Vipi maeneo ya Isanga, Nonde, Mabatini, Simike, Nzovwe, Ikuti, Iyunga, Iyela, Mwanjelwa, Ilolo, Kalobe, Mbalizi, etc mji unazidi kutanuka na serikali ya CCM haifikirii kufanya planning. Only 27% wanaishi kwenye surveyed area.
Wewe unaijua Mbeya vizuri sana,
Hayo maeneo yote uliyotaja ni ya kibabe sana na yanapendeza kubaki vile yalivyo sababu yamezalisha watu wagumu wa pale Mbeya,
Ila serikali sasa inawaboreshea huduma za Kijamii kama maji, hospital, shule na miundombinu ya barabara.
Ila tayari barabara ya lami kutoka kabwe hadi Isanga ilishajengwa mda mrefu sana,
Pia barabara ya kiwango cha lami kutoka Mwanjelwa, Ilemi hadi Isanga pia ilishajengwa mda mrefu sana.
Pia kuna barabara ya kisasa inyotokea pale uwanja wa kumbukumbu ya sokoine karibu na Rift valley Hotel, barabara ile inapitia Isanga hadi Chunya pia imefanya yale maeneo kupendeza zaidi na kuwasaidia watu wa Wilaya ya Chunya kutumia mda mfupi hadi kufika Mbeya mjini.
Ila Ilolo Kule ni utata sababu ni kama mkondo wa maji lile eneo, hata mvua za Elnino zilisababisha maafa makubwa sana katika maeneo yale ya Ilolo.
Kuhusu Iyunga, Mabatini, Simike n.k
Ni kwamba miji mingi mikubwa haikosi maeneo kama yale.
Mfano miji kama Nairobi, Kampala, Lagos Lilongwe, Dar es salaam, Durban, Mumbai, New Delhi n.k maeneo kama yale yapo pia, hiyo yote inasababishwa na kuongezeka kwa kasi idadi ya watu na serikali kutojipanga mapema na ongezeko la watu