Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki[emoji116]

[emoji445]Wengi mlijiuliza waloniteka ni Askari
Mkanitafuta vituo vyote central hadi Staki shari
Wakasema hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari.
(Daaaaah)
Ya kaisari muachie kaisari ,machozi yenu yatalipwa
Mi nafunga na kusali
(Imba Roma imba x3)
Mungu wa Paulo ndo Mungu wa Daudi
Na ndo Mungu wa John mnayemuita Yohana Wayahudi
Mwanangu alimuuliza mama baba lini atarudi
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi
Fahamu kuwa mimi siyo rapa tu ni baba wa familia
Na Watoto mahitaji nawapa kama isemavyo Biblia

Je
Kipi bora nife mseme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa ila nawaachaje waliobaki?
Je
Nani kati yenu mwabangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji? Wapi atapata mapenzi?
Mama naye wapi atapata mahitaji na malezi?
Na ripoti ya upelelezi vipi akiiteka mtekaji?
Je
Kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja niona mnangoja mje msibani ee?
Nilipokuwepo sikuwa najua hii saa nne hii saa nane
Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu zangu tuonane
Nimechapwa mijeledi ,nimevunjwa bila huruma
Asante mlopaza sauti nimeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefungwa macho mikoni imefungwa nyuma

Chorus
[emoji445]Nakwendaaa Zimbabweee Zimbombo
Iyelele mama weee x4
Imba Roma Imbaaaaa
Aaaaaaah Aaaaah
Eeeeehee Roma
(Sema baba wee)

Nasimama na ninaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Na nanasi linaoza Msoga, tikiti linaoza shamba
Walioniteka hawakuja na Noah ni uvumi na visanga
Ila kutekana tekana huu ni uhuni wa kishamba
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu kuijenga Tanzania moja
Mi sikuona nyota kwa shoulder ila najua we ni solder
Inshaallah
Ulikuja mwenyewe au ulipewa order? (ewala)
Aminini siku hazigandi
We ni Yanga mimi Simba kuwa mpinzani siyo dhambi
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani
Simba akichukua kombe sijui atapona nani!
Na kuna mbunge alisema nimemtukana mkuu
Utakuhukumiwa na mkono wa Mungu
Namshitakia aliye juu
Kwanza lini?
Na kwa nini?
Mi nimtukane Mjomba?
Umepewa gari ya wagonjwa mi Tanga wananijengea bomba
Mi mbarikiwa na nikifa kuume kwa Baba nitaketi
Na mtu wa watu that's why lilisimama Bunge la bajeti
Kunijadili Mtanzania kuwa makini pia
Makinikia nayatungia kuwa mapini pia
Nilitabiri utaitwa Rais kipindi ukiwa Waziri
Japo maisha siyo rahisi ila pongezi unastahili
Na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya jumapili
God bless imetimia Injili niliyoitabiri

Chorus
[emoji445]Nakwendaa Zimbabweee Zimbombo
Iyelele Mama weee x4
Aaaaah Aaaaah
Eeeeehee Roma
(Sema baba wee)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiki na uzuzu kabisa, yeye angesema wazi tu, haya ya mafumbo na sijuwi kumtumia mke wake na nini, ni kiki tu auze nyimbo zake, nyambafu kabisa...
Wewe ungeweza kusema?

latest edition
 
Kwanini ameamua kuita kibao chake Zimbabwe?

Je anamaanisha Zimbabwe anaenda yeyetu au yupo na watanzania wengine?

Jamaa ametumia fasihi iliyokomaa
 
hata alietekwa yupo kwenye sintofahamu! anamjua aliemteka lkn hamjui aliemtuma mtekaji..!
ni mambo ya siasa tu hakuna cha nguvu ya uma wala nini,hawakuhitaji kumzamisha jumla bali rejareja ndio maana anatutumbuizia sasa..

"nanasi linaoza msoga"
kumbe nanasi leo limekuwa tamu! tikiti nalo..? e ajuae nyasi..

kupuliza na kung'ata ndo stairi ya huyu jamaa lkn mungu wa daudi,paulo ndo mungu wa yohana john.. sasa kwanini kwa mmoja umempuliza sana lkn mmoja umemng'ata sana!!
hata hivyo yangoswe namuachia ngoswe..

ila upambanaji wako ni wakawadai jaribu kuongeza mbinu fanisi watakuuwa ndugu!
 
