'Obama wa Urusi' Mwafrika Anayetaka Kufuata Nyayo za Obama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Obama wa Urusi' Mwafrika Anayetaka Kufuata Nyayo za Obama

Discussion in 'International Forum' started by TANMO, Sep 2, 2009.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Mwanafunzi wa Afrika aliyemaliza digrii yake na kulowea nchini Urusi akifanya biashara ya kuuza matikiti maji anataka kufuata nyayo za Barack Obama kwa kufanya vitu ambavyo haviwezekani kwakuwa mweusi wa kwanza kuingia kwenye siasa za nchini Urusi nchi ambayo ina kiwango kikubwa cha ubaguzi wa rangi.

  Mkulima aliyezaliwa barani Arfrika anataka kufanya miujiza ya kuwa mweusi wa kwanza kuingia kwenye siasa ya nchini Urusi baada ya kupata changamato ya Barack Obama kuwa rais wa kwanza wa Marekani.

  Joaquim Crima mwenye umri wa miaka 37, alizaliwa nchini Guinea Bissau na baadae kuanzisha makazi yake kusini mwa Urusi baada ya kumaliza digrii yake ya kwanza nchini humo na kuoa mwanamke wa Urusi.

  Crima ana nia ya kuwaletea maendeleo watu wa wilaya yake na kutokomeza rushwa kwenye wilaya hiyo iliyopo kwenye ukanda wa mto Volga.

  Kutokana na ndoto zake za kuleta mabadiliko kwenye nchi hiyo ambayo ina kiwango kikubwa cha ubaguzi wa rangi, Crima amebatizwa jina la "Obama wa Urusi".

  "Nampenda Obama kama mwanasiasa ambaye amethibitisha kuwa hakuna kitu kigumu duniani" alisema Crima na kuongeza "Nafikiri naweza kujifunza baadhi ya vitu kutoka kwake".

  Crima ambaye pamoja na kuwa na digrii yake alikuwa akiuza matikiti maji kabla ya kuingia kwenye siasa, amefanikiwa kuwavutia watu wengi hata hivyo bado ana kazi kubwa ya kuwabadilisha mawazo warusi ambao hawataki kuwa na kiongozi mweusi.

  "Alikuwa akiuza matikiti maji na ghafla sasa anataka kuwa kiongozi wetu, Urusi ina wageni wengi hatutaki wageni zaidi, Urusi haiko tayari kuwa na viongozi weusi" alisema mkazi mmoja wa wilaya hiyo.

  "Ni bora akarudi Afrika akauze matikiti maji yake, hana nafasi nchini Urusi, hatuhitaji Obama mwingine hapa" alisema mkazi mwingine wa wilaya hiyo.

  Crima ambaye analonga kirusi kama kazaliwa Urusi vile, ni vigumu sana kwake kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Srednyaya Akhtuba yenye wakazi 55,000 sio tu kutokana na upeo wake mdogo kwenye siasa bali pia kutokana na kwamba yeye ni mweusi na lazima atakabiliwa na ubaguzi wa rangi.

  Mwezi disemba mwaka jana, mwanafunzi mmoja mweusi toka Marekani aliyekuwa akisoma nchini humo, aliuliwa kwa kuchomwa kisu katika mji wa Volgograd katika kile kinachoaminika kuwa ni chuki za ubaguzi wa rangi.

  Crima kwa upande wake ili kujiweka salama, wakati wote wa kampeni zake hutembea na kaka wa mke wake mzungu mwenye asili ya Armenia ambaye ni baunsa kama mlinzi wake.

  Crima ana shamba la eka 55 nchini humo ambalo amelima matikiti maji. Amewaajiri jumla ya watu 20 kumsaidia kazi za shambani. Mkewe ndiye anayeuza matikiti maji hayo.

  "Kiongozi wa wilaya hii yuko madarakani kwa miaka 10 sasa lakini hajafanya chochote cha maendeleo. Familia nyingi zinahitaji makazi, maji na barabara hakuna" alisema Crima na kuongeza "Mabadiliko yanahitajika katika wilaya hii na Urusi kwa ujumla".

  Crima alimalizia kampeni zake kwa kusema "Yes We Can" akiiga kibwatizo cha rais wa Marekani Barack Obama.


  Chanzo cha habari Nifahamishe
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  In this photo taken on Thursday, July 30, 2009, Joaquim Crima, 37, waves greeting the people in a local bus in the village of Srednyaya Akhtuba, outside Volgograd, 900 kilometers (550 miles) southeast of Moscow, Russia. The African-born farmer is making an improbable run for office in Russia, inspired by President Barack Obama and undaunted by racial attitudes that have changed little in decades. (AP Photo/Ivan Sekretarev)

  http://news.ronatvan.com/2009/08/15/joaquim-crima-a-black-watermelon-merchant-may-become-the-obama-of-russia/
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  Huyu hayapendi maisha yake nini? hizi story kama za kweli basi jamaa watamuua..ile nchi sio mchezo kule watu weusi wanabaguliwa bila kuficha....halafu atakuwa amewabip maskinhed
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha..hata mimi naona the guy is asking too much of trouble. His ambitions are too stupid and unrealistic.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  Kitu kitakacho tokea kitawaathiri hata wageni wengine manake sasa ivi tu hawaishi kwa amani ....kwanza nasikia baada ya obama kupata urais ndio balaa liliongezeka ..sasa huyu muuza matikiti si watammaliza kirahisi tu ....lakini hili ni fundisho kwa hata MIJITU inayosoma nje hasa nchi kama urusi...we angalia mwenyewe hizi ni stress wewe una degree halafu unauza matikiti maji...hehe!!! huyu ana stress .....
   
