Ocean Road kuitwa Barack Obama road

Ocean Road kuitwa Barack Obama road

Waafrika kwa ubaguzi wa rangi tu hatujambo.

Kaja George Bush kamwaga misaada ya kupigana na Malaria hawakumpa hata kimtaa cha mkia kama cha Joshua Nkomo pale SHIHATA.

Obama hata hajafika washampa Ocean Road yetu, wengine vitovu vyetu vimetupwa hapo mkibadilisha jina la barabara numerology zitakataa kukubaliana mambo yetu yatakosa kwenda sawa /s 🙁
 
MWAI KIBAKI ana barabara imejengwa 4 ways THIKA SUPER-EXPRESS HIGHWAY,wewe unamwita hapa unatafuta kichochoro cha matajiri uchwara wa MBEZI beach kukwepea traffic jam unakiita MWAI KIBAKI ROAD?Ndiyo maana mzee wa watu akashauri WATZ mtembee tembee hata huku EAST AFRICA muone wenzenu wanafanya nini!PITY!

Ningekuwa na cm ya maana ningekugongea "Like".
 
eeeeeeeeeeenhe sitashangaa hata ikulu ikibadilishwa
jina.huu utawala wa majanga kabisa.
 
Kinadharia itaitwa hivyo lakini kivitendo itaendelea kuitwa Ocean road.
 
Hizi tabia za kuwapa viongozi wa nchi zingine majina ya barabara wamerithi kwa Nyerere.

Kwahio urithi huo ni mzuri sana maana baadae walibatiza uwanja wa ndege na ukaitwa JKN au sio?

Lakini ni watu wanagombana kule Mbeya kuhusu jina la Mheshimiwa Kikwete liwe jina rasmi la uwanja wa ndege, sifahamu wamefikia wapi.

Ila sidhani kama ni urithi bali kasumba tu na ushamba.
 
Mbona sasa watamaliza zote kuzigawa mpaka itafika wakati zianze kurudiwa sasa
 
Plato alisema hakuna mfumo mbaya wa utawala kama demokrasia maana unawafanya wapumbavu kuwatawala werevu. mnaona matokeo ya mfumo huo? Watu wanaoamini kuwa hatuwezi chochote bila kusaidiwa wanatuongoza hivyo wanalamba viatu vya bwana zao. Du! hebu na watangaze J3 hakuna kwenda kazini tukajilimie vishamba vyetu huko Kisarawe maana hata tunachozalisha sioni faida yake zaidi ya kufadhili safari za kujikomba kama hii ya Obama. Yaani we acha tu nina hasira na hawa wakware wanaotufanya wote tuonekane tunasupport ndoa za jinsia moja!!!!!
 
umezoea uwongo na kueneza chuki ... lakini ujinga ndiyo sababu

Wewe mtoto wa Bavicha hujui chochote kaa kimya.

Unaijua barabara ya Nkuruma? Unaijua barabara ya Lumumba? Unaijua barabara ya Rwagasore? Unaijua barabara Kenyatta? Unaijua barabara ya Nkomo? Unaijua barabara ya Azikiwe? Unaijua barabara Sam Nujoma? Unaijua barabara ya Indira Gand?
 
Kila mtu na apewe chake. Akija David Cameron naye atapewa yake. Francois Hollande naye atapata yake......hadi ziishe zote.

Wale mababu zetu waliopigania ukombozi akina Kinjekitile, Mkwawa, Isike, Mirambo na wengineo walie tu...!
 
Kuna watu watajitolea Ma bint na Wake zao kwa Obama.
Kuna watu washatoa PHD (OUT)
Tutaona mengi sana ...
 
Hii ni ulimbukeni tu na kujionyesha watanzania jamani tuamke wenzetu wakenya wanatucheka na kutuona wajinga.
 
Waafrika kwa ubaguzi wa rangi tu hatujambo.

Kaja George Bush kamwaga misaada ya kupigana na Malaria hawakumpa hata kimtaa cha mkia kama cha Joshua Nkomo pale SHIHATA.

Obama hata hajafika washampa Ocean Road yetu, wengine vitovu vyetu vimetupwa hapo mkibadilisha jina la barabara numerology zitakataa kukubaliana mambo yetu yatakosa kwenda sawa /s 🙁
Hahhaaah.
Mkuu Kiranga, ndio nyie mliozaliwa Ocean Road halafu kitovu kikazikiwa baharini sijui.
BTW, nadhani jina la hospitali yenu litaendelea kubaki hivyo hivyo. So mutaendelea kuwa wa mujini tu.
 
Me nawaza tu hapa na Ocean Road Hospital itaendelea kuitwa hivyo hivyo au itaitwa Obama avenue Hospital.
 
Hiyo bara bara ilikuwa inatambulisha hospitali, hawapaswi kufanya hivyo. Kwanini wasiipe jina hilo bara bara ya Tabata-kinyerezi-majumba sita, kama shida ni kumuenzi?
 
sasa na hospitali itaitwaje? Ocean road hospital au barak obama road hospital? Poor minded! Akili ndogo kutawala akili kubwa.. Aagh..!
Nadhani itaendelea kuwa Ocean Road Hospital. Ni kama vile ilivyokuwa National Bank of Commerce (NBC) kwa mfano, hata baada ya kuuzwa iliendelea kuwa NBC hivyo hivyo japo safari hii haina kirefu chake. Yaani inabaki kuwa NBC bila kuwa na maana yoyote.
 
Back
Top Bottom