki tisa ( zaidi ya 45% kura alizopata) katika uchaguzi mkuu wa 2010, kwanini aupe kisogo na kukimbilia kaskazini sehemu ambayo aliambulia kura chache ukilinganisha na za mkoa huu?
- Michango ambayo uwa inakusanywa katika mikutano ya hadhara inakwenda wapi hadi kufikia ofisi kukosa viti na kulazimu viongozi kukaa katika vigogo ofisini hapo?
- Je Viongozi wa kanda na mkoa huu wanaogopa kuhoji ruzuku ya chama inapoishia wakihofia kunyang'anywa vyeo vyao na kufukuzwa uanachama?