Mkuu kweli unaomba GOP wachukue White House kisa Obama amebariki ndoa za u-cameroon? kwa kifupi, u-cameroon (gays and lesbians) unaenea kwa kasi kubwa zaidi usa. Wa-usa kwa kiasi kikubwa wako very sympathetic na hawa jamaa..ss CiC afanye nini zaidi ya ku-seize the moment hasa baada ya Mitt (GOP presidential candidate) kutowaunga mkono? Binafsi siwakubali, lkn chonde chonde ndugu yangu, ukiwa usa hata kama huwakubali inabidi uwavumilie tu uwepo wao... hivyo kutumainia kwamba Obama akose another 4yrs kisa ameunga mkono same sex marriage nafikiri utakuwa unasahau makubwa aliyoyafanya kwa taifa lake. afterall, wa-cameroon hao ni meal ticket yake kuelekea WH!
Ikumbukwe kwamba ni sera zao GOP zilizopelekea kutikisika kwa uchumi Marekani hadi unemployment ikafikia double digit? Je unafahamu ni hao hao GOP waliosababisha watu wa-default mortgage zao na hivyo kuishia kuwa homeless? Je unafahamu kwamba ni hao hao GOP waliopelekea wamarekani weusi katika Gulf states, hasa Louisiana, kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao wakati wa mafuriko? GOP sera zao siku zote ni kumneemesha mwenye nacho - pure capitalists. Mbaya zaidi huyo Mitt Romney ndio hafai kabisa kuongoza hiyo nchi. Kabla hajawa gavana wa Massachusetts, Mitt kupitia kampuni yake ya Baine & Capital alisababisha watu wengi sana kupoteza ajira kutokana na policy zake (M&A, Outsoursing, Discrimination against women nk). Hapana, nafikiri Wamarekani bado wanamuhitaji Obama kuendelea kuongoza nchi yao kwa kipindi kingine cha 4yrs..sera zake kadri siku zinavyokwenda zinathibitika kufanya kazi..consumer confidence inapanda, private sector job creation inaongezeka, makampuni yaliokuwa hoi (GM, AIG, BOA, etc) yameimarika nk.