OCI ya CHADEMA huko Igunga yaendelea kuchanja mbuga vijijini

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Wakuu ingawa mawasiliano na makamanda walioko field huko Tabora katika Operesheni Chukua Igunga (OCI), si mazuri sana, bado tumeweza kupata walau taarifa kidogo juu ya kinachoendelea. Taarifa zilizopo ambazo zilipatikana kabla mawasiliano hayajakatika kabisa zilikuwa zinaonesha maendeleo mazuri kwa OCI. Jana (katika siku ya pili) makamanda hao, baadhi yao kutoka makao makuu wakisaidiana na makamanda wa huko, waligawanyika katika timu kama nane hivi, wakishambulia tarafa kadhaa kwa mpigo.Mathalani katika katika vijiji vya Mwamashimba na Mwamakona, kulikuwa na mikutano mizuri sana. Naambiwa na mtoa taarifa kuwa wanavijiji wengine wanatoa machozi kila wanapopigwa dozi juu ya local issues zinazowasumbua na jinsi zilivyo na uhusiano na utawala mbovu wa CCM kwa miaka 50 baada ya uhuru. Wakuu hii ya kuwatoa machozi wahudhuriaji mkutano nimeishuhudia sana katika mikutano ya hawa jamaa. Mara ya mwisho nilimwona Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, Bw. John Mrema niliwashuhudia akiwatoa machozi akina mama pale Mzumbe, Morogoro. Taarifa zinaongeza kuwa OCI pale Mwamashimba ni kama vile ilichukua kijiji kizima, kwa jinsi walivyopigania kadi wakitaka kujiunga katika course for change kupitia people's power. Nitaendelea kuwapatia vitu kadri ya muda...
 
Taarifa zingine nilizozipata punde tu baada ya kurusha hiyo post, zinasema hali ya namna hiyo kama ilivyotokea katika Kijiji cha Mwamashimba, pia imetokezea huko Ijogohya, Imalanguzu. Wanakijiji wanakimbilia kujiunga CHADEMA, kwa kasi ya ajabu. Aliyetoa taarifa yeye anasema "kijiji kizima kimehamia CHADEMA (lakini nimemkatalia kusema lugha hiyo, haiwezekani kijijiji kizima! Kijiji kizima aisee! hapana) Lakini kwa wale wasiojua, vijijini wananchi wanajivunia sana kadi. Nimewahi kushuhudia wengi wao wakishakabidhiwa kadi, kwa kununua, huwa wanazikumbatia kwa furaha utafikiri wamepata mkombozi hivi. Nitaendelea kuwapatia taarifa. Hii ya mwisho aliyenipatia/kunijuza, alikuwa amepanda juu ya mti ili afanikiwe kupiga simu. Mawasiliano ni shida balaa. This is interior penetration brothers. Hiyo ndiyo OCI (Operesheni Chukua Igunga).
 
Je huoni kuwa kufanya mikutano sasa hivi wakati hilo jimbo liko wazi sio kuvunja sheria?.Je hiyo haitaonekana kama ni kupiga kampeni kabla ya uchaguzi?
 
Hao kina mama wa Igunga inaonekana ni hodari wa kulialia, wakati Mlafi Rostam anawaaga walilia, saizi wanagongelewa dose wanalia. Hata akienda msanii Jah-Kaya watalia tu...the trust I have in them is depreciating with days
 
Siyo kampeni kwa vile hawana mgombea wanae mnadi. Wangekua tayari wana mtu wao wanaomba wananchi wampigie kura muda ukifika ndiyo ingekua kuvunja sheria za uchaguzi. Kama unavyo takiwa kufahamu mkuu hakuna kampeni bila mgombea. Unless kuwe na ushahidi kuwa kuna mtu wameanza kumnadi.
 
Safi sana CDM,songa mbele huu ndiyo wakati muafaka kwenu!!
daftari la kudumu la wapiga kura lingerekebishwa kwanza kabla ya huo uchaguzi kwa sababu maelfu ya vijana watawekwa kando kiulazima.
hAWA VIJANA NI WENGI NA NDIO WATAKAOAMUA MSHINDI
 
Taarifa zingine nilizozipata punde tu baada ya kurusha hiyo post, zinasema hali ya namna hiyo kama ilivyotokea katika Kijiji cha Mwamashimba, pia imetokezea huko Ijogohya, Imalanguzu. Wanakijiji wanakimbilia kujiunga CHADEMA, kwa kasi ya ajabu. Aliyetoa taarifa yeye anasema "kijiji kizima kimehamia CHADEMA (lakini nimemkatalia kusema lugha hiyo, haiwezekani kijijiji kizima! Kijiji kizima aisee! hapana) Lakini kwa wale wasiojua, vijijini wananchi wanajivunia sana kadi. Nimewahi kushuhudia wengi wao wakishakabidhiwa kadi, kwa kununua, huwa wanazikumbatia kwa furaha utafikiri wamepata mkombozi hivi. Nitaendelea kuwapatia taarifa. Hii ya mwisho aliyenipatia/kunijuza, alikuwa amepanda juu ya mti ili afanikiwe kupiga simu. Mawasiliano ni shida balaa. This is interior penetration brothers. Hiyo ndiyo OCI (Operesheni Chukua Igunga).

Asante kwa Taarifa. Ila kuweni makini na hizo kadi, isije kuwa CCM wamewatuma wakanunue kisha Magamba yakianza yanaigiza zinarudishwa.
 
jimbo hili likichukuliwa na chadema itakuwa ni meseji nzito kwa magamba kuwa nchi imewashinda hivyo wanapaswa kuondoka ilkulu kabla ya 2015
 
Hao kina mama wa Igunga inaonekana ni hodari wa kulialia, wakati Mlafi Rostam anawaaga walilia, saizi wanagongelewa dose wanalia. Hata akienda msanii Jah-Kaya watalia tu...the trust I have in them is depreciating with days

Mchungaji mmoja alikua anahubiri,na katika mahubiri yake mama mmoja alikua akimuangalia
analia kweli kweli,basi yule mchungaji akaendelea kuhubiri akijua "neno" lina muingia yule mama!

Baada ya ibada akamfuata yule mama akamuuliza:-
mchungaji: inaonekana umemkosea Mungu sana,ni dhambi gani hiyo ili nikuombee?

mama:sijafanya dhambi yoyote mchungaji,ila kila nilipo kua nakuona na ndevu zako hizo
nilikua nakumbuka beberu wangu aliye ibiwa week moja iliyo pita!

mchungaji: *************!!!!!!!!!!!!?????####

Wamama hao kulia haimaanishi ushindi kwa wale wanao watolea machozi,ila ni busara kuwadadisi wanalilia
lini,yawezekana wametapeliwa sana na kila wakimuona mwanasiasa wanataka "kumla nyama" ila
dhamira zao zinawasuta na kujikuta wanalia,msishabikie kila kitu kwa kudhani kiko on your beneficial side
 
Asante kwa Taarifa. Ila kuweni makini na hizo kadi, isije kuwa CCM wamewatuma wakanunue kisha Magamba yakianza yanaigiza zinarudishwa.

haha,wananunua buku wanaenda kuuza 10,000/=
ama kweli maisha magumu sana,ndo wakati wa biashara lakini huu
 
The CHADEMA political Cubs; BAVICHA - mambo mbele kwa mbele huko Igunga mpaka kieleweke!!!!!!!!!! Wananchi kote miji na vijijini huko wakishaamua kukipenda CDM na kukipotezea Chama Cha Magamba, je ni nani wa kuwazuia Tanzania hii???

Back
Top Bottom