kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 18,501
- 16,580
Obama kwa mara ya kwanza ndani ya Marekani ametembelea msikiti. Very good news to hear,
Obama anajenga umoja mzuri sana ndani ya Marekani.
Obama anajenga umoja mzuri sana ndani ya Marekani.
Rais Barack Obama wa Marekani
Jumatano alifanya ziara yake ya kwanza
katika msikiti nchini Marekani tangu
aingie madarakani na kutumia ziara hiyo
kupinga kauli zinazotolewa hasa wakati
huu wa uchaguzi dhidi ya waislamu.
Ziara hiyo katika msikiti mmoja wa mjini
Baltimore katika jimbo la Maryland
Obama alisema "Wamarekani waislamu
wanatuweka salama," akitoa sifa kwa
michango wa waislamu katika jamii zao.
"Ni polisi wetu, zima moto wetu. Wako
katika wizara ya ulinzi na usalama,"
alisema.
Msikiti huo wa Islamic Society of
Baltimore umekuwepo kwa miaka 47 na
una maelfu ya waumini. Obama alisema
michango kadha inayofanywa na
waislamu huku akipinga vikali lugha
inayotumiwa na wagombea urais
warepublican kama Donald Trump.
Obama ametembelea misikiti katika siku
za nyuma lakini sio ndani ya Marekani
ambako kuna waislamu karibu millioni
tatu, kulingana na kituo cha utafiti cha
Pew. Makundi mengi ya kiisalmu
yamekuwa yakimwomba atembelee msikiti
ndani ya Marekani ili kuonyesha upinzani
dhidi ya hisia zinazopinga uislamu, kama
vile Rais George Bush alivyofanya siku
chache baada ya mashambulizi ya
Septemba 11, 2001.