Mnh... Hapo kwenye 'nanasi' nilikua sijapang'amua.... Thanx
 
Mtu mmoja, mtaalamu wa elimu ya fizikia, Hisabati na elimu ya anga, Bw. Archimedes wa Syracuse aliyeishi kati ya mwaka 287 - 212 Kabla ya Kristu, aliwahi kutoa kanuni aliyoiita kanuni ya Archimedes (Archimedes' principle) akielezea namna chombo kinavyoweza kuelea juu ya uso wa maji, na yanayotokea hadi chombo hiko kiweze kuelea. Kwa lugha rahisi kanuni ya Archimedes' inasema; "chombo chochote kinapozamishwa chote au kwa sehemu fulani, chini ya maji/kimiminika tulivu, kuna nguvu inayokisukuma kitu hiko juu, nguvu hiyo inakuwa kubwa zaidi katikati ya uzito wa hiko chombo...."

Mfano wa maelezo ya kanuni hii; unapoweka mpira wa soka juu ya maji yaliyotulia, mpira utaelea, kwa kuwa kuna nguvu inayosukuma mpira huo juu, na nguvu hiyo ni kubwa zaidi katikati ya uso wa mpira. Mathalani, mpira huo ukizamishwa, bado nguvu ile ipo, na ikiwa nguvu ya kuuzamisha mpira itaondolewa, mpira utarudi juu ya uso wa maji. Na kwa hiyo, ili mpira uendelee kuzama, lazima nguvu ya kuuzamisha iendelee kuwapo. La sivyo mpira utaibuka na kuendelea kuelea.

Falsafa hiyo, ya 'The Floating balloon' ndio falsafa inayotumika kuelezea upinzani wa kiitikadi. Tangu kale jamii imekuwa na watu wanaopinga itikadi za kiutawala. Kuna misukumo kadhaa inayopelekea kuwepo kwa upinzani, ingawa sababu kubwa na rahisi kuelezea ni kwamba binadamu hawawezi kamwe kufikiri sawasawa, tofauti za kifikra ni tunda la asili, tamu kwa watu werevu, lakini chungu kwa wajinga.

Misukumo mingine ya kuwapo kwa fikra kinzani, zinazozaa upinzani wa kiitikadi, siasa nk, ni hamu ya kutaka kuongoza au kutawala kwa kuwa labda mtawala hawezi, au anaonekana kutoweza, au utawala uliopo unakiuka miiko iliyowekwa na jamii husika. Misukumo mingine inaweza kutokana na tamaa za kutawala kwa lengo la kufaidi tunu za jamii. Misukumo hiyo wanaweza kuwa nayo watawala, na ikiwa hivyo basi watawala hufanya matendo yanayopelekea upinzani kuongezeka.
Ndio vile, unapogandamiza mpira chini ya maji, nguvu ya kuurudisha juu inaongezeka. Kadiri unavyoongeza nguvu ya kuuzamisha, ndivyo nguvu ya mpira kurudishwa juu inavyoongezeka. Tofauti ya nguvu hizo mbili ni kwamba, ile ya kuuzamisha mpira chini, mara zote ni ya kutengeneza, lakini nguvu ya kurudisha mpira juu ya uso wa maji ni nguvu za asili. Fikra kinzani ni jambo la asili.

Ndio maana, kwa kutambua hili, R.O.M.A MKATOLIKI katika wimbo wake wa Zimbabwe, mwishoni mwa shairi la kwanza anawaambia walengwa wake; "kutekana tekana huu ni uhuni wa kishamba, weka bunduki chini si tushindane kwa hoja".

Kwa kuwa kutekwa kwa R.O.M.A MKATOLIKI kunahusishwa na msimamo wake wa kupinga watawala, na kwa kuwa watawala hawajatoa taarifa zozote zinazoshawishi kutokuhusika na uhuni huo, basi jamii inabaki na imani thabiti kwamba watawala walihusika. Na kama hivyo ndivyo basi falsafa ya mpira unaolea, inakubali hasa.
Kwamba, nguvu ilitumika kutaka kumzamisha R.O.M.A MKATOLIKI ili asionekane, lakini baada ya nguvu hiyo kuondoka, R.O.M.A MKATOLIKI anaibuka. Na ieleweke wazi, kwamba nguvu inayomuibua R.O.M.A ni ya asili. Wakati ile ya kumzamisha ni ya kuazima. Pia, si kila mtu anayeonekana kuwa mpizani ni mpinzani. Mfano halisi upo kwa madiwani wa Chadema wa Kaskazini wanaodaiwa kupokea pesa ili kuhama chama na kusaliti itikadi ya mabadiliko, hao ni cowards, wanaoingia kwenye siasa kwa ajili ya kipato, wakishapata kipato wanayasahau mahubiri yote waliotangaza kwenye mimbari ya siasa.

