Timu ya Alexei Navalny imedai mwili wake unazuiliwa makusudi na serikali ya Urusi.

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Msemaji wa Navalny, Kira Yarmysh, ameiambia BBC kuwa timu ya Navalny inaamini Vladimir Putin aliamuru kifo cha mwanaharakati huyo, ambaye bila shaka alikuwa mkosoaji maarufu wa rais wa Urusi.

Alisema: "Tunajua kwa hakika kwamba haikuwa kifo tu, ilikuwa mauaji.

"Wanajaribu kuficha athari, ndio maana hawatoi maiti kwa familia yake na ndio maana wanamficha tu wasimwone."

Yarmysh alisema hajui mwili ulipo na lini utatolewa kwa familia ya Navalny.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria za Urusi, mwili wa mfungwa unapaswa kupewa jamaa ndani ya siku mbili baada ya kifo.

Hapo awali, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema ilikataa tathmini "za upendeleo na zisizo za kweli" kutoka Uingereza kuhusu sababu ya kifo cha Navalny.

Wachunguzi wa Urusi wamesema mwili wa Alexei Navalny hautakabidhiwa kwa familia yake hadi uchunguzi utakapokamilika, kwa mujibu wa msemaji wa mwanaharakati huyo Kira Yarmysh.

Familia haijui ni wapi mwili wake umehifadhiwa
 
kwan siku mbili hazijaisha kwann wasitoe mwili wa marehemu ?
 
Back
Top Bottom