Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,322
- 10,799
Salaam,
Tunaelewa kwamba Rais Magufuli ana PhD katika nyanja ya Kemia. Tunaelewa pia Barack Obama ana Juris Doctor!
Sasa Bwana Obama juzi ka-publish policy piece kwenye journal namba 2 kwa ubora duniani, Science. Cheki Hapa
Humu Obama anaongelea suala la namna gani sekta binafsi inavyoweza kutoa mchango mkubwa katika kupunguza utoaji wa hewa/gesi mkaa (Carbon dioxide) na uendelezaji wa clean energy, utakaochangia ukuaji wa uchumi wa kijani.
Sasa ningependa kuona Rais wetu mwenye PhD katika kemia akitumia muda wake katika kutoa mchango wake wa kitaaluma (intellectual contribution) katika mambo mbalimbali ya kisera ambayo serikali yake inayapigania. Kwa mfano, anaweza kuandika policy opinion kwenye journal mojawapo ya masuala ya maendeleo kuhusu 'msimamo' wake katika kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Alichoandika Obama ni imani yake juu ya taifa lake kupaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Obama katoa fundisho kubwa Rais Magufuli na viongozi wengine wote duniani walio na academic credentials za kushiriki katika intellectual, policy na scientific debates; lakini utumia kisingizio cha kuwa busy na majukumu ya kitaifa.