Lakini alichoonesha R.O.M.A ni ile nguvu ya asili ya kuonesha fikra kinzani, halisi na za asili dhidi ya mambo yasiyompendeza.

FUNZO.
Kuna jitihada za makusudi za kutaka kudhulumu utu wa mtu mwenye mawazo kinzani dhidi ya utawala wa Tanzania. Serikali kupitia jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola imehusishwa moja kwa moja na vitendo hivi ambavyo R.O.M.A anaviita uhuni wa kishamba. Rafiki na kamarade Ben-Rabiu WaSaanane hajulikani alipo hadi leo. Ile nguvu ya kukandamiza mpira chini ya maji, imeendelea kudumu katika suala la Ben Saanane, lakini kwa kuwa ni nguvu ya kuazima haiwezi kukandamiza milele yote. Akina Ben wataendelea kuwapo vizazi na vizazi. Na huo ni ujumbe wa kweli unawatia jazba, na aibu wanaofanya 'uhuni wa kishamba'. Kwamba, watahitaji nguvu hizo milele yote, kwa maana ingine, watakosa kufanya mambo mengine ya msingi kwa kuelekeza nguvu kubwa dhidi ya fikra kinzani, ambazo haziishi, hazichoki, hazina 'expire date'.
"Ni mtu mdogo tu wa kichwa anayedhani bunduki ya mwanadamu inaweza kubadili ubongo wa Mungu. Mungu wa Paulo, Mungu wa Daudi, ndio huyo Mungu wa John wanaomuita Yohane wayahudi.

MWISHO.
R.O.M.A MKATOLIKI, namfananisha na mpira uliozamishwa lakini nguvu ya kuuzamisha ikashindwa na nguvu ya asili, ambayo R.O.M.A ameibatiza na kuiita nguvu ya umma kama anavyoimba,

"Nimechapwa mijeredi, nimevunjwa bila huruma, asante mliopaza sauti nimeiona NGUVU YA UMMA".

Nguvu ya Umma aliyoiona R.O.M.A ndio hiyo hiyo iliyomfanya aimbe kwa namna ya kufunguka kwa kile kilichomsibu, ni nguvu inayojidhihirisha kwa namna tofauti tofauti. Kwa kuimba, kwa kukemea majukwaani, kwa kuandika na wakati mwingine kwa uasi. Ndio, uasi! Sio mara zote waasi ni watu waovu, uasi dhidi ya uasi ni wema unatukuka machoni kwa Mungu. isipokuwa, maana halisi ya uasi inaweza kupotoshwa. Wapo waasi wanoishi ikulu, kuamuru majeshi na taasisi za kiserikali, nao wanastahili adhabu ileile wanayostahili waasi wengine. Lakini nirudie, tafsiri ya uasi inaweza kupotoshwa.

Tuendelee, kunakili vipande vya mashairi ya R.O.M.A MKATOLIKI huku tukijiuliza kama tunafanana na falsafa ya mpira wa soka juu ya maji, au pengine nguvu kidogo inahitajika kututoboa na kutuzamisha kusipo na jua, ambapo hujui hii saa nne au saa nane?
Nawakumbusha pia, mtakao comment kwenye makala hii; R.O.M.A anawaambia; Kunijadili mtanzania, kuwa makini pia, Makinikia...."

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeandika bango lenye kuchosha kusoma ila point ni chache sana, huku ukitolea mfano wa kanuni ya Archemedes uliyoikosea, mkuu ulikuwa unasoma physics kwa kukariri au kuelewa, mbona maelezo ya kanuni ya archimedes hayapo hivyo.
Ngoja nikurekebishe kidogo, ina maana hii...
kiasi cha kiiminika kilichopatikana baada ya chombo kuzamishwa hufanana na nafasi ya ukubwa wa chombo (hii ni quoloquial language ya kiswahili)..the amount of water displaced is equal to the volume of the object immersed into a liquid.
 
Hkna neno kiiminika kweny kiswahili ndgu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani katika huu wimbo mpya wa Roma Mkatoliki (ZIMBABWE) hii verse bado sijailewa kabisa kwamba alimaanisha nini?

Mungu wa Paulo, ndio Mungu wa Daudi, ba ndio Mungu wa John mnayemuita Yohana wayahudi...

Swali ni je

1,Hivi hapa alimmaanisha Daudi huyu wa dsm, au?

2, vp kuhusu John na Yohana?

Karibuni (ila msinipime mkojo)
 
Back
Top Bottom