Office Romance

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,449
18,454
Mapenzi mahali pa kazi au maofisini ni kitu cha kawaida sana kusikia siku hizi, hii ni kwa sababu kushuka kwa nidhamu makazini na kwamba tunatumia muda mwingi sana kuwa ofisini kuliko nyumbani hivyo wafanyakazi huwa na muda wa pamoja kuliko hata familia.
Urafiki wa mapenzi ofisini kama hujaoa au kuolewa unaweza kukusaidia kuoa au kuolewa au unaweza kukusababishia madhara makubwa kiasi cha kufukuzwa kazi au kufungwa jela na kupata magonjwa kama UKIMWI, kuharibu taaluma yako na sifa zako, pia kuvunja ndoa za wengine kitu ambacho ni hatari zaidi.

Pia suala la mapenzi kazini huweza kusababisha kuzorota kwa utendaji na ufanisi binafsi wa mtu kazini.
Mapenzi na kazi ni vitu viwili tofauti sana ndiyo maana waajiri wengi hawaruhusu watu kujihusisha ma masuala ya mapenzi kati ya wafanyakazi.

Pia kuna utafiti unaonesha kwamba (Vault.com) nusu ya watu wanaofanya kazi maofisini huvutiwa kimapenzi na mtu mwingine wa jinsia tofauti katika ofisi moja na wengine hupelekea hata kuoana kabisa.

"Si vema kuchanganya biashara, kazi na mapenzi ofisini"

Wapo watu wamejitoa muhanga kuwaridhisha mabosi wao kwa mapenzi ili kujihakikishia kupata kazi nzuri au kuongezewa mshahara, au marupurupu au kupewa visafari kikazi au kupelekwa kusoma nje ya nchi, hata hivyo matokeo yake ni kudhalilika na wakati mwingine kujipatia bonus ya magonjwa kama HIV/AIDS.
Pia wapo mabosi au waajiri ambao bila kutembea (sex) na mtu anayemwajiri bado hajakamilisha taratibu zake za kuajiri, hii ni tabia mbaya sana na si ya kistaarabu.

Je, hali ipoje katika ofisi yako kuhusiana na suala la mapenzi kazini au ofisini?
Je, katika ofisi zetu za serikali hali ipoje?
Na huko kwenye sector binafsi hali ipoje?

Naamini kila mmoja wetu ana jibu kwa haya maswali

 

Gaga

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,558
1,942
kwenye kila ofisii nafikiri hili lipo, utakuta tu kuna watu fulani wana uhusiano, sie kuna bosi wa kike single lakini kazaa kabisaaa na kijana wa chini yake na tupo tunaendelea na kazi, huwezi jizuia kama hisia ziimezidi juu a mtu fulani, na hasa kama nafasi unayo(yaani uko single) hizi hook ups ziko sana tu
 

Twande

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
543
169
Mara nyingi zinatokea sababu ya insecurities! Mazingira mageni ya kazi wenyeji wanampiga vikumbo anatokea kijana anakuwa karibu na mlengwa (especial mwanamke) ambae anapata ujacr sasa anapokuwa na uyo kijana! Pia mwingine ajajua kaz vzr mgen akitokea msaidiaji bas wanamaliza yote! Wengine ndo izo za mabos ila iz zimekaa kifuska zaid! Izo zingine zinatokea automaticaly! Thats my little research..na zingine zinatokea mazoea ukaribu kila cku hatimae ndo ivo! Mi mvivu sana kuandika ningeeraborate zaid hii mada!
 

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
hapa suala la kuwa wapezi si tatizo .. tatizo kufanya mapenzi ofisni maana nalo hilo linafanyika sana
 

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,199
17,991
mwaya naona speed zao kubwa wacha tukumbushie wengine wameanza akuzaa nao m hny swt baby wa kazini loh..

Inapendeza... ila angalia maana mara ya mwisho wewe ndio ulichangia nipate na Mupenzi hapa hapa JF....lol
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,449
18,454
Inapendeza... ila angalia maana mara ya mwisho wewe ndio ulichangia nipate na Mupenzi hapa hapa JF....lol

ndio maana nikisikia mtu anataka kugusa mali yangu nampm shemeji fasta sitaki kero nyumban mizigo inaongezeka ukirudi tena na wewe loh@@
 

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
790
Semina zote, warsha, mikutano ya nje ya ofisi na safari za kikazi watataka wapangwe pamoja!
 

UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,365
5,040
Ni kweli kabisa haya yapo na yamenikuta kwani
Utakuta ni mtu mpo naye office moja mnashare
Matatizo yenu na unajikuta asipokuwepo
Kazini unanyongonyea isipokuwa hamtakiwi
Kwenda zaidi kama nyie wote mna familia
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom