Hivi hii jadi ya utumwa itaendelea mpaka lini? Kila akija mgeni basi barabara zinabadilishwa majina, kwani JK anapokwenda Marekani na nchi zingine zote ameshawahi kupewa hata kichochoro? Tumezidi kujidhalilisha kila kukicha. Hilo jina lina historia yake likimaanisha barabara inayopakana na Bahari (ya Hindi). Juzi tu jina la barabara ya Bagamoyo ya Zamani (old Bagamoyo Road) lilibadilishwa na kuwa Mwai Kibaki... Kwa nini kama wanampenda sana huyo Obama wasijenge barabara mpya wakaiita Obama Road? Na hospitali ya Ocean Road, hospitali kubwa ya kwanza kujengwa hapa Dar Es Salaam nayo sasa itaiwa Barack Obama Hospital? jk na serikali yako mnatia kichefuchefu... halafu mnatuambia watanzania hatuna uzalendo, uzalendo utoke wapi wakati mnauza mpaka barabara? Shame on you...