Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Daud wa dsm, john wa mjengon ambaye wayahudi (mafisi) wanamwita Yohana kwa maana amekuja kutengeneza nchi si huwa anajitapa at anainyoosha.
 
kitu pekee ambacho nimekuwa nikimuombea uyu dogo ni kwamba, awe alitekwa lakini walimhurumia kumtatua rinda. kama atakuwa amepoteza rinda hapo sasa, sijui atafanyeje. ila kwa trauma ile aliyokuwa nayo wiki lile, aisee kuna siku Mungu atawalipa watesi wake tu.


Hilo la "KUTATULIWA RINDA" ndiyo issue yenyewe !!!!
 
Mungu wa Abraham,mungu wa yakobo,mungu wa isaka hata mungu wako pia..
 
Nilichoelewa kwenye Wimbo wa Roma.

Maana ya nakwenda zimbambwe ni kuwa nchi yetu inaelekea kwenye hali ambayo zimbabwe wanayo kwa miaka mingi sasa.

Zimbabwe ni nchi ambayo ipo katika hali duni ya kisiasa, kiuchumi na masuala ya kijamii pia..( Pale kwenye video utaona watoto wamevaa nguo chakavu na zilizochanika, hicho ni kiashiria cha maisha duni)

Kiashiria cha maisha duni tena ni yule bibi. Kuna bibi kama anapiga kinanda hivi (Kuna bibi yuko peku, hajavaa viatu pia usoni ana huzuni na amechoka sana...hii pia ni kielelezo cha hali ya Tz ikifaninishwa na hali ya zimbabwe)


Tatu, kuna jamaa kama ni Daktari hivi na yule jamaa anaetengeneza pikipiki..inafika mahali wanaonyesha kumlalamikia Roma ( hii hapa inaonyesha namna wafanyakazi wanamlalamikia kiongozi na serikali kwa ujumla, hali ambayo pia ipo nchini Zimbwabwe...kuna watu wanaumia kwa sababu ya maamuzi mabaya ya viongozi3)

Nne, Mazingira aliyofanyia video yanaashiria ukame na hali ya ujangwa na mifugo inapita (Kuna hali ya ukame sana zimbabwe na ndio hali ambayo tunaeleka Tz, mambo ya kama njaa na n.k)


Tano, Kuna dogo amevaa T-shirt imeandikwa Diamond Platnumz, Ikumbukwe kuwa Daimond alitoa nyimbo inaitwa "Nakaa kimya" wakati Roma yuko ndani.

Nyimbo yenyewe ilikuwa inajaribu kuweka usawa kati yake na mlezi wake Bw. Paulo Makonda. Wakati huo makonda alikuwa anapigwa vita sana kuhusu elimu yake kwenye social media. Sasa Diamond akawa anataka kuweka lile jambo libalance badala ya kutoa wimbo wenye Harakati za kumtafuta Roma.(Though alimtaja kwenye wimbo huo pia). Ile T-shirt ni ujumbe kwa DP


Mwisho, Roma anaongoza msafara mkubwaa wa watu wanamfata nyuma. Hii maana yake ni utabiri kuwa kuna siku atatokea mtu wa kuongoza watu na kuwatoa pale jangani

Kama utafanyika ukombozi flani hivi wa kutoa watu Zimbabwe...

Binafsi nimpongeze Roma kwa usanii wake.
 
Hakuna kitu nimeusikiliza huo wimbo mara 6 hakuna sehemu amemtaja aliyemteka zaidi ya kuwazodoa waliokuwa wanasema ilikuwa Noah or Wajeda...
Hana jeuri ya kuwataja waliomteka ana tafuta huruma tuu ya wananchi...
Mkuu ndo wewe alikutaja katika wimbo wake kuwa"mpaka rutashobolwa awe hakim kisutu"?

huwezi jua
 
Back
Top Bottom