 6. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Leadership is not for the heart fainted and weaklings. Mwache ajaribu. Martin Luther King angeogopa kifo kule USA Obama angekuwa wapi? Pole pole watu weusi wanaanza kuchomoza duniani na Crima ni mmoja wapo. Sasa hivi kule Sweden kuna waziri mhamiaji toka Rwanda.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  mi sijamkataza halafu usifananishe marekani na urusi kule mablack walikuwa wengi halafu inavyoonekena humpendi huyu mwenzako...
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Mkuu naona kama una mtazamo wa kushindwa zaidi, binafsi nadhani kuwa itamuwia ngumu jamaa kukamata hayo madaraka lakini angalau atakuwa amefungua njia kwa wageni wengine waishio Urusi kuweza kutoa changamoto kwa Warusi kuwa na wao wanaweza. Mara nyingi mafanikio yoyote huambatana na kujaribu na kushindwa (Trials and Errors).

  Kuna mwanajamvi mmoja kwenye signature yake aliandika: "We miss 100% of shots that we don't take." Bora ujaribu ushindwe utapata uzoefu fulani kuliko kutokujaribu kabisa.

  Cha muhimu tumuombee mweusi mwenzetu ambaye ameweza kuthubutu.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  Kajaribu sasa na wewe unaja nini??????????????????????????????????????????????
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tatizo la watu weusi ni wagumu sana kukubali kuwa Nyumbani ni Nyumbani, na Nyumbani kwa Mtu Mweusi ni Afrika. Ukiwa ngozi nyeusi nyumbani kwako ni Afrika. Period!

  Ukililia kuishi kwenye nchi za watu inakubidi ukubali ku-suffer consequences and challenges nyingine usilalamike maana hamna atakaye-guarantee maisha yako ukiwa kwa watu.

  Hebu jaribuni kuona upinzani anaoupata Obama sasa hivi kwenye ishu za AFYA, nadhani kwa kiwango kikubwa watu wanamkwamisha kwa makusudi kabisa kwa sababu ya kijicho.

  NUKTA.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Usiwaogope Wazungu kwa kiasi hicho. Huo ni woga kama wa VIONGOZI wa CHADEMA. Kama kijana hana uwezo na wao ni Wabaguzi, si acha agombee na akione? Akipata kura 10 ndiyo atajua.

  Wazungu na waafrika ni watu pekee wakienda sehemu huwa wanajichanganya. Hawa assians ni wagumu sana na siku zote huwa wanajitenga. Waliokaa Japan wanalifahamu hili na hasa Wazungu. Ndiyo maana huko huoni hata kwenye TV wakiwaonyesha. Wazungu na Mipingo ni damudamu kabisa na ndiyo maana siku zote ndiyo Race zinazogombana na kupatana duniani. Wengine wamejikalia kimyaa......
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Sounds True!

  LOL!
   
 13. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #13
  Sep 3, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Sep 3, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Huyu si mzima huyu. Kuwa na shahada halafu kulowea huko Urusi vijijini na kuanza kuuza hayo madude ni dalili tosha kuwa ana hitilafu kichwani.
   
 15. K

  Koba JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..wewe ***** mbona uko states mwaka wa 15 na huna dalili ya kurudi huko unakokuita home,na tofauti gani na huyo chizi wa urusi?wote walowezi tuu
   
 16. K

  Koba JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...mawazo kama haya ni yale majamaa ignorant huku tunayaita KKK,tuko States almost 20 yrs na life is good kwa hiyo acha kutupangia na kuja na theory zako za kipuuzi!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Sep 3, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tofauti ni kwamba mimi nafanya kazi corporate America na huyo jamaa ni muuza matikiti maji!!

  Hela ninayotengeneza mimi wewe, bonge lako la makaratasi,
   
  Last edited by a moderator: Sep 3, 2009
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Sep 3, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nenda basi ukawe meneja wa kampeni yake .
   
  Last edited by a moderator: Sep 3, 2009
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...inategemea unafanya nini na hizo corporate america maana kuna position kuanzia Janitor mpaka CEO,mwenzako ana acre 25 za matikiti maji sio za kitoto hizo.
   
  Last edited by a moderator: Sep 3, 2009
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Sep 3, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mashirika mengi ya corporate America yanaajiri makampuni ya usafishaji kuja kusafisha maofisi yao. Huna experience na corporate America ndio maana unabwabwaja hovyo hovyo tu.
   
Loading...