Obama aja Tanzania

Status
Not open for further replies.
Huo ujio lazima utajwe sana kwenye list ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne. Sitashangaa hilo poa likitajwa kama miongoni mwa ahadi za JK alizozikamilisha.

These opportunists bana...!

Kila kitu sasa kinakuwa mtaji for mission 2010!

Huu ndo wakati mzuri wa kusanua maskendo ya vigogo, maana watajitahidi kuyashughulikia fasta ili wajioshe...huh!

Ma'trafffic wa Iringa wamekuwa 'scapegoats!
 

Samahani mbona unakua hivyo jirani yako akipata ugeni si na wewe pia utanufaika na masalia....

Tafadhali punguza hasira ndugu ipo siku moja atakuja na huko pia..😉
 
usumbufu tu barabarani na kudhalilishwa na walinzi wa msafara uo, aje aende akatembelee mbuga zetu na msafara wote ainue sekta ya uchumi iliyokua imeanza kutetereka kwa global economic crunch etc

sera za marekani zishapangwa miaka mingi, obama ni kivuli tu hamna kipya anachofanya, msaada ni uleule uliopitishwa na senate hana mabadiliko anayoweza fanya, aje asije yote sawa sidhani maka ni breaking news kama mengi alivyotaka iwe
 

Hivi Mengi anaweza akanzisha habari ya kiprotoko namna hii?
Who is he by the way?.
Soma vizuri basi babaake!
 

FOR information

We earn very little in tourism since most of the companies are owned by them and bad enough is that it most of Tanzanian tourism products is sold package tours where by every thing is just being paid in generating countries. Most of the tourist come here with vouchers only.
 
Ameisaidiaje KENYA kwani huko ndio kwenye ASILI yake.........?

Lazima kuna la ziada kwenye uo ujio

Hakuna mwenye data za watalii wanaoingia Kenya tangu uteuzi wa Obama kuwa mgombea uraisi na hata kuwa raisi wa Marekani. Lakini ni jambo lisilofichika kwamba raia wengi wa Marekani wanaifahamu Kenya kuliko huko nyuma. Kwa maana hiyo jinsi safari yake ya kuja Tanzania itakapotangazwa katika vyombo vya habari vya Marekani ndivyo raia wake na wa mataifa mengine watakapotaka kufahamu Tanzania na vivutio vyake.
 
Hivi akija
tutapunguza ufisadi?
tutapunguza ukimwi?
tutajenga barabara?
tutaacha kuuziana nyumba za walipa kodi?
tutapunguza kunhyenyekea wezi?

Labda...
 

Anakuja kukagua maendeleo ya proposal ya mradi wa Kigamboni!! Wajinga ndio waliwao!!! Nduguzanguni ukiona hiyo proposed investments pale, basi jua ni mafisadi tu watapata miradi pale!!! Halafu kuna cultural heritage sites for Islamic developments, ilizua mtafaruku sana. Nchi hii bwana!!! Mbona hatuna dini katika katiba jamani!!!! Basi waweke heritages pale kwa dini zote, kama wameshaingiza suala la dini katika katiba.
 
Hivi haya mambo ya AfriCom hayaishi tu?

Americans bwana!
 

" We earn very little in tourism since most of the companies are owned by them and bad enough is that it most of Tanzanian tourism products is sold package tours where by every thing is just being paid in generating countries. Most of the tourist come here with vouchers only." .....PRODIGAL SON


Need i say more.................!!???
 
You mignt not be correct. Our people getting employment in the tourism industry is one of benefits. Secondly, hotels are being paid what they quote in their price list which compensate their cost of rendering services. By the way do you have any data to support your argument that we earn very little? I dont think so becuase I know a lot of tourist businesses owned by locals and are doing very well
 

From what i know:

-They pay for Hotels
-They pay for the vehicles taking them to parks,
-They pay for park-entry fees and game drive
-They pay for AIR transport to/from the parks
-They pay tips- if you want me to mention at all!
-And all the above said sectors employ so many.
Tanzanians.
Jamani, mnataka nini?- si lawama tu hizi!

TUJIFUNZE KURIDHIKA SOMETIMES!
 
Hell yes!! BUT,

Unajua ni magari mangapi ya serikali yanatumika kwenye ziara kama hiyo?
watumishi wangapi wa serikali wanatumika kuandaa ziara? kazi zao anafanya nani wakati huo?
posho zote za watumishi wa serikali wakati wa ziara zitakuwa Sh ngapi?
almashauri hazina bajeti za ziara, utaratibu unakuwa kwamba, mukulu anatoa taarifa kuwa tutakuja arusha, mkuu wa mkoa anawaambia wakurugenzi wote wa halmashauri walete hela ya ziara, DED anazielekeza departiment zilete kiasi fulani, haijalishi wanatoa wapi......wakuu wa vitengo inawabidi kuto hiyo fedha...hata kama ni ya elimu, maji, kilimo n.k.
 
Watanzania tufunguke macho. Ujio kama huu siyo wa kuomba misaada kama viwete. Wamarekani wana usemi wao kuwa"There is no free lunch". Hivyo akupaye lunch kuna anavyotegemea kutoka kwako. Je atakavyo Obama na wamarekani twavijua? Twaviweza?

Tuitafute Ubia katika shughuli tunazoweza kufanya na Wamarekani hawa katika hali ya usawa na siyo misaada kama zawadi. Misaada kama hiyo haitufikishi popote. Baba wa Taifa alisema Tanzania hatuna mjomba wa kutupa maendeleo. Maendeleo ya kweli tutayafuta na kuyaleta wenyewe.

Tuchngamkie tenda hii ya Obama tusiwe kama watoto wa kupokea pipi.
 
tutegemee usumbufu wa usafiri wa daradara kutokana na foreni kwa sababu ya msafara wake lakini hana jipya kwa tanzania, mwenye jipya na la kutegemea kwa tanzania ni Bwana Yesu tu hutaki ndiyo hivyo unataka sawa
 
Atakwenda kwao Kenya akiwa Tanzania? Au ameamua kupiga chenga?
 
Hakuna lolote la maana atakaloleta zaidi naona yafuatayo:-

1. Shughuli zote za kiuchumi zitasimama siku hiyo yaani foleni za magari na barabara kufungwa.

2. Viongozi wetu watachukua ujiko kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi wa 2010.

Tena huku Arusha ni heri asije kabisa maana itakuwa habari mbaya, mji hautaingilika na watu itabidi walale KIA has wa Interabnational Flight kusubiri ndege za kesho yake maana wakisema waende KIA siku ya kusafiri basi lazima watachelewa ndege.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…