October to remember

October to remember

Vaa viatu vya ndugu, jamaa, marafiki wa hawa wote...

Kama bado moyo wako unapiga, na bado damu yako inatiririka ndani ya mishipa,

Huwezi kukaa kimya kwenye taifa ambalo UHAI WA MTU NI KAMA WA KUKU, yaani mtu mmoja anaweza kuamua tu KIJINGA JINGA LEO USIWEPO na kesho TUNAOKOTA MAITI YAKO au FAMILIA INASIMULIA ULIVYOCHUKULIWA NA MANINJA au WATU WENYE GARI LA POLISI AU NAMBA ZA SERIKALI KAMA STJ, STK nakadhalika!

Kama USALAMA WA TAIFA (Watu na mali zao, rasilimali za nchi) SI KIPAUMBELE CHA UTAWALA, tunawezaje KUKAA KIMYA NA KUSUBIRI MIAKA 5 TENA YA NAMNA HII? KATU, ABADANI, MUNGU HATARUHUSU HILO, NA WENYE NCHI, WANANCHI HAWATARUHUSU HILO NG'O!

Kwenye VIDEO HII, hata uwe CCM, CHADEMA au CHAMA CHA SHETANI, huwezi KUBAKI ULIVYO, maana, WAKIZOEA KUUA NA KUTEKATEKA NA TUMEKAA KIMYA, ZAMU IJAYO NI YAKO UNAYESOMA NA KUCOMMENT,

NA OKTOBA HII, KAMA MUNGU AISHIVYO WAMEFIKA MWISHO, WANAOSAFIRI HAWAFIKI WAENDAKO! HAWAFIKI, HAWAFIKI NA HAWAFIKIIIIII....
 
BREAKING: Kapteni John Charles Tesha ni mwanajeshi halali wa anga. Tumepata intake slip yake, intake 58, mkufunzi SAK (Airforce) tokea July 2022.
 
IMG-20251004-WA0030.jpg
 
^Nimeambiwa hapa kwamba unajua kwenye protocol za Jeshi

Captain anaongoza kikosi kizima so huyu kwenye kikosi chake tu akiamuru kiwake kinawaka mazima maana akiita parade wanakuja wote mpaka walioko nje ya Dar.

Halafu Mwanajesh mmoja ni sawa na police 3-5.^

Haya mambo ndo nimejua leo, yajayo yanaburudisha😂
 
Kwa Mujibu wa Taarifa mbali mbali mtandaoni zinadai taarifa za Captain Tesha ni kama ifuatavyo:

Jina: John Charles Tesha (J. C. TESHA)
Rank: Captain
Intake No. 58, 2014
Force No. P. 13353

Taarifa za July 22, 2025 zinathibitisha Tesha bado ni “active” (A1)
Ni mkufunzi wa zana za anga za kivita katika shule ya kijeshi ya anga SAK (Airwing) ndani ya Airforce.

Chanzo: Mtandaoni
1759631388822.jpg
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI



Job Mrema: Hiyo Flash utaitambuaje pia?

Kaaya: Nitaitambua ina GB 8 na ina rangi nyeupe.

Job Mrema: Waheshimiwa Majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.

Vituko sana. Muda wote shahidi anatusumbua nitaitambua video, nikiona kitu fulani na kitu fulani. 😂

Mwisho wa siku kumbe video yenyewe na flash hiyo italetwa na shahidi mwingine sio yeye.

Makaratasi mengi wanatumalizia misitu tu bila sababu ya msingi.😂

Ngoja sasa aanze kusokotwa.

Kinachofuata sasa ni CROSS EXAMINATION yaani maswali ya DODOSO kutoka kwa CRISTIANO RONALDO AU MESSI wa Sheria Mh. Lissu.

Jaji anasema Mshitakiwa unasemaje?

Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu Shahidi asiende hivi hivi naomba mnipatie nusu saa nianze nae leo leo au hata kama mkiniruhusu niendelee nae hadi saa mbili usiku niko tayari.

Jambo lingine off record jana niliwaahidi nitawaleteeni kitabu nilichoandika miaka mitano iliyopita kinaitwa "Remaining in the Shadow" kuhusu mambo ya Uchaguzi pia.

Nimebeba copy tatu hapa naomba niwape na Mawakili wa Serikali Copy moja nao wakasome ili wajue mambo mengi wasidhani mimi ni mtu wa mchezomchezo na waache kutumika tu.

Majaji pia nawapatieni copy moja.

Jaji Ndunguru anasema sasa unatupatia copy moja tunasomaje si bora ungetoa copy mbili?

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nikiwapa mbili mtagombana sana maana mko watatu.

Watu wanacheka.

Jaji Ndunguru: Sasa wewe ugomvi wetu haukuhusu, tupe hizo copy mbili sisi tutajua cha kufanya.

Watu wanacheka. 😂😂😂

Mhe. Lissu: Basi nyie Vijana anawanyooshea Wakili Kisabo na Mahinyila kuwa hakikisheni kesho mnaongeza copy zingine 4 zije hapa.

Jaji Ndunguru anasema sasa jamani tutaendelea kesho.

Muda umeshakwenda.

Shahidi kapumzike na Mshitakiwa na wewe kajiandae na kesho tuendelee na Cross Examination saa tatu kamili asubuhi.

Inapigwa Courttttttt kubwa sana.

Majaji wanasimama na kutoka.

Kesi imeahirishwa hadi kesho asubuhi saa tatu.
 
Back
Top Bottom