Obama atoa fundisho kwa Magufuli

Obama atoa fundisho kwa Magufuli

Wapuuzi wachache waliokuwa CCM ambao tunashukuru Mungu walijivua gamba wenyewe wakahamia kwenye kile chama chetu pendwa(tunawatakia kila kheri huko walipo) wakiongozwa na fisadi mkuu EL....sasa kazi ni kujenga chama upya na kure concile na watanzania kurudisha misingi ya chama katika matendo na ku "make this natio great again"....una swali lingine chief??
Over my dead body...[HASHTAG]#kwa[/HASHTAG] siasa zenu za majitaka na kuiba ruzuku za vyama pinzani ??????sahau kuwa great nation under ccm.haya mazingaombwe ya mtukufu ni sawa na mfamaji....
 
Kwahiyo Obama katoa katika muhula wa ngapi wa Uongozi wake
 
Obama naye ni intelectual? Huyo Obama maisha yake yote kasaidiwa na Affirmative action ambayo ni quota system USA, mpka uraisi wenyewe kaupata shauri ya quota system, kwa maana nyingine ni upendeleo maalumu wanaopewa watu weusi nchini USA, hivyo hawashindanishwi sawa na jamii ya watu wengine kama Waasia,Wazungu na wengineo!

41ZiflDe7WL.jpg
Punguzeni uongo wakati mwingine haufai katika jukwaa hili la great thinkers. Hakuna kitu kama quota system katika uchaguzi wa marais marekani angalia historia toka rais wa kwanza hadi kufikia Obama ndio utajua he is the only president who rose outside the white supremacy.
 
Salaam,

Tunaelewa kwamba Rais Magufuli ana PhD katika nyanja ya Kemia. Tunaelewa pia Barack Obama ana Juris Doctor!

Sasa Bwana Obama juzi ka-publish policy piece kwenye journal namba 2 kwa ubora duniani, Science. Cheki Hapa

Humu Obama anaongelea suala la namna gani sekta binafsi inavyoweza kutoa mchango mkubwa katika kupunguza utoaji wa hewa/gesi mkaa (Carbon dioxide) na uendelezaji wa clean energy, utakaochangia ukuaji wa uchumi wa kijani.

Sasa ningependa kuona Rais wetu mwenye PhD katika kemia akitumia muda wake katika kutoa mchango wake wa kitaaluma (intellectual contribution) katika mambo mbalimbali ya kisera ambayo serikali yake inayapigania. Kwa mfano, anaweza kuandika policy opinion kwenye journal mojawapo ya masuala ya maendeleo kuhusu 'msimamo' wake katika kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alichoandika Obama ni imani yake juu ya taifa lake kupaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Obama katoa fundisho kubwa Rais Magufuli na viongozi wengine wote duniani walio na academic credentials za kushiriki katika intellectual, policy na scientific debates; lakini utumia kisingizio cha kuwa busy na majukumu ya kitaifa.
sijaona watu wa kutengenezea sera wala machapisho kwenye nchi hii. hapa ni kanyaga twende mpaka mkae level. misingi ya uhuru wetu inajulikana na mahitaji ya watanzania wengi (kuacha wa humu JF) kula keki ya taifa kwa pamoja kwa kuhakikishiwa huduma za kijamii,uchumi na biashara,miundombinu rafiki,na usalama.digrii za uzamivu na astashahada za kupiga disco hazina nafasi kiviiiile katika maisha yetu kwa sasa. Mzee Magufuli chapa kazi huo uzamivu uliozamia unatosha sana wala watanzania walio wengi hawauhitaji sana kutoka kwako bali wasaidizi wako ni lazima wawe intellectual kama unavyoendelea kuteua.
 
Wapuuzi wachache waliokuwa CCM ambao tunashukuru Mungu walijivua gamba wenyewe wakahamia kwenye kile chama chetu pendwa(tunawatakia kila kheri huko walipo) wakiongozwa na fisadi mkuu EL....sasa kazi ni kujenga chama upya na kure concile na watanzania kurudisha misingi ya chama katika matendo na ku "make this natio great again"....una swali lingine chief??
Kama fisad si mumpeleke court ? Mnaogopa nn . Na fisad zilizoendelea je !! Tunakujua ww ni rangi ya kijani nyeupe utasema nyeusi
 
Nakuu ya JKN "kuna watu hata jambo la kijinga ili mradi limeongewa na Mzungu kwa kiingeleza wao watashangilia tu" mwisho wa kunukuu.
Acha kulinganisha elimu ya obama na vitu vya kijinga kijinga. Kwanza mwanafunzi wa harvard first year ni zaidi ya mwenye mastrz ya tz.
 
You must be crazy! And brain washed as well as drained for sure!
 
Salaam,

Tunaelewa kwamba Rais Magufuli ana PhD katika nyanja ya Kemia. Tunaelewa pia Barack Obama ana Juris Doctor!

Sasa Bwana Obama juzi ka-publish policy piece kwenye journal namba 2 kwa ubora duniani, Science. Cheki Hapa

Humu Obama anaongelea suala la namna gani sekta binafsi inavyoweza kutoa mchango mkubwa katika kupunguza utoaji wa hewa/gesi mkaa (Carbon dioxide) na uendelezaji wa clean energy, utakaochangia ukuaji wa uchumi wa kijani.

