Obama asema huwa hapaki nywele zake rangi

Obama asema huwa hapaki nywele zake rangi

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
Obama asema huwa hapaki nywele zake rangi


151121072554_barack_obama_512x288_epa.jpg

Obama aliingia mamlakani akiwa na nywele nyeusi 2009

Rais wa Marekani Barack Obama amesema yeye huwa hapaki rangi nyele zake kuficha mvi kama viongozi wengine duniani.

Kiongozi huyo wa umri wa miaka 54 alikuwa akimjibu mwanafunzi mmoja kutoka Cambodia aliyekuwa amemuomba ushauri wa busara.
Bw Obama aliingia mamlakani 2009 akiwa na nywele nyeusi lakini miaka ilivyosonga ameanza kuwa na mvi nyingi.
Rangi ya nywele za rais huwa suala tata wakati mwingine, na viongozi wengi wamekuwa wakificha ukweli kwamba hupaka rangi nywele zao.
"Jambo la kwanza ninalotaka vijana wakome kufanya ni kuniita mzee,” rais huyo alimwambia mwanafunzi huyo.

151121072749_obamapotratits.jpg


"Huwa sipaki nywele zangu rangi, na viongozi wengi duniani hufanya hivyo (kupaka nywele rangi),” alisema. "Sitasema ni kina nani. Lakini vionyozi wao wanawajua, na wasusi pia”.
Rais Ronald Reagan, kwa mfano hakuwahi kukiri kwamba alizoea kupaka rangi nywele zake, na kinyozi wake pia hakufichua hilo.

Chansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schroeder wakati mmoja alishtaki shirika la habari kwa kudai kwamba yeye alikuwa akipaka rangi nywele zake.Obama asema huwa hapaki nywele zake rangi - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom