Odila Ongara afariki dunia

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,495
1,250
Marehemu Odila Ongara alikuwa mtumishi mwandamizi serikalini hadi kufikia ngazi ya Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali. Amefia Iringa jana.

Poleni wafiwa wote.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,221
2,000
katibu mkuu wizara zipi?kama nishati na madini aliwahi kupita apumzike kwa amani
 

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,012
2,000
AliKUwa ni mme wa wake wengi mke mmoja wapo wa kwake ni Dr. Mariam Ongara aliyekuwa ni Mganga mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
 

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,438
2,000
Aliwa ni mme wa wake wengi mke mmoja wapo wa kwake ni Dr. Mariam Ongara aliyekuwa ni Mganga mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
ni kipi ambacho kimefichika mbele ya macho ya JF?labda kibol ni nani ndio haifahamiki,lakini the rest yamo humu.
 

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
775
1,000
Wajaluo waliowahi kushika madaraka makubwa TZ

Mzee Opio
Sylvanus Adel
Mzee Odunga
Mzee Ongara


Malizia...............!
 

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,826
2,000
Mzee Odira Ongara alikuwa ni mmoja wa viongozi wachache ambao Mwalimu aliwaamini sana katika nyadhifa ya Ukatibu Mkuu (Wizara ya Ujenzi n.k) na Ukurugenzi wa Maendeleo wa Mikoa mbalimbali na alitumikia taifa kwa uaminifu na uzalendo mkubwa sana katika nyadhifa zake hizo;

Ifahamike kwamba ukatibu mkuu wa Wizara ndio nyadhifa ya juu kabisa/highest rank ya utumishi wa umma katika nchi yetu; Inasikitisha kukabiliana na ukweli kwamba serikali yetu haina angalau mpango wa na kuja maktaba ya kumbukumbu/historia za viongozi wa taifa letu ili vizazi vya baadae vije kujifunza kuhusu viongozi mbalimbali waliotumikia taifa letu; Poleni sana wana familia; Mungu amlaze mahali pema peponi; Amina;
 

prince pepe

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
215
0
Kila nafsi itaonja mauti. Mwenyezi Mungu awape faraja ndugu, jamaa na marafiki katika wakati huu mgumu

R I P ONGARA
 

RORYAKWETU

Member
Nov 18, 2011
83
95
Mama yangu mzazi ni mtu wa Utegi na binafsi nimesomea elimu yangu Nyanduga sekondari shule iliyo karibu sana na kwao marehemu. R.I.P mzee Odira Ongara
 

cham

Member
Dec 20, 2011
24
0
Mzee Ongara kumbe alikuwa bado hai !! Alikuwa muungwana sana na Katibu mkuu safi sana kwa muda mrefu. Mungu amlaze mahali pema peponi.AMINA
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
12,688
2,000
Lala pema peponi Mzee Ongara!!! Ila kwa kweli sijui ni namna gani systme inawatunza viongozi waandamizi wastaafu!! Maana kana ni kwa pensheni kwa miaka yao si ajabu akawa analipwa sh. 150/- kwa mwezi!!! khaa!! Pension nayo iwe na kima cha chini kwa kuangali hali ngumu ya maisha jamani. Wazee kama hawa hawakuwa na ufisadi wa aina yoyote ile ni kama akina Makweta tu.
 

Vegetarian

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
642
500
Poleni sana wafiwa. Naamini mlimpenda ila Mungu kampenda zaidi,mi binafsi simfahamu,ila nimewahi kusikia sifa yake ya uadilifu akiwa katibu mkuu wa wizara ya ujenzi. Mwenyezi Mungu amlaze pema mbinguni. Amina.
 
Top Bottom