Sasa ningependa kuona Rais wetu mwenye PhD katika kemia akitumia muda wake katika kutoa mchango wake wa kitaaluma (intellectual contribution) katika mambo mbalimbali ya kisera ambayo serikali yake inayapigania. Kwa mfano, anaweza kuandika policy opinion kwenye journal mojawapo ya masuala ya maendeleo kuhusu 'msimamo' wake katika kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alichoandika Obama ni imani yake juu ya taifa lake kupaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Obama katoa fundisho kubwa Rais Magufuli na viongozi wengine wote duniani walio na academic credentials za kushiriki katika intellectual, policy na scientific debates; lakini utumia kisingizio cha kuwa busy na majukumu ya kitaifa.

Tunamshukuru na kumpongeza kwa andiko ambalo linatoa mwelekeo kwa hali halisi ilivyo sasa duniani, kwani wasipo sema wao tuko katika hatari kubwa ya dunia hii kupotea kabisa ndani ya kipindi cha miaka 25 ijayo kuna uwekano mkubwa dunia ikakumbwa na majanga makubwa kama ukame, mafuriko makubwa ya kuyeyuka kwa barafu, kuripuka kwa mitambo ya nyuklia kwa sababu ya ongezeko la joto. tulioko huku nje tunaona na tunaifahamu hali hii ni jukumu letu sote kuendelea kuhabarisha. This is a fantastic forum ever in Tanzania, big up Max, your team and all folks in this forum.
 
Salaam,

Tunaelewa kwamba Rais Magufuli ana PhD katika nyanja ya Kemia. Tunaelewa pia Barack Obama ana Juris Doctor!

Sasa Bwana Obama juzi ka-publish policy piece kwenye journal namba 2 kwa ubora duniani, Science. Cheki Hapa

Humu Obama anaongelea suala la namna gani sekta binafsi inavyoweza kutoa mchango mkubwa katika kupunguza utoaji wa hewa/gesi mkaa (Carbon dioxide) na uendelezaji wa clean energy, utakaochangia ukuaji wa uchumi wa kijani.

Sasa ningependa kuona Rais wetu mwenye PhD katika kemia akitumia muda wake katika kutoa mchango wake wa kitaaluma (intellectual contribution) katika mambo mbalimbali ya kisera ambayo serikali yake inayapigania. Kwa mfano, anaweza kuandika policy opinion kwenye journal mojawapo ya masuala ya maendeleo kuhusu 'msimamo' wake katika kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alichoandika Obama ni imani yake juu ya taifa lake kupaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Obama katoa fundisho kubwa Rais Magufuli na viongozi wengine wote duniani walio na academic credentials za kushiriki katika intellectual, policy na scientific debates; lakini utumia kisingizio cha kuwa busy na majukumu ya kitaifa.
Acha ulimbukeni, sasa akiandika Obama na Magufuli alazimishwe kuandika?
Ungemlazimisha Obama naye asiwape wananchi wake misaada ya kimbunga cha 2012 kama Magufuli alivyofanya kwa misaada ya tetemeko la Kagera ungeonekana wa maana.
 
Kuandika alishaandika akiwa shule nenda UDSM archives....huu ni muda wa [HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
Ha ha ha ha. Ukilipata hilo andiko lilete hapa nikupe Dollar 1000.
 
Hapa kuna tofauti kubwa sana, Obama ni mzao wa upendeleo maalumu kuanzia Shule, Chuoni mpka kazini inaitwa Affirmative action! Yaani watu weusi au wanaojiita weusi kama Obama, wanapewa upendeleo maalumu kwenye mambo mengi kwa mfano kuingia elite Universities kama Yale, Harvard &Co. Mzungu au Mchina inabidi akomae na kupata maksi za juu sana lkn mweusi akiwa na wastani tu anachuliwa, ni kama akina Chenge, Sumaye tu & Co. wote hawa waliingia elite Unis za USA kwa njia hiyo lkn siyo kushindanishwa kwenye uwanja ulio sawa na Binadamu wengine ktk sehemu nyingine za Dunia!
Watu wa ajabu sana nyie. Leo mnawaponda wazungu kesho mnabongoa kuweni na msimamo.
 
Ndiyo, hilo liko wazi kabisa, hata IQ ya Pombe Magufuli (PhD) wetu, kamuacha Obama kwa mbali sana!
Kuna bwana kajificha chatle kisa lugha. Mgeni akiondoka atarudi kuja kushughulikia wanaosema nchi ina baa la njaa
 
Kingereza hajui,hayo machapisho atoe kwa kisukuma ama???
Aandike kingereza kwani yeye ni lugha yake.? Acheni utumwa kwa lugha za watu sio kwa kujikomba huko agh! Hadi mnakera sas mmekazania kingereza kingereza. Wakati kiswahili chenyewe kina wshinda mnashindwa kunyoosha maneno
 
Africa tuna safari ndefu sana tukiendelea kuabudu miungu wa ulaya,ndio maana unashangaa kuona msomi anasema walifuata utafiti wa wazungu katika kupata mgombea wao!
 
Kama fisad si mumpeleke court ? Mnaogopa nn . Na fisad zilizoendelea je !! Tunakujua ww ni rangi ya kijani nyeupe utasema nyeusi
Kwa mambo EL alotufanyia watanzania ni Mungu pekee ndio mwenye uwezo wa kumhukumu hakuna mahakama ya kibinaadam yenye uwezo huo....Lowasa ametuumiza sana watanzania.
 
Unazungumzia watanzania gani? Tuonyeshe , wewe kama "mtanzania", Lowassa amekuumizaje?
 
Back
Top